Mama mzazi wa Feisal aitaka TFF itende haki


Kwa kutumia chombo gani cha kutoa haki? Hii video ya huyu Mama au Sheria?
 
Timu gani bongo imecheza saa nane mkuu,hali ya hewa ya wenzetu si kama ya kwetu,kwani hizo team kubwa kucheza saa 10 wanacheza peke yao yani bila mpinzani au zinacheza timu mbili?

IKIFIKA ISHU YA MPIRA TUONGEE KIMPIRA BASI.
Kitu ambacho jamaa hafahamu, Mechi zinaweza kuchezwa ata saa sita mchana inategemea na Hali ya hewa ya eneo husika.
Hakuna Mechi ya DAR au Pwani kwenye ligi kuu ikachezwa saa 8. Ila Ipo mikoa apa Nchini mechi inaweza ikachezwa saa 8 au Sita na kusiwe na madhara yoyote kwakua jua linawaka Kama tochi halina nguvu Wala madhara.
Vilevile mpira ni biashara mechi kubwa kuiweka saa nane ni hasara kwakua muda uo Kwa apa kwetu watazamaji watakua wachache Kwaiyo viwanjani na kwenye Luninga utakosa wa kuangalia na kukosa hamasa kibiashara.
 
Lakin pia na mwenye haki ya matangazo yeye anainfluence kubwa kwenye kupanga muda wa mechi
 
huyu maza anatakiwa kujua kua kuna taratibu na sheria inatakiwa zifuatwe..... Je ni uamuzi gani ambao ukichukuliwa na tff yeye ataona wametenda haki? aache kua na majibu yake mfukoni mwanae kalikoroga sasa alinywe. Hapo sio suala la kutenda haki ila angesema anawaomba Yanga+ tff watumie busara kudeal na hii issue.
 
Akihojiwa na chombo kimoja cha habari Mama mzazi wa Mchezaji Feisal Salum Fei Toto amelitaka shirikisho la Mpira wa Miguu kutenda haki hapo kesho.

View attachment 2534235
Inachekesha sana pale mama anaposema tu TFF itende haki, huku hasemi ni haki gani iliyopotezwa. Na si walisema kesi imepanda juu? Huko juu kuna muafaka gani umefikiwa?
 
Wewe ni muungwana gani unamdhalilisha mama wa mwenzio kisa ushabiki ambao haukupi chochote mbele ya Mungu kama kweli u muungwana hupaswi kusema mama wa mtu anajitangaza kama Malaya......kavunja sheria ya dini gani kisa kumuongelea mwanae?
 
Inawezekana kati ya watu waliompa bichwa Feisal ni pamoja na mamaye
 
Hilo liko kibiashara zaid kati ya tff na Azam ..Moja ya mashart ya Haki ya matangazo , Azam waliwaambia tff Simba ,yanga ,na Azam..zisicheze siku Moja...pia mda WA kucheza uwe tofauti na Tim zingine...hii ni kwa sababu timu hizo zinafatiliwa sana hivyo inarahisisha utangazaji WA biashara....upo?
 
Biashara za hovyo! Kama kweli mnatakq kufanya biashara katika ligi uwekezaji uwe wa kutosha kila timu inufaike sawa na wengine kama nchi zilizoendelea sio kwa matabaka.....ifikie kipindi kila timu inayoshiriki ligi iwe na mvuto wa kutazamwa na kila mtu nadhani itakuwa ni maendeleo makubwa ya hizo biashara....kama Bongo Movie KWA sasa wamepiga hatua kwenye Tamthilia(series)....kila series inayotoka kwa sasa inamvuta kila mtu kuifutilia tofauti na zamani mf,kama hizo Huba,Nyavu n.k,sasa na huku kwenye soka ifikie kipindi Ihefu vs Singida BS unakuwa mechi ya kutazamwa wasiangalie Timu 2 au 3 tu.
 
We hujui kitu....hata UEFA Kuna gem special zinazofutia watazamaji zinatengewa mda na siku maalumu.....sio kubwabwaja hapa kama jibwa kolo Waheed wewe
 
We hujui kitu....hata UEFA Kuna gem special zinazofutia watazamaji zinatengewa mda na siku maalumu.....sio kubwabwaja hapa kama jibwa kolo Waheed wewe
Aisee! Sawa mr khinzir.
 
Mama kongea kama Mama ila kaongea vitu ambavyo vinaonyesha kabisa hajui chochote kuhusu Mikataba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…