Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa

Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa

"Lakini nataka niwaambie kwamba katika wakati muhimu watanzania kushikamana ni wakati huu, kujenga umoja, ni wakati huu. Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje nasi yakatuparaganya vichwa."

Ahsante Mama tumekuelewa pamoja na kwamba wengine hawatakuelewa.
 
My take:

Sasa hivi kuna power struggle ndani ya chama chetu. Mama kagundua anaweza kuwa side-stepped na MATAGA gang.
Speech yake ya leo ni kilio kwa Watanzania wote (hususani wasio wafuasi wa chama chetu na wasio MATAGA gang) wamuunge mkono ili asienguliwe na hao wahafidhina.

It's there for all to see and hear!
 
Dah.. kwa maneno ya TL huko Twitter, basi kweli dunia ni mapito tu jamani. Cha muhimu hapa duniani ni kuishi vizuri na watu na kufata misingi aliyoiweka Muumba basi!! Hakika hatuijui kesho yetu. Inasikitisha sana sana.
 
Hii ziara naona muhimu sana kwa Taifa, Yaani Leo Mama Kaongozana na Mawaziri na Manaibu waziri, tulishazoea hiyo hali inakuwepo Jiwe akiwa kwenye shughuli za kuijenga nchi.
Muda muamuzi wa kweli
 
E86BFD4D-D3FA-48AF-ACA8-6053B89BCB58.jpeg


Jamaa wa kaunda suti kibao, wengi leo wamekuja kivingine.
 
Yaani, yaani ugali wangu haushuki tena! Mama, tushikamane kwa sababu gani? Nani anakaguliwa kaguliwa afya? Yaani mwili wote umelegea! Mama, kwa nini unaongea kwa mafumbo? Kuna nini? Mbona mnataka tufe kwa kihoro jamani? Tupo tayari kupokea taatifa yoyote. Tuambieni tu jamani? Tunaumia jamani!
 
Yaani, yaani ugali wangu haushuki tena! Mama, tushikamane kwa sababu gani? Nani anakaguliwa kaguliwa afya? Yaani mwili wote umelegea! Mama, kwa nini unaongea kwa mafumbo? Kuna nini? Mbona mnataka tufe kwa kihoro jamani? Tupo tayari kupokea taatifa yoyote. Tuambieni tu jamani? Tunaumia jamani!
Time will tell.usipaniki
 
Mama Samia Suluhu tuko pamoja Huyu mama Magufuli akimaliza kipindi chake cha uraisi apewe uraisi ana akili nyingi mno nampendekeza ugombea uraisi najua kuna makundi ya nje yamekaa kama fisi kwenye bucha yakisubiri muuza bucha atoke yale Nyama hayatafanikiwa.

Bucha haitaachiwa fisi wa nje hata siku moja! meseji ndio hiyo Kila fisi wa nje anayedhani atapewa bucha hapewi kwa gharama yeyote awaambie fisi wenzie

Tanzania ni Tanzania na itabaki kama Tanzania ya watanzania milele.
 
15 March 2021
Tanga, Tanzania

Ziara ya Makamu wa Rais mkoani Tanga

Nukuu ya salamu za Mh. Makamu wa Rais akizungumza na wananchi wa Mkata wilayani Handeni mkoani Tanga aliposimamishwa kusalimia wananchi :

Makamu wa Rais : " ...kumekucha ....Ziara hii niliipanga nije kabla yaani mwezi wa pili ... lakini nikaighairisha ila nashukuru leo imetimia nimeweza kufika Tanga ... miradi yote aliyoahidi Rais ...muda hautoshi ndugu zangu wa Mkata Hadeni..mmenisimamisha niwasalimie ila nawahakikishia waTanzania tupo salama, ni kawaida ya wanadamu kukaguliwa kaguliwa mara mafua mara homa .. au chochote kile ....ila nataka niwaambie ..." mwisho wa nukuu.
 
Mama Samia Suluhu tuko pamoja Huyu mama Magufuli akimaliza kipindi chake cha uraisi apewe uraisi ana akili nyingi mno nampendekeza ugombea uraisi najua kuna makundi ya nje yamekaa kama fisi kwenye bucha yakisubiri muuza bucha atoke yale Nyama hayatafanikiwa.Bucha haitaachiwa fisi wa nje hata siku moja! meseji ndio hiyo Kila fisi wa nje anayedhani atapewa bucha hapewi kwa gharama yeyote awaambie fisi wenzie

Tanzania ni Tanzania na itabaki kama Tanzania ya watanzania milele.
Nimekusoma mjomba ✔️
 
Kifupi miifisi ya nje ya nchi inayodhani Magufuli akiondoka 2025 au kabla kwa sababu yeyote itashika nchi .Wasahau Tanzania ni ya watanzania full stop.Wapeni huu ujumbe mafisi wote wa nje .Kuwa Tanzania ni ngome ya chuma isiyopenya fisi

Kila silaha ya fisi haitafanikiwa juu ya Tanzania .Hii habari mfikishieni yule fisi mbwa mkubwa
 
Back
Top Bottom