Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa

Mama Samia: Katika wakati muhimu Watanzania kushikamana ni wakati huu, Si wakati wa kusikiliza maneno yanayotoka nje yakatuparaganya vichwa

"Niwashukuru kwamba nimeweza kusimama tumesalimiana, ninalotaka kuwahakikishia ndugu zangu, Tanzania tuko salama, Tanzania tuko salama. Ni kawaida ya mwanadamu kukaguliwa kaguliwa, mara mafua, mara homa mara chochote kile"

Maneno haya Mama yetu mbona yanaleta maswali sana, Anashukuru ameweza kusimama? Mbona hatujawai pewa taarifa yoyote kua alikua anaumwa? Au kusimama kwa namna gani? Maana hiyo ziara imeandaliwa muda maana ake alijiandaa kwa hilo.

Huyu aliyekaguliwa kaguliwa ni yupi?

Yaani Leo mama yetu kasafiri kutoka DSM ili kuja kutuhisia watanzania tuwe na umoja na kushikamana kipindi hiki. Hiki kipindi anachokisema mama yetu ni kipindi cha namna gani?

Maana huku sisi tunaendelea kujifukiza, na kushagilia nchi yetu pamoja kua dunia inakubwa na korona sisi uchumi umepanda hadi uchumi wa kati.

Leo sijamuelewa kabsa Mama Yetu
Naanza kuamini kuwa akina @Chahali na ile story You Tube na Kigogo Tweer wametuingiza chaka.
 
🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔🤔

Things Fall apart by Chinua achebe
 
Mihimu wandugu ni mshikamano, madhanio Kama haya sio nadra kuwepo katika jamii, si busara kuyashikilia.
Kila mmoja kwa nafasi yake afanye linalo mpasa Hali ya kua Mungu amekua kipaombele kwetu.
 
Machozi ya Abood aliyolia kwa Allah tena kwa uchungu alivyodhalilishwa hadharani Moro Mungu ameyasikia nakuyafanyia kazi.
 
Dah.. kwa maneno ya TL huko Twitter, basi kweli dunia ni mapito tu jamani. Cha muhimu hapa duniani ni kuishi vizuri na watu na kufata misingi aliyoiweka Muumba basi!! Hakika hatuijui kesho yetu. Inasikitisha sana sana.
kasemaje tena?
 
Mama hapa kuna kitu alitaka kuongea ,lakini hakumalizia.Wanasema'',Samaki anayo mengi ya kuongea lakini mdomoni ana maji''.
9C5779DA-6D01-4CCC-AB24-173B15C1E738.jpeg
 
Kifupi miifisi ya nje ya nchi inayodhani Magufuli akiondoka 2025 au kabla kwa sababu yeyote itashika nchi .Wasahau Tanzania ni ya watanzania full stop.Wapeni huu ujumbe mafisi wote wa nje .Kuwa Tanzania ni ngome ya chuma isiyopenya fisi

Kila silaha ya fisi haitafanikiwa juu ya Tanzania .Hii habari mfikishieni yule fisi mbwa mkubwa
Ukiitaka Tanzania ya Magufuli baada ya muda wake. Omba mungu PM ateuliwe VP (whilst acting as the president) na Jaffo/Biteko awe PM hao ndio waliomuelewa.

Mama Samia abaki ceremonial president kama katiba inavyompa mamlaka should anything happen to Magufuli.

Vinginevyo andika maumivu hakuna namna ni gombania goli upya.
 
WABONGO NAONA MNAANDALIWA KISAIKOLOJIA TENA LIVE TBC KILA MWANANCH ASKIE KAANZA KUWA ELEZA KUWA NI KWELI PREZDAAA ANAUMWA NI KAWAIDA SASA NEXT TIME ANAKUJA KUWAAMBIA UKWELI WAKATI NYI BONGO ZEN ZI RECALL KWAMBA MAMA ALISEMA ALIKUWA ANAUMWA NAONA HALI ILIKUWA MBAYA
 
15 March 2021
Michungwani, Korogwe
Tanga
Tanzania

RAIS MAGUFULI ANAWASALIMIA, Anasema TUPO SALAMA" - MAKAMU wa RAIS..

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameanza ziara yake ya Siku 5 mkoani Tanga ambapo leo Machi 15 ameweka jiwe la msingi kwenye jengo la Halmashauri ya Pangani na Kiwanda cha matunda.
 

🤣🤣🤣🤣🤣🤣mdomo ndembe ndembe umejaa maji! Nani kaujaza maji mdomo wa Samaki? Hahahahaha
Mama hapa kuna kitu alitaka kuongea ,lakini hakumalizia.Wanasema'',Samaki anayo mengi ya kuongea lakini mdomoni ana maji''.
 
Wakati Tundu Lissu amepigwa risasi na watu wanataka kufanya maombi mlikuwa mnatawanya watu kwa mabomu ya machozi.
Sasa hivi anakaguliwa mafua binadamu wenu mnataka mshikamano kwa taifa.
Yaani taifa lishikamnae na watesi, wauaji. Tushikamane kwa lipi?
 
Back
Top Bottom