Mama Samia Suluhu karibu Nairobi, kweli umedhamiria kurekebisha

I like this part, " The Tanzania Head of State will be seeking to lure Kenya’s business community to consider investments in the neighbouring country. "
Si mje tu! Kwani kuna tatizo gani? Kama sisi tunaweza kuwa wamachinga na omba omba kwenu kwanini nyie mshindwe huku kwetu.

Ila mkija msituzingue. Maparachichi yetu myabrand kama product of Tanzania na yaende ulaya kupitia hapa hapa. Tunandege za kutosha na viwanja vya kutosha.

Napia muache kusema kila kitu kizuri cha Tanzania ni chenu. Mnakera sana! [emoji23]
 
Ona venye ulivyo fala, kwani hamjui kubrand ndiyo mtegemee wakenya kuwafanyia branding?
 
Ona venye ulivyo fala, kwani hamjui kubrand ndiyo mtegemee wakenya kuwafanyia branding?
Nyie janja yenu ni janja ya nyani tu. Safari hii tumewaonea huruma tu. Mtake msitake. Mama ni muugwana sana ndo maana kaona aware chance mapema. Mkizingua tu imekula kwenu. Hii nafasi haitojirudia.
 
Mazungumzo ndio kila kitu dunian, Mama Anafanya vizuri, Bado USA,CANADA,European Union, England, China,na nyumbani waweke kitako wajue wajue unataka wafanye nini, Tunataka BIASHARA zifufuliwe ili watu wapate ajira, mtaani hali ni ngumu sana, Tunaomba BOT izipe kampuni ambazo zina return ya zaidi ya Bilion moja kwa Mwaka mikopo isiyo na riba kwa miaka 5 ili zipite ktk kipindi hiki kigumu
 

Kwa namna alivyoanza huyo mama naona atakua na kundi la washauri wazuri tu, kwanza keshaanza kuwekana sawa na upinzani Tanzania, halafu papo hapo ameamua kurekebisha mahusiano ya kimataifa na majirani pia. Kwenye jopo la washauri wake kutakua wadau waliokua wanasubiri sana fursa za kushauri, na hapo hata kiuchumi ataweka sawa sana.
 
Waziri wa mambo ya Nje ni Mama mzoefu sana kwenye Diplomasia ya kawaida na ya uchumi, pia Raisi anaonekana ni mtu mwenye maono makubwa sana ya maendeleo hivyo atachagua team Nzuri. Mungu amsaidie
 
Hawa Kenge ni wapumbavu sana! Wanafikiria wao tu ndo wanaongea vernaculars!



wengi wenu hamjui vernaculars zenu. Mnaogopa kuzizungumza hadharani maana mtaitwa wakabila. Watoto wenu wanazaliwa na kukuwa watu wazima bila kujua kuzungumza lugha zao za asili eti kwa sababu lugha hizi zimedhalilishwa na kudharauliwa sana huko TZ. Na aliyeleta hii dhana potovu ni Mwalimu Nyerere mwenyewe. Lugha hizi zinachukuliwa kama takataka huko TZ.
Yeyote anayeizungumza hata anaweza kutiwa mbaroni na polisi kwa kisingizio kwamba yeye ni mkabila.

Cc MK254
 
wanaoishi mijini tu na tena wale wa baba na mama makabila tofauti na wasiofundisha watoto wao lakini nakuhakikisha over 75% can speak their vernaculars! Nenda majumbani kwao ndo utajua hujui!
 

Nilishangaa na kuona huruma sana unakuta mbaba mtu mzima kabisa lakini lugha yake ya asili hawezi hata kusalimia, japo kidogo wanaotokea mikoani kama Moshi, Mwanza na Kagera hujaribu jaribu lakini wengi wa hapo Dar ni hovyoo kabisa, wamemezwa na mambo ya Uswahilini mpaka wamekua watumwa wasiokua na asili yoyote, mtu hajui lugha yake ya asili na pia uandishi wa Kiswahili ni umagumashi, Kingereza ndio hajui chochote kabisaaaa.

Wanakuambia kuongea Kingereza ni ukoloni, kuongea lugha ya asili ni ushamba, na hata hicho Kiswahili bado anayumba yumba kwenye uandishi. Kile hunishanga, mtuhumiwa akikamatwa kwenye uhalifu wowote hutajwa kabila lake kwenye dodoso, check hii...

