Hii taarifa kama itakuwa ni kweli
Basi makonda soon anaenda kuwa soon mbunge wa kigamboni
Kumbuka Ubunge unapingwa Mahakamani .
Lisu amerudi na watu wana data zote za lile jina halisi la yule mtu.
Yeye asubiri uteuzi tuu lakini sio ubunge wa kuchaguliwa.
Alikosea sana huyo kijana .
Nitaamini kabisa kuwa nchi hii kuna ukabila na urafiki mkubwa katika utawala.
Huyo kijana alipewa heshima kubwa sana kupewa ukuu wa mkoa wa DSM. Ni mtu asiyefaa tu na mwenye tamaa anayeweza kuacha nafasi ya ukuu wa mkoa mkubwa kama DSM na kukimbilia Ubunge wa jimbo. Tamaa tu ndiyo inayomwandama. Na yote hiyo ipo wazi huyo mtu sio msafi ndio maana anakimbilia Ubunge mana kula ukishachaguliwa hakuna kutumbuliwa.
Umri wake bado ni mdogo alikua na nafasi ya kumsaidia mh. Rais kwenye nafasi yake aliyoaminiwa ya Ukuu wa mkoa na baada ya miaka kumi angegombea Ubunge baada ya Rais kustaafu.
Sasa amekimbia kazi iliyompa umaarufu na kukimbilia Ubunge akilenga Uwaziri.
Na pia tunatatizo la kuwa na nchi inayoamini katika kutumia nguvu kwa kila kitu badala ya akili ndio maana kila mtu analenga ubunge na uwaziri na utawala ili awaendeshe watu kama Punda na sio kama watu wenye akili ya kukosoa na kutoa wazo mbadala.
Makonda hastahili kabisa kabisa kumtoa Ndungulile kwenye Jimbo kwa sababu tu ya kabila lake.
Noo,tusiwe na taifa la namna hiyo. Alipewa heshima kubwa sana kuwa mkuu wa mkoa mkubwa kuliko na wenye pato na mipango mikubwa sana kuliko hata baadhi ya Wizara. Sasa anataka nini ? Wakati wapo vijana wengi sana wa umri wake ambao hawana ajira na wana maisha magumu sana na wengi wana Elimu na uwezo mkubwa kuliko yeye.
Kama Makamu wa Rais anaona huyo Makonda basi amrudishe kwenye kazi yake ya awali kwenye Chama na Serikali.
Uchaguzi huu CCM wasiubeze sana. Huku uchaguzi ndio utakaoamua urahisi au ugumu wa Rais atakayekuja wa awamu ya sita 2025- 2030. Wakiwapuuza wajumbe basi wanaweza wakawapitisha watu wao mwaka huu ila 2024 CCM itapasuka vibaya sana na Lisu atachukua nchi kirahisi au Membe.
Wajumbe ndio wanaopiga kampeni Nyumba kwa nyumba,kitanda kwa kitanda.Mkitumia mamlaka yenu kuwapuuza wajumbe mjue mtawatisha wale wagombea lakini wapiga kura watasikiliza kauli za wajumbe.
Wajumbe wanapiga kura kutokana na maoni ya wananchi wanaowazunguka mana wao ndio wanaowajua. Ndio maana wote walioshindwa hakuna mwananchi anayelalamika zaidi ya wao wenyewe.
Kama ubunge una maslahi na ulinzi mzuri kuliko Ukuu wa mkoa basi tujue kabisa hata Huyo mtoto wa mkulima Dr .Andungulile naye anautaka na aliutafuta kwa nguvu zake mwenyewe bila kubwa wakati mwenzake anataka kubebwa na alibebwa pia na uRC wake.
Mungu atuepushie mbali na vijana wadogo wenye tamaa Kali kama huyo Paulo. Watu wanatamani hata ukatibu tarafa hawapati tena wana mpaka Digrii za masters.
Nitashangaa sana kama watamuacha mtu makini aliyepigania hilo jimbo la Kigamboni mwaka 2015 wakati ule wa mafuriko eti kwa sababu ya utabiri wa umakamu wa Rais. Hivi waafrika tumelogwa na nani?
Kusema tu kuwa Fulani unafaa kuwa Dereva au mvuvi basi inatosha kupuuza maoni ya Wajumbe zaidi ya 400?
Hapana Demokrasia iheshimiwe kwa kweli .
Kwanza hatukupewa nafasi ya kuwasikiliza kuwa ni kwa nini wameamua kugombea Ubunge na wana mikakati gani ya zaidi.!!