Ali Nassor Px
JF-Expert Member
- May 6, 2022
- 2,384
- 3,926
- Thread starter
- #481
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Santoo sana Alii nimefikaaa!! Ngoja niendelee nilipoishia..Analyse Palina Antonnia Depal Kapeace Numbisa baby zu Watu8 Dr Restart Kalpana Bantu Lady charrote Nylon Half american Amehlo Jane Lowassa Franky Samuel Leejay49 Nourhan Robot la Matope Elli Makindajr Vinci Dayot Upamecano IFRS Sinoni kyala Ulinamaka Joannah Nuzulati Da Vinci XV masai dada Kalpana Lovelovie Premij canoon Lamzettttt
Dah..hio sehemu ya Sadamu kuuwawa inahuzunisha sana poleni sana mkuuCHAPTER 9
baada ya kuandika barua nikaambiwa nitoke staff nimsubiri mama na sister wanaongea na teacher lakini mda natoka nje pale nje nikakutana na mjomba..
mjomba aliniambia " mjomba umeyatafuta matatizo"
nikamjibu " mjomba sijayatafuta matatizo ila matatizo yamenitafuta mimi ila najutia sana na naona nimemkosea mama na familia kiujumla "
mjomba akaniambia kitu kimoja ambacho kilinishtua kidogo " tulia mjomba yangu mambo madogo tu haya tunayamaliza na umenifurahisha sana😁😁😁"
INAENDELEAAAA....
nikamuuliza kwanini mjomba lakini hakunijibu akarusha mada. na mpaka upleo hii ajanipa jibu nimemfurahisha kivipi.
lakini baada ya mama na sister kutoka ikabidi sisi sote tuongozane nyumbani kwa sister na mjomba pia akiwemo.
kufika kikao kikaanza mda uo nina barua yangu safi kabisa ya suspension. mama mda uo alikaa kimya tu sister ndo alikuwa ananisema sana.
maamuzi yaliyotoka kuwa nitafutiwe tution niwe naenda kusoma ili kufidia mda wa suspension nisikae bure bure tu lakini pia nikaambiwa kuhusu maisha ya ghetto niyasahau sitoruhusiwa tena kwenda kukaa kule. so nitakaa kwa sister lakini mjomba akaomba mimi nikakae kakwe.
hilo alikuwa alikupigwa hata na mtu mmoja lakini acha niwaambie mjomba alikuwa na mtoto wa kiume mmoja tu anaitwa Sadamu gape la miaka baina ya mimi na sadamu ni tofauti kama ya miaka 2 hivi sadamu ni mdogo kwangu.
lakini sadamu ni mtukutu balaa japo baba mdogo anakipato kidogo coz anapoga kazi manispaa anakusanya kusanya ushuru masokoni.
enzi hizo alipambana sana sadamu asome lakini ilikuwa kinyume chake sadamu alikataa shule mapema sana.
mjomba kwanza alimpeleka shule hizi za kata za kawaida performance ya sadamu ikawa ovyo akampeleka shule ya msingi bunge lakini alipofikia form 1 akaacha shule kabisa akasema akasema anataka mtaji wa pesa afanye biashara yoyote ile.
mjomba akampotezea akaona toto pimbi ili akampotezea dogo kusugua sugua mtaani akaanza kutumia bangi ,mara anaiba ndani pesa ndefu alafu aonekani miezi, mara siku nyingine halali nyumbani.
dakika ya mwisho likatoka wazo asomewe dua akasomewa dua fresh tu.
sasa likaja na wazo kuwa kama vipi apelekwe veta kuna mtu mjomba anajuana nae wanampokea kiujanja ujanja hivi bora sadamu asome japo ufundi kuliko kumpa biashara wakati dogo sana anaweza kutia hasara biashara yote msingi akaonga na mtaji akalewea.
So, baada ya kikao kuisha me nikaenda zangu maghetto nikasepa zangu kwa mjomba na swala la deni la ada mjomba akasema sister na mama waachane nalo analilipa yeye na hiyo pesa ya tution atalipa yeye pia.
kufika kwa mjomba nikakutana na mjomba , aunty na sadamu mwenyewe sadamu mdomo mweusi balaa yani kawa bangi mtu.
kitu ambacho niligundua mjomba kutaka nikakae kwake, kuwa anataka sadamu na mimi tukae karibu labda mimi naweza nikamshawishi sadamu na yeye akapenda shule kiasi fulani. daaaah kilichotokea ni kitu tofauti kabisa.
Sadamu aliuliwa kwa tukio la kupora bodaboda.
siku hiyo nakumbuka sadamu ajarudi nyumbani kama siku 2 hivi siku aliyorudi tukaonana fresh sema alikuja kama mnyonge mnyonge hivi sio kawaida yake kabisa .
akaja tukaongea ongea sana tu dakika ya mwisho akasema " oi me natoka tena "
nikamjibu " fresh"
akaondoka zake siku hiyo mjomba na aunty walikuwa wameenda shughulini, kwahiyo baada ya sadamu kuja tukawa wawili ila baada ya kuondoka nikajikuta nyumba nzima nipo peke yangu.
mida ya saa 3 au 4 hivi hivi, mjomba anakuja kuniamsha kuwa kuna matatizo yametokea niaamka fresh kwenda kumsikiliza.
