Mama Samia: Paul Makonda alisimama ndani ya Bunge la Katiba na kusema mimi nafaa kuwa Makamu wa Rais na Bunge zima likashangilia!

Mama Samia: Paul Makonda alisimama ndani ya Bunge la Katiba na kusema mimi nafaa kuwa Makamu wa Rais na Bunge zima likashangilia!

Makamu wa Rais mama Samia Suluhu amesema ni Paul Makonda ndiye aliyemtabiria kuwa makamu wa Rais baada ya kusimama ndani ya bunge la Katiba na kusema " huyu mama ndiye anayefaa kuwa makamu wa Rais wa JMT "

Mama Samia amesema hayo katika kongamano la Wasichana lililofanyika katika ukumbi wa JKNCC jijini Dsm leo.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!

Huyu Mama nilikuwa namheshimu na sikuwahi kuwaza kuwa kumbe nae ni Mnafiki mkubwa hivi. Kuna tukio liliwahi Kumtokea miaka miwili iliyopita ambapo Mpangaji Mkuu wa Tukio zima hilo ni huyu huyu ambaye leo ' anajikomba ' Kwake kujifanya ' anamsifia ' hivi. Sasa leo anamuona kuwa ndiyo ' aliyemtabiria ' kuwa hapo kwanini zaidi ya mara mbili alikuwa akimsemea kwa Baba yake Mpendwa kuwa hamuheshimu na anamdharau?
 
Mama anasema alifanya vizuri kwenye Bunge la katiba kiaje.

Mpaka leo hatuna katiba mpya wala hayo matunda waliyosimamia vizuri kama anavyodai.

Zaidi anapaswa kujuta kuomba radhi kuwa walikula posho za bure kwa kazi tuliyowatuma ambayo hakufanikiwa.
 
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu amesema ni Paul Makonda ndiye aliyemtabiria kuwa makamu wa Rais baada ya kusimama ndani ya bunge la Katiba na kusema " huyu mama ndiye anayefaa kuwa makamu wa Rais wa JMT "

Mama Samia amesema hayo katika kongamano la Wasichana lililofanyika katika ukumbi wa JKNCC jijini Dsm leo.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!
ametumwa huyu mama, si bure!
 
[SUP]Huyu makamo wa Rais speech nikuhusu yeye mwenyewe tu, hata ile kutembea na mikasi hatumuoni kama waliomtangulia. [/SUP]
 
Hahaha sheikh wa mkoa ajiandae, au aombe uamisho akawe sheikh wa mkoa wa huko mbali, maana kiranja wao anarudi hivyo.
 
CCM wakipuuza Demokrasia ya vyama vingi wao ndio watakaoumia zaidi.

Mfano Dr.Ndungulile akipigwa Chini itabidi abakie ndani ya CCM mana hana pa kwenda .
Ataugulia rohoni tu kama mtu aliyewekewa Lock down ya Corona.

Hofu na kufungiwa ndani ya Chama kimoja itawaua wengi kisiasa na kuwadhoofidha kisiasa au hata kiafya.
 
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu amesema ni Paul Makonda ndiye aliyemtabiria kuwa makamu wa Rais baada ya kusimama ndani ya bunge la Katiba na kusema " huyu mama ndiye anayefaa kuwa makamu wa Rais wa JMT "

Mama Samia amesema hayo katika kongamano la Wasichana lililofanyika katika ukumbi wa JKNCC jijini Dsm leo.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!
Ilikuwa kabla hajamshindilia magumi Mwenyekiti wa Time ya Katiba na ni Wabumge wa CCM kama kawaidà yao hawatumii akili kufikia uamuzi wowote Mwanachama wao au Chama ndo wote walishangilia. Mama anatoa agizo toka juu kutaka afikiriwe kupendekezwa baada ya kibarua kupotea ikiwa ni fadhila kwa mhusika kupokea agizo toka juu kufanikisha kuteuliwa kwake. Msg sent and received ndo maana hata Ofisi hajakabithi akitegea uamuzi wa mwisho unaotegemea siku maana siku zote si sawa.
 
