Mama Samia ameingia kwenye mtego wa wafanyabiashara kubembelezwa kulipa kodi, tumekwisha!

Kodi sio sababu ya kwanza ya kukimbiza wafanyabiashara. Hii ni hoja ya watu wajinga ambao hawakwenda shule.

Huko ulaya kuna very strict laws za kodi, umeona kama wafanyabiashara wanakimbia ulaya?
Umenena vyema kabisa
 
Kodi sio sababu ya kwanza ya kukimbiza wafanyabiashara. Hii ni hoja ya watu wajinga ambao hawakwenda shule.

Huko ulaya kuna very strict laws za kodi, umeona kama wafanyabiashara wanakimbia ulaya?
We pumba heri uache kuongea na ule serengeti lite kwa helo uliyosevu vikao!
Na mmepatikana sasa.
 
Punguza VAT tufungue biashara tulipe kodi,kama alivyofanya Mwinyi Zanzibar achana na mataga hao
 
Saivi hata ukinunua bidhaa risiti hupewi unaambiwa mashine mbovu. Soon tutaona mengi.
 
Nadhani wengi wenye maoni kama yako hamjamuelewa mama,yeye anataka mazingira mazuri ya ukusanyaji wa kodi bila kutumia nguvu nyingi, akili kidogo .
Zingatia points zifuatazo ;

1. Hataki mambo ya kubambikiziwa mikodi isiyolipika na kusababisha biashara kufungwa.
2.Hao wafanyabiashara wanaofunga biashara sababu ya kodi zisizo rafiki ,unafikiri wanapenda wafunge biashara zao?
3.Kila mwaka biashara zikiendelea kufungwa na kufungwa taifa litaendeleaje?
4. Mataifa yote duniani yanahimiza uwekezaji,kunakua na new business nyingi kila mwaka zinaongeza ajira.
5. Hujiulizi kwa nini kila kona ya Tanzania kilio kikubwa ni ajira na uhaba wa fedha mtaani? Jibu ni kwamba hamna biashara mpya zinafunguliwa ,zile chache zilizokuwepo zinafungwa kila siku .Na kama hamna ajira na hamna biashara mpya,hiyo cashflow itatoka wapi?
6. Hizo nchi ulizotolea mfano,hazikusanyi kodi kwa mabavu,wameweka mifumo mizuri ya kukusanya kodi isiyokua na double standard na kila mtu analipa kodi pale inapostahili sio kwa kushikiwa bunduki .

Wale wote wenye maoni hasi juu ya maono ya mama kuhusu biashara ,fungueni biashara ili nchi iwe na wawekezaji wengi naa walipa kodi wengi.
 
Kodi sio sababu ya kwanza ya kukimbiza wafanyabiashara. Hii ni hoja ya watu wajinga ambao hawakwenda shule.

Huko ulaya kuna very strict laws za kodi, umeona kama wafanyabiashara wanakimbia ulaya?
How strict are they ?
Tuambie
 
Unazungumza masuala ya kodi kama layman kabisa!

Ukusanyaji wa kodi ni taaluma. Huko ulaya unaowasifu kwa kukusanya kodi wanatumia wataaluma,hawaendi na bunduki kama wewe unavyopenda.

Kwa nini mnapenda kutumia mifano ya mbali wakati kuna ya karibu? Kenya,jirani zetu ambao tunafanana nao mazingira,kwa kuzingatia weledi katika ukusanyaji wa kodi,wanakusanya kodi marambili ya ile tunayokusanya sisi na task force zetu!

Acheni kumwingilia na kumpangia mama yetu. Msimuingilie,anajua anachofanya,hataki kodi za dhuluma. Na sisi watanzania wazalendo hatutaki kodi za dhuluma!

HAKI HUINUA TAIFA

Songa mbele mama,raisi wetu mpendwa mama Samia Suluhu Hassan. Tuko begakwabega na wewe!
 
Umemaliza yote Tumuombee sana huyu mama mtego mwengine mbaya zaid nicovid 19 tume ya usaliti ikiundwa tumeangamia tutaanza kuhesabu maiti kama walivyosemaga nawaza kama mzee afufuke vile ila Munguyupo kiza nene tutapita tu
 
Kodi sio sababu ya kwanza ya kukimbiza wafanyabiashara. Hii ni hoja ya watu wajinga ambao hawakwenda shule.

