Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike

Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike

CHAPTER 5

I moved to the bed nikamuamsha akaamka ile kivivu sana maana shughuli mwanzo ilikuwa nzito sana. nikamuuliza vipi umeshakula akanijibu hapana sijala nikamuuliza kwanini sasa na pesa nimekuachia Naa akasema aaah najisikia vibaya nimekunywa juice tu najiisi kama nina homa hivi na kichwa kinaniuma na kiuno kinauma mda uo Naa kabadilika sura namuona rangi kabadilika fulani hivi macho mekundu sana na kama sura imevimba hivi.

Nikaona oooh sasa jela ile pale nyimbo ya Hussein Machozi " KAFIA GHETTO" kama inaenda kunitokea mimi hivi.

INAENDELEAAAA.....

Ujue ile hali niliichukulia poa poa sana . nikadhani kwamba aaah labda uchovu hivi na kwa vile si kalala sana. ila kila mda ulivyozidi kwenda na mtoto wa watu hali yake ndo ulizidi kuwa mbaya.

kuna mda nilitamani kama nichukue bagi langu hivi nisepe alafu nimpigie yule mchizi wake kuwa manzi wako yupo Kivulini guest house mitaa ya sinza huku njoo umchukue ila nikaona hapa kuna dalili kama zote za kujikamatisha.

kwanza yule babu wa pale guest ananijua vizuri tu. na hata kama hanijui lakini kwa siku nilizokaa pale nina uhakika atakuwa kashanikalili sura zile ingia toka ingia toka sura yangu atakuwa kashaimanya kiasi chake.

ikabidi nimpigie mwanangu yule aliyechukua namba za head girl wa kina naa

"Cosmas njoo guest hapa kuna msala umetokea"

ubaya wa mambo jamaa nae akawa anachukulia kama jokes hivi ananiuliza vipi kaka dogo kapandisha nini au teyali ushamvunja kiuno mtoto wa watu, ulimpakia mkongo nini.

nilimmaind kwa kiasi fulani ila nitafanya nini alafu ukitazama ndo mwana pekee niliyekuwa namtegemea kwa mda uo hiyo ilikuwa kama mida ya saa 5 hivi usiku inakimbilia 6 usiku Naa anamwaga jasho kama maji yani pale kitandani kama maji yalimwagika hivi kumbe jasho la binadamu tu.

Cosmas baada ya kufika sasa na kumuona Naa yale makuzi yake akaweka pembeni swali la kwanza akaniuliza huyu kala kweli

nikamjibu hajala chochote kaka kaniambia kanywa juice tu

"Njaa na mapenzi haviendanii kabisa 😂😂😂 fanya dogo ale kwanza kamnunlie na dawa za Diclofenac alafu tufanye mpango tumpeleke hospital fast sana, alafu hizi inshu wewe usihofu wala nini ? yalinitokeaga kama aya yako sitokaa nisahau alafu demu niliyekuwa nae mimi ni bonge kumubeba siwezi acha tu 😂😂😂"

wakati mimi nina hofu kuwa mtoto wa watu asije akafa mule guest Cosmas hana hofu kabisa yani alishtuka mara moja tu lakini baada ya hapo jamaa anafanya matani mengine.



MwanaJf aya masuala yanahusiana na mahusiano kufungia mtoto wa watu akaumwa ghafla wewe sikia sikia tu kwa mtu, lakini usiombe iwe live kwako yaani utajamba kisamvu ulichokula mwaka juzi.

Cheka Sana lakini omba yasikukute. So many innocent people wapo magerezani kwa inshu kama hizi.

Kiufupi pamoja na ujanja wangu lakini nilipagawa mpaka nikamuuliza Cosmas hivi akifa huyu itakuwaje.

Cosmas alinitazama akanijibu " Acha maswali ya kipumbavu omba mungu mtoto wa watu apone ufanye mpango wa kumrudisha kwao sasa mambo ya atakufa atakufa ynatokea wapi mtu anaomba dua njema wewe umeona wapi mtu anazaa mtoto alafu anasema huyu atakuja kuwa papai ataliwa sana na wenzake, kwanz shukru sana sasa hivi usiku tunatoka na dogo hakuna anaetuona hapa"

nikatoka nje fasta nikaenda kuchukua bajaji. Tukampandisha Naa safari mpaka Soinza Palestina hospital pale

Dr aliniuliza huyu ni nani yako . nikamjibu ni mdogo wangu akataka kuniuliza maswali mengi sana kivile.

Naa akapigwa dripu nakumbuka zilikuwa kama dripu tatu hivi au mbili sikumbuki vizuri sana ila dripu zote 3 zilinicost elfu 15. Dr akaniandikia dawa kadhaa nikazifata dawa. Total cost niliyotumia pale hospital tu ni kama elfu 20 hv plus na usafiri kiufupi nilikuwa nazitekeza tu pesa za ada na pesa zinakaribia kuisha.

Dakika ya mwisho tukamuacha dogo anaongezwa maji wakati nipo na Cosmas nikamuuliza kwa mfano kama ningekupigia simu usingepokea simu ingekuwaje na tupo mbali mbali.

" Aaaah achana na hizo mada tunajichoresha sio eneo la kuongea hizo mada hapa"

mda uo peace of heart ilikuwa ishaanza kurudi nikamwambia Sema siku nikipata zigo jengine nalileta ghetto kwako kule 😁😁😁

Cosmas akacheka kisha akanijibu " Hii tabia ya kuazimishana maghetto ni kuwanyima tu wamiliki wa guest na lodge mapato na wao wana watoto ,watoto wao watakula nini sasa kama nyie hamutaki kwenda guest "😂😂😂


Tukaachana na maongezi ya masihara Cosmas akawa serious sasa akaniambia sikia kaka" Huyu dogo una mpango nae gani mpaka dakika hii"

nikamuuliza " mpango nae gani kivipi"

" Yani unaishi nae vipi maana siku ya tatu leo inakatika upo nae guest tu haujui anakaa wapi wala wazazi wake wakina nani ?"

Daaah ilinibidi nishushe pumzi ya kuchoka kwanza. maana Cosmas naona alinishtua jambo zito sana maana nilifikiria mara mbili inawezekana kweli alikuwa mkoa X anaishi na mama yake lakini inawezekana pia Nasra alinidanganya mkoa X anaishi na wazazi wake wote wawili ili kuna inshu labda kaifanya kaamua atoroke kwao.

nikamjibu" kaka sina inshu nae ya kuishi nae sana kwa sababu mpaka dakika hii pesa niliyokuwa nayo inakaribia kuisha hapa "

Cosmas :Sikia mpotezee dogo

Mimi : nