Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Utakoma hadi roho itakutoka, kalime upate chakula maana bwanako ndo hivyo tena hatawali tena au bado unaamini ataogezewa muda🤣🤣🤣🤣
Mimi na kula maisha tu kama kawa mkuu!! Wala sifikiri mimi ni mlalahoi kama wewe!
 
Changanya dua za wafungwa elfu tano na ushee +ndugu na jamaa za wafungwa,ukipata jumla yake,kaanayo

Kisha laana huyo bibi na kijana wake msaliti wa taifa upime mzani .
Kosa alilofanya huyu dogo kwa taifa hili alistahili kunyongwa,sema Magufuli anahuruma sana

Sent using Jamii Forums mobile app
ingefaa sasa utuambie Kabendera alifanya nn?
Tito magondi alifanya nini?
 
Hehehhehe dah nacheka kama mazuri vile. Ila dingi alikuwa ana roho inafanana na huu mmea kama unavyofanana nae. 😂😂
 

Attachments

  • 20240311_141602.jpg
    20240311_141602.jpg
    94.6 KB · Views: 3
Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.

Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.

Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.

Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”

"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.

Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.

Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.

"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."


View attachment 1291137
Halafu kuna mbwa zinaomba apumzuke kwa amani, WTF, malipo hapa hapa, baadae mbinguni, amemkuta Mama Kabendera amekaa kuume kwa bwana, wakati lenyewe likiungua moto, linaomba japo mama kabendera alipatie maji ya kunywa hata tone
 
Back
Top Bottom