Mama wa TRA akutwa amefariki Bunju Beach, mume wake naye amepotea

Mama wa TRA akutwa amefariki Bunju Beach, mume wake naye amepotea

Wana JF,

Mama mmoja mke wa mzee maarufu wa Kiti Moto ya kwa Mzava, amekutwa amefariki na damu zimetapataa sakafuni. Haijulikani chanzo kilichopelekea kifo chake.

Baada ya kifo, mme hapatikani kwenye simu yake, gari la mme limekutwa limetelekezwa getini na halijafungwa. Huyu mama alikuwa mfanyakazi wa TRA Samora karibu na Salamander.

Mzava ni mtu maarufu kule Bunju kwa utaalam wa kupika kitimoto ambaye awali alikuwa wanafanya kiti moto Ubungo shekilango dagaadagaa.

Mama anaitwa Irene Mzava, alihamishwa kutoka TRA Temeke, akaletwa Tegeta. Wanyetishaji wanadai, waliandaa safari kwenda Moshi saa tisa. Lakini safari ikageuka shubiti, baba anaonekana alimpiga na kitu kizito ikawa ndio mwisho.

Baba akaenda baa akawaomba wahudumu wampatie mauzo ili apelekwe mgonjwa hospital, basi akafika getini na kutelekeza gari, akaingia ndani katoa gari jipya aina Toyota Harrier new model 2015 inaitwa matako ya nyani, gari ilikuwa full tank kwa ajiri ya safari na imepakia vitu, baada ya mauaji akaipiga mogul mpaka Moshi inawezekana alifika saa 11, akaitelekeza gari mpya na kutokomea. Yeye na mke wake ni majuzi walitoka kwenye msiba wa mama wa mauaji. R.i.P Mama Irene Mzava.
Mkuu hizi details umezipataje?

Kuna details za mashuhuda wa tukio lakini hizi ni kama involved na tukio
 
Inatisha mnoo... Dada mmoja nae kafanya hivyo huko wapi sijui... Kamuua mumewe kwa maji ya moto na petroli...

What is happening!??
 
Kuachana ni mbaya sana kunaathiri Sana watoto ila ni afadhali kuliko kuuana.
Lakini kama ulikosea kuoa utafanyaje? Maana sumu za wanawake ni hatari utakufa siku si ko.

Mke mfanyakazi tra mume anapika kitimoto. Mme atakua alivumilia mengi hadi vikafika mwisho
Uzoefu nilionao.
Inawezekana wakati wanaoana, mume alikuwa na kipato kizuri tu, na huenda ndiye aliyemfanyia mipango akapata hiyo kazi.
Muda umesonga, mambo yamebadilika.
Mume ameisha wekeza( labda nyumba, mashamba, nk).
Mume, sehemu aliyokuwa kumeharibika, hana alternative! Mke sasa ana kipato, jeuri, na pengine jeuri imeambukiza mtoto. Baba anadharauliwa, mpaka mezani akichelewa anakuta makombo, hakuna ile heshima ya kuwekewa chakula chake.
Hana pa kwenda. Hana jinsi. Akijaribu kuomba msaada kutoka kwa mkewe, hapewi, kufokewa mtindo mmoja!

Ilitokea. Ila kwa kesi hii, jamaa yangu kwa kuwa alikuwa mnyenyekevu sana na asiyependa makuu, alifungasha virago na kurudi kwao. Inahuzunisha!
 
Back
Top Bottom