 
Hawa watu hawaeleweki. Wanasema kwamba wao sio wakabila ila wanataja kabila la mtu waziwazi? Huo ni unafiki wa hali ya juu. Kama wao sio wakabila basi wasitaje kamwe kabila la mtu.
 
Ukiona maadui zako wanakusifu, tafakari — By JPM.

John Pombe Joseph Magufuli.
 
Mama hana mda wa kufanya ushamba na upuuzi wa mwendazake,anasaka pesa uchumi wetu urudi tena kwenye viwango kama zamani.

May day kamuumbua mwendazake Jiwe na wapambe wake kwamba uchumi umeshuka kwa 4.7% kwa sababu ya covid wakati Jiwe lilikuwa liongo liongo,tunashukuru kwa kusema ukweli.Kila la heri huko ziarani
 
mkuu, Kenya ina makampuni 529 ndani ya Tanzania, against Tanzania's 23 ndani ya Kenya kufikia mwaka 2016.
I hope you know what I mean.
Sio jambo la ajabu given the historical background of the two countries with their path each country took.

Ko wakenya walifunguka mapema ,tunahitaji tujifunze kwao kwa kufanya biashara nao
 
Hehehe!! Yaani tu, duh....nimejikuta nacheka sana, ila sidhani kama tatizo lipo kwa viongozi wao, hii ni wao wenyewe wajilaumu, hawana ule uthubutu, waoga waoga sana hawa ndugu zetu.
Historia yetu ya njia ya uchumi ndio ilitugharimu.

******** badala arekebishe makosa ya JK akaturudisha enzi za Nyerere ikafika mahali kitaani biashara haziendi vijana wanasubiri ajira za.serikali ambazo hazipo.

Wanawake wajiajiri kudanga.Nakumbuka kipindi cha JK watu walikuwa wanaacha Kazi government wanaenda kujiajiri,ile spirit ya kujiamini kwa kujiajiri ilianza kujengeka jamaa kaja kuharibu kila kitu eti anajenga stand.

Mama anajua hali ya mtaa ni ngumu sana kama haijawahi kuwa kwenye biashara eti leo uanzishe biashara na vimitaji vidogo vya start ups inakufa hata miezi 6 haijafika maana purchasing power hakuna,TRA na Halmashauri wanapora mtaji yaani tabu tupu.
 
Mkileta retail kama hizo malls mtafunga wenyewe ,,middle class Tzn ni kama hakuna na purchasing power imeshuka Sana labda awamu ya pili ya Mama akijitahidi kurudisha pesa kwa watu.

Mkiwa na Rais aliyekulia kwenye umaskini huko kijijini na akalelewa na mzazi wa kambo wanakuaga na roho mbaya,makatili na wasiojali .

Hicho ndicho alikuwa yule mwendazake,Sadamu na watu wote wenye shida ya malezi,kama ni mke ukioa wa hivyo jiandae kufa mapema Sana sasa mama amekulia familia nzuri na amekuwa serikali na kwenye nyanja ya kimataifa mda mwingi.Hapo hata English inapanda sio mchezo.
 
Wewe ni taahira sababu unaongea kitu kisichokuwepo

Inaonekana ulivyo shallow minded na hujawahi hata siku 1 kufika Tanzania,

Hivi yupo mtanzania asiejua lugha yake ya asili? Hata watoto waliozaliwa mijini wanaweza wasijue lugha yote Lakini baadhi ya maneno wanajua

Zaidi ya 40% ya wa Tanzania wapo vijijini, unataka kusema huko vijijini hawaongei lugha zao?
 
Hawa watu hawaeleweki. Wanasema kwamba wao sio wakabila ila wanataja kabila la mtu waziwazi? Huo ni unafiki wa hali ya juu. Kama wao sio wakabila basi wasitaje kamwe kabila la mtu.
Wewe ni kichaa

Maana ya ukabila ni kumpendelea mtu katika nafasi fulani, kipaumbele, huduma, huba, chuki, maslahi au kumdunisha sababu ya kabila lake na si vinginevyo

Kila mtu ana kabila sababu watu sio mawe, kabila lako litaishia kwenye mambo ya kimila, lugha, mavazi, utamaduni kwa ujumla Lakini sio zaidi ya hapo, Huwezi kupata nafasi sehemu yoyote sababu ya kabila lako wala Huwezi kuzuiliwa kufanya makazi, biashara, mahisiano sababu ya kabila lako
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…