Hii taarifa kama itakuwa ni kweli

Basi makonda soon anaenda kuwa soon mbunge wa kigamboni
Kumbuka Ubunge unapingwa Mahakamani .
Lisu amerudi na watu wana data zote za lile jina halisi la yule mtu.
Yeye asubiri uteuzi tuu lakini sio ubunge wa kuchaguliwa.
Alikosea sana huyo kijana .

Nitaamini kabisa kuwa nchi hii kuna ukabila na urafiki mkubwa katika utawala.

Huyo kijana alipewa heshima kubwa sana kupewa ukuu wa mkoa wa DSM. Ni mtu asiyefaa tu na mwenye tamaa anayeweza kuacha nafasi ya ukuu wa mkoa mkubwa kama DSM na kukimbilia Ubunge wa jimbo. Tamaa tu ndiyo inayomwandama. Na yote hiyo ipo wazi huyo mtu sio msafi ndio maana anakimbilia Ubunge mana kula ukishachaguliwa hakuna kutumbuliwa.

Umri wake bado ni mdogo alikua na nafasi ya kumsaidia mh. Rais kwenye nafasi yake aliyoaminiwa ya Ukuu wa mkoa na baada ya miaka kumi angegombea Ubunge baada ya Rais kustaafu.
Sasa amekimbia kazi iliyompa umaarufu na kukimbilia Ubunge akilenga Uwaziri.

Na pia tunatatizo la kuwa na nchi inayoamini katika kutumia nguvu kwa kila kitu badala ya akili ndio maana kila mtu analenga ubunge na uwaziri na utawala ili awaendeshe watu kama Punda na sio kama watu wenye akili ya kukosoa na kutoa wazo mbadala.

Makonda hastahili kabisa kabisa kumtoa Ndungulile kwenye Jimbo kwa sababu tu ya kabila lake.
Noo,tusiwe na taifa la namna hiyo. Alipewa heshima kubwa sana kuwa mkuu wa mkoa mkubwa kuliko na wenye pato na mipango mikubwa sana kuliko hata baadhi ya Wizara. Sasa anataka nini ? Wakati wapo vijana wengi sana wa umri wake ambao hawana ajira na wana maisha magumu sana na wengi wana Elimu na uwezo mkubwa kuliko yeye.

Kama Makamu wa Rais anaona huyo Makonda basi amrudishe kwenye kazi yake ya awali kwenye Chama na Serikali.

Uchaguzi huu CCM wasiubeze sana. Huku uchaguzi ndio utakaoamua urahisi au ugumu wa Rais atakayekuja wa awamu ya sita 2025- 2030. Wakiwapuuza wajumbe basi wanaweza wakawapitisha watu wao mwaka huu ila 2024 CCM itapasuka vibaya sana na Lisu atachukua nchi kirahisi au Membe.

Wajumbe ndio wanaopiga kampeni Nyumba kwa nyumba,kitanda kwa kitanda.Mkitumia mamlaka yenu kuwapuuza wajumbe mjue mtawatisha wale wagombea lakini wapiga kura watasikiliza kauli za wajumbe.

Wajumbe wanapiga kura kutokana na maoni ya wananchi wanaowazunguka mana wao ndio wanaowajua. Ndio maana wote walioshindwa hakuna mwananchi anayelalamika zaidi ya wao wenyewe.

Kama ubunge una maslahi na ulinzi mzuri kuliko Ukuu wa mkoa basi tujue kabisa hata Huyo mtoto wa mkulima Dr .Andungulile naye anautaka na aliutafuta kwa nguvu zake mwenyewe bila kubwa wakati mwenzake anataka kubebwa na alibebwa pia na uRC wake.

Mungu atuepushie mbali na vijana wadogo wenye tamaa Kali kama huyo Paulo. Watu wanatamani hata ukatibu tarafa hawapati tena wana mpaka Digrii za masters.

Nitashangaa sana kama watamuacha mtu makini aliyepigania hilo jimbo la Kigamboni mwaka 2015 wakati ule wa mafuriko eti kwa sababu ya utabiri wa umakamu wa Rais. Hivi waafrika tumelogwa na nani?
Kusema tu kuwa Fulani unafaa kuwa Dereva au mvuvi basi inatosha kupuuza maoni ya Wajumbe zaidi ya 400?
Hapana Demokrasia iheshimiwe kwa kweli .
Kwanza hatukupewa nafasi ya kuwasikiliza kuwa ni kwa nini wameamua kugombea Ubunge na wana mikakati gani ya zaidi.!!
 
Makamu wa Rais mama Samia Suluhu amesema ni Paul Makonda ndiye aliyemtabiria kuwa makamu wa Rais baada ya kusimama ndani ya bunge la Katiba na kusema " huyu mama ndiye anayefaa kuwa makamu wa Rais wa JMT "

Mama Samia amesema hayo katika kongamano la Wasichana lililofanyika katika ukumbi wa JKNCC jijini Dsm leo.

Source TBC

Maendeleo hayana vyama!
Na yeye leo anajaribu kutuambia Makonda anafaa kuwa nani?
 
Tuleteeni makonda kigamboni iwe km Paris

Nyie wajumbe wa jf msituletee uchawi,

Naamin kamati kuu ndo kila kitu na watatuletea mtu wetu,

Kigamboni itawaka moto,
Hivi Mbunge ana nguvu kuliko Mkuu wa Mkoa ?
Tena mkoa kama DSM.?
Hujui kuwa akitokea mkuu wa mkoa mtoto wa baba kama alivyokuwa yeye basi hawezi hata kufurukuta kwenye hilo jimbo!!
Mkuu wa mkoa wa DSM ni mtu mkubwa sana ! Ni mbunge gani anaweza kumwita Mfanyabiashara na kumpa kazi yoyote anayoitaka ifanyike na ikafanyika!!
Mkuu wa mkoa wa DSM hata mawaziri wanamuheshimu.
Hapo sasa tutaanza kutafsiri ukabila lakini sio vinginevyo. Kijana anachagua anachotaka yeye na sio jamii au mkuu wa nchi aliyempa kazi ya kumsaidia kujenga mkoa wake na anakimbilia jimbo tena lililokua Tarafa tu miaka ya nyuma.
Acheni kusifia mambo yasiyofaa.
Wajumbe wameona Ndungulile anafaa kuendelea na ni mwanachama wa CCM sisi tuheshimu maamuzi yao.
Na mwenyekiti alisema mahali penye Mbunge wa CCM atakayepitishwa kuendelea basi asipingwe. Yani yeye ni Mbunge aliyepo tumkate ili asubiri uteuzi wakati kuna mtu mwenye tamaa amekataa uteuzi na Ubunge ukamkataa kwenye kura za maoni.
Huku kubwebwa namna hii ni ili tu afaidi kodi za watanzania au ni kwa manufaa ya nani?
Ndio maana nchi zetu tunarithishana visasi.

Akitokea Rais mwingine huko mbeleni ndio maana Mara nyingi Mali za watu kama hao zinafanyiwa figisu mpaka wafilisike mana wanaonekana wazi walikua wanatafutiwa namna ya kula kodi ya wananchi huku wengine wakionekana hawafai na wanakatwa bila sababu.

October ni uchaguzi wa Vyama vingi kumbuka hilo ,CCM.
 
Kwa hii airtime ya kujadiliwa anayopewa mtu wa aina hiyo inathibitisha nchi imerudi nyuma zaidi ya miaka 40. Kwa sifa zipi za akili, hekima na busara achilia mbali uongozi? Typical banana republic!
 
Aliyetabiri huyo mama kuwa makamu wa Rais ni Marehemu Samuel Sitta nilikuwepo ukumbuni asitudanganye..
 
Nakumbuka......
Ni Mh.Makonda aliye sema Simba jike.
Nadhani...
Hiki kipande cha kusema Mama anafaa kuwa VP kilipangwa na mtekelezaji akachaguliwa kuwa Mh.Paul Makonda.
Naomba.......
Shule tulizo soma ziheshimiwe na elimu tuliyoipata ithaminiwe
 
Back
Top Bottom