Huko ulaya kuna very strict laws za kodi, umeona kama wafanyabiashara wanakimbia ulaya?
Wewe umeenda shule gani ambayo ulifundishwa kwamba wafanyabiashara huwa wanabankiwa kodi? Huwa wanadaiwa kodi kwa bunduki na pingu. Huwa wanyanganywa pesa zao benki kwa mabavu?

Kama kweli ulienda shule basi hukuelimika! Ulikaa tu kwenye xhumba cha pembe none ukatoka huko na makaratasi!

Huko ulaya unakosema,naamini haujawahi hata kufika achilia mbali kukaa. Wale wako very professional. Wanahubiri voluntary tax compliance. Wanatoza kodi tu kutoka kwa watu siyo kunyanganya mitaji ya watu!
 
Acheni hoja za kijinga, TRA walichokuwa wanafanya ni unyang'anyi wa wazi tena uliokuwa na siasa ndani. Hii ndio sababu baadhi ya watu walihamisha biashara kwenda nchi jirani. Katika nchi zinazojitambua, walipa kodi hasa wale wakubwa hulindwa, na serikali huweza kutoa pesa kuwasaidia wakiyumba kibiashara.Ile task force ya kuvamia maduka kwa jina la kodi ianze kulima Viazi kwa sasa.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Kaka umeongea kila kilichokua akilini mwangu. Mstari baada mstari, neno kwa neno. Hakika ameingia mtego wa ajabu sana. Ninachojiuliza kama wafanyabiashara wanalalamika kodi na hivyo biashara nyingi zinafungwa. Mbona toka serikali ya awamu ya tano inaingia madarakani, mapato yalikua yanaongezeka kila siku hayashuki. Sasa kwanni anataka yashuke ili yapande tena? Ili iweje? Haoni kama hiyo ni kucheza bahati nasibu? Anataka kuwafurahisha kina nani?

Kwann amuondoe Kamishna wa TRA aliyeperform vizuri amrudishe mtu alieunder perform mpaka akatumbuliwa, kapelekwa ubalozini kashindwa, katumbuliwa. Leo tena unamrudisha pale? Kuna jambo kubwa sana tusilolijua kwenye hii nchi. Muda utaongea!!!!
 
Hapa kwenye issue za Kodi mama angeenda slow kidogo apokee ushauri afanye analysis ya kutosha ndo atoe matamko na maelekezo . I can see umakini mkubwa unahitajika kwenye hili maana tunaweza kuja kulaumiana badae.
Kwa hiyo unataka mama aache TRA waendelee kudhulumu wafanyabiashara? Hebu ongeza sauti kidogo.
 
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]
 
Wakati wa JK hakukua na ubabe kwenye kodi. Alikua anakusanya sh. Ngapi? Alivyoingia JPM yaliongezeka mara mbili na hayajawahi kushuka. Sasa alikua anayapata wapi na biashara mnasema zilikua zinafungwa?
 
Nchi inaelekea enzi za mzee ruksa, itafikia wafanyakazi wa nakosa salary. Awe serious na kodi.
 
mlipotumia mabavu ni kodi gani endelevu mliyoipata?
Kodi ilitoka bil. 700 kwa mwezi mpaka wastani trilioni 1.7 kwa mwezi. Hakuna kubembelezana kwenye kodi. Nchi zilizoendelea watu wanalipa kodi mpaka kero. Lakini wenzetu wamezoea coz wanajua wanachangia maendeleo yao. Huku kwetu tunataka lele mama. Haya tumempata mama wacha atulee. Muda utaongea
 
Sera za kodi huwa zinaweza kubadilishwa kwa kuangalia maeneo ya kimkakati lakini siyo kutoa 'loop holes' za watu kukwepa kodi ukidhani ndo unawavutia wafanyabiashara. Mwinyi yeye alitaka kodi zipunguzwe ili watu wengi wafanye biashara akusanye kodi lakini siyo kubembeleza wafanyabiashara. Mama kama angetaka, angepunguza tu kodi ili tuone hizo biashara nyingi zikifunguliwa tena kwenye maeneo maalum. So far makusanyo yapo juu hayajawahi kushuka, ina maana Serikali haina hasara yoyote ile. Isipokua tu angewapa ahueni wafanya biashara
 
Hii mijamaa haijui biashara zilikuwa zina kufa na mwisho serikali isingepata kodi kabisa!
Isingepata kodi wapi? Toka kelele zimeanza kupigwa, ndo kwanza mapato yalikua yanaongezeka kila mwezi. Kwa ufupi, mama kaingia mtegoni, huku kwenye kodi asingepagusa kabisa. Miradi yote itasimama, tutaanza bakuli tena.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…