Kuna dogo mmoja alikuwa hasalimiani na mama yake. Sijui walikosana nini. Bahati nzuri niliongea naye na akanipa hiyo ishu. Nikamuuliza mama yako yuko wapi? Akasema alikuwa amelazwa hospitalini anasumbuliwa na shida ya figo.
Nilimuuliza swali rahisi sana. Ati, huyo mamako akikata roho leo, wewe utakuwa na hali gani? Hutajuta maisha yako yote?
Nilimwambia sasa hivi acha kila kitu unachofanya. Nenda hospitalini alikolazwa mama yako. Wala usinunue zawadi yo yote. Nenda kamsalimie mama yako. Nenda ukamkumbatie. Mwambie mama nakupenda sana na nisamehe kwa kujaribu kukosana nawe. Lia naye. Mfute machozi. Mwangalie machoni. Mwambie mama utapona. Nakupenda sana!
Nafurahi kwamba alifanya hivyo maana baada ya siku kama tano hivi mama yake alifariki. Mpaka kesho na kesho kutwa huwa ananishukuru hatari na huwa ananiona kama nabii au apostle fulani hivi. Na ukimuuliza ni tukio gani la muhimu sana ambalo limeshawahi kumtokea katika maisha yake atakutajia kuwa ni siku ile alipojishusha na kwenda kuomba msamaha na kuagana na mama yake aliyekuwa anapambania maisha yake hospitalini.
Na maneno ya mwisho kutoka kwa mama yake ameyaandika kabisa: Asante mwanangu James. Na mimi nisamehe. Sikuwa mama mkamilifu lakini nakupenda mwanangu. Nakuombea mibaraka katika maisha yako. Utaishi maisha mema mwanangu"
Kwako wewe kwa vile umeshachelewa kuomba msamaha kwa mama yako fanya yafuatayo:
Kwanza msamehe mama yako kwa makosa aliyokukosea mpaka ukafikia kumchukia. Mwachilie kabisa kabisa kwa moyo wako wote. Mwambie kabisa: Mama mimi nimeshakusamehe! Na wewe nisamehe mamangu. Tusameheane! Ukiweza nenda kaburini kwake alipolala mkasameheane huko!
Pili kimbilia kwa Mungu (kama unaamini katika uwepo wake). Mwambie Mungu Akusamehe pia kwa niaba ya mama yako maana kumchukia mama yako ulivunja amri mojawapo ya Mungu - amri ya muhimu sana na iliyofungamanishwa na urefu wa muda wako wa kuishi hapa duniani.
Ukishamsamehe mama yako na Mungu Akakusamehe, basi chukua kisadaka kidogo ukipeleke madhabahuni au kwa watoto yatima huko kama ishara ya neema, msamaha, upendo na kusonga mbele. Na kila unapopiga magoti kuomba muombee mama yako na mshukuru Mungu kwa muda wote aliomuweka hapa duniani....
Ukiyafanya haya kwa moyo mweupe, chuki yako itaisha, mahangaiko unayopitia na hii sense of guilty inayokutesa pole pole itaanza kupungua na hatimaye utakuwa huru. Utakuwa mwenye furaha mpya na mambo yako mengi tu yataanza kufunguka.
[emoji3591][emoji3591][emoji3591] Na hili liwe funzo kwa nyinyi ambao bado mna wazazi. Epukeni sana mabifu na wazazi wenu. Wasameheni. Jishusheni kwao. Wajalini, kuwaombea na kuwasikiliza maana wakija kuondoka aisee ni mtihani sana. Na hakuna majuto yanayouma kama mzazi wako kufariki wakati mmekosana na mpaka kufikia hata kutosalimiana.
Kila la heri mkuu....
View attachment 2447445