inshu ya sadamu kuuliwa alianza kuniambia mimi kabla ya kumuambia aunty, tukitoka nje tukaenda kukaa sehemu ya mbali kidogo na nyumbani lakini pia akutoka yeye tu lakini pia simu ya aunty aliichukua akanipanga inshu nzima kuwa sadamu kashauliwa inasemakana kachomwa moto yeye na mwenzake mitaa ya kitunda huko.
daaah ile siku niliudhunika sana.
kwanza niliudhunika kwa mambo mawili ndo siku ya kwanza kumuona mjomba akilia kile kilio chenye uchungu mzito ndani yake lakini pia kumpoteza sadamu ambae mchana nilikuwa nae na kauli ya mwisho aliniambia " natoka".
mjomba aliongea sana na alilia sana kama mzazi ila tutafanya nini sasa na jambo lishatokea lakini pia kuna mda hauwezi kupindisha mipango ya mungu.
kuna mda utatamani kutoa msaada kwa mgonjwa lakini mgonjwa hawezi kumeza dawa hata kama una huruma kiasi gani hauwezi kumeza dawa wewe ili yeye hapone.
Aunty mkewe mjomba alikuwa na matatizo mawili yanamsumbua sana cha kwanza alikuwa na pressure lakini cha pili mashetani.
mjomba akaniambia kuwa mimi nibaki nyumbani na aunty ila nisimwambie kitu chochote aunty mpaka mwili ufike kwa vile mda ule aunty kalala nisimuamshe ila akiamka kama akija kwangu nisimwambie chochote kile kilichotokea.
kweli bhana aunty hakuamka japo kuna siku alisema kuwa siku ile waliyoenda harusini mchana kitovu kilikuwa kinamvuta sana.
maiti ilikuja home yani daaah kuna mambo sikieni sadamu alikuwa kachomwa moto ile kaungua kikweli kweli vuta picha binadamu kachomwa mtoto alafu ukimshika hivi ile nyama yake anabanduka kama nyama ya ngombe yenye mafuta mengi iliyoiva sana.
kiufupi tu ilikuwa ngumu sana kumtazama mara mbili mbili, hata kuosha mwili wake ilikuwa ngumu nani sasa unadhani anakubali kuosha binadamu kachomeka moto anatokota mafuta kiasi kile. tulimzika bila hata kumuosha na kumkafini
yani siku zote nikimkumbuka sadamu mood inakata kabisa nikikumbuka alivyoniaga nikikumbuka nilivyouona mwili wake uliochomwa moto.
mpaka leo hii aunty hayupo sawa kabisa tunaishi nae tu lakini daaah.... wakina mama wanapitia magumu mengi sana.
life lilienda nikamaliza form 6 fresh tu nikiwa nasubiri matokeo ya form 6 kwenda chuo nikachaguliwa kwenda JKT KIGOMA.
nikaona jau kwenda JKT mjomba akaniambia niende nikapige nae kazi ya kukusanya ushuru soko la vietnal na tandika me.nilikuwepo upande wa tandika kwa mwezi nilikuwa napata kama laki 3 hivi, kaa kaa pale sokoni nikajikuta naingia kwenye penzi la mama ntilie jimama moja hivi jeupe lina lafudhi ya kizanzibar lina watoto 3 moja alikuwa darasa la 3 mwengine form 2 lakini huyu alubahatika kumaliza alipigwa mimba na mwengine alikuwa yupo form 4.
iki kisa nitawasimulia siku nyingine lakini nilionga mpaka mashati mawili ya shule na viatu, nikawa namlipa kodi hapo kumbuka mimi ni dogo tu hapo lakini nina date na limama lenye miaka kama 40 hivi.
piga piga kazi matokeo yakatoka nimefaulu natakiwa ni apply chuo. lakini mda uo pesa ya chuo sina yani licha ya kukusanya laki 3 kila mwisho wa mwezi. lakini nilijikuta kama nina laki 3 na nusu tu, na hapo sokoni teyal nishapiga kazi kama miezi 4 hivi.
kumbuka aunty alikuwa na matatizo ya pressure na mashetani kuna siku mmoja akapandisha ikabidi tumpeleke kwa sheikh mmoja hivi ambae ni jirani yetu mitaa ya kigogo hapo.
yule sheikh alikuwa na tatizo mmoja anasoma soma madua yake weeeeeh alafu anatulia hivi kama anazima nadhani yale madudu yake yalikuwa yanamtuliza hivi.
sasa baada ya aunty kutulia lakini kalala hapo tumemfunika na kanga na sheikh kukaa sawa uncle si akaanzisha mada kuwa kuna sehemu yeye anaijua na kuna mada kazisikia kuna shimo linatoa madini.
ila hiyo sehemu ipo Mkoa X ndani
onahindanii huko, sheikh akaingilia mada akasema yeye hiyo ndoto kashawahi kuiota kuwa kaongozana na watu wawili waenda kufata madini sehemu lakini yeye hajui ni sehemu gani wala sura za ao watu usingizini hakuzijua ni za kina nani ila alikuwa anaongea nao ila sura zao hakuzijua ni za kina nani.
ITAENDELEAAAA....
Mr devi ww moton moja kwa moja twna utawekwa kule kwenye kuni kavu 😂😂😂
Daaaah 🥴🥴🥴 inaendlea bhnaKwani bado inaendelea?
Amin 🤲🤲🤲Dah..hio sehemu ya Sadamu kuuwawa inahuzunisha sana poleni sana mkuu
!! Mungu atusaidie watoto wetu wasikengeuke!
Tuko pamoja 🤝🤝🤝Asante 🙏