Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Mama Mzazi wa Erick Kabendera amuomba Rais Magufuli kumsamehe mwanae

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426
Verdiana Mjwahuzi (81) ambaye ni mama wa mwandishi wa habari, Erick Kabendera amemuomba Rais wa Tanzania, John Magufuli kumsamehe mwanaye.

Akizungumza kwa huzuni leo Ijumaa Desemba 13, 2019 katika mkutano na waandishi wa habari, Verdiana amesema Kabendera ni mwanaye pekee anayemsaidia katika matibabu.

Kabendera anakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la utakatishaji za zaidi ya Sh173 milioni na tayari amemuandikia barua mkurugenzi wa mashtaka (DPP) kukiri makosa na kuomba msamaha. Oktoba Mosi , 2019 kupitia wakili wake Jebra Kambole, alimuomba msamaha Rais Magufuli kama kuna makosa ameyafanya.

Verdiana amesema kati ya watoto wake wanane, Kabendera ni wa saba kuzaliwa na ndio alikuwa na uwezo wa kumtunza na kumuuguza.

Mheshimiwa Rais na yeye ni mtoto kama walivyo watoto wengine hata kama ni mkubwa. Ni mzazi na analea watoto. Namwomba anionee huruma.”

"Angalia maisha yalivyo magumu, dawa sipati. Naomba Rais anisaidie kama anavyosaidia wazazi wake,” amesema.

Amesema mwanaye alijitahidi kuitunza familia yake, yeye na ndugu zake wengine na kusisitiza kuwa ndio mhimili wa familia.

"Siwezi kumsifia mwanangu, wanaume wengi wakitoka kazini wanakwenda kulewa lakini Eric anafanya kazi zake hapa nyumbani hadi saa saba usiku na wakati mwingine hadi saa nane . Mambo yote aliyopata ni kwa sababu ya kufanya kazi," amesema mama huyo huku akibubujikwa machozi.

Ameongeza, “kule Segerea (gerezani) siwezi kwenda kwa sababu kuna msongamano wa watu, mahakamani kuna ngazi. Lakini mara ya mwisho nilijitahidi nikaenda nilipomuona mwanangu sikulia, nilijikaza lakini chozi moja lilinitoka. Sikujua kama ni yeye, amekonda na ana nywele nyingi kama mwehu. Ni mweusi lakini amezidi kuwa mweusi.

"Huyu mtoto ni Mungu amenizawadia, ni tunu kwangu. Akisikia mama anaumwa anakimbia haraka. Sasa hizo dawa sizipati tena, macho yalikuwa yanauma na moja halioni tena na hili linaloona naona vitu vyeusi."

Pia, soma: Mwanahabari Erick Kabendera akamatwa na Polisi nyumbani kwake; yadaiwa anaendelea na Mahojiano

 
Ina maana kina zitto na kina maria sarungi wamemtekeleza huyu mama pamoja na kumtumia kote kule kabendera wakishirikiana na mabeberu? Ama kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Nae ajifunze akitoka, alipokuwa anatumika hakujua kuna mama na ndugu zake wanamtegemea.?Wacha ale jeuri yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimemuonea huruma sana huyu bibi na sisi watoto tujifunze tunapokuwa sehemu tujifunze tutii mamlaka tunawapa tabu sana wazazi wetu
Changamoto ni kwamba mamlaka zinajisahau kwamba zipo kwaajili ya nani,zikijitambua utii utakiwepo bila shaka.Nisawa na mama na mwanaye(Kabendera),kila mmoja anajitambua na anatambua nafasi yake kwa mwenzake.Sasa hizi mamlaka za kujimwambafy unadhani nini kinafata kama sio misuguano isiyo na ulazima?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ina maana kina zitto na kina maria sarungi wamemtekeleza huyu mama pamoja na kumtumia kote kule kabendera wakishirikiana na mabeberu? Ama kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Nae ajifunze akitoka, alipokuwa anatumika hakujua kuna mama na ndugu zake wanamtegemea.?Wacha ale jeuri yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kabla hujafa hujaumbika , hivi kama kweli Kabendera ni mtakatisha pesa huyu mama angelia namna hii ? endeleeni na ukatiri wenu lakini mtakuja kulipa tu
 
Ina maana kina zitto na kina maria sarungi wamemtekeleza huyu mama pamoja na kumtumia kote kule kabendera wakishirikiana na mabeberu? Ama kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Nae ajifunze akitoka, alipokuwa anatumika hakujua kuna mama na ndugu zake wanamtegemea.?Wacha ale jeuri yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
tena ilipaswa aliangalie hilo na akatae kutumika
 
Changanya dua za wafungwa elfu tano na ushee +ndugu na jamaa za wafungwa,ukipata jumla yake,kaanayo

Kisha laana huyo bibi na kijana wake msaliti wa taifa upime mzani .
Kosa alilofanya huyu dogo kwa taifa hili alistahili kunyongwa,sema Magufuli anahuruma sana
Naombeni mniombee

Alisikika mnafiki mmoja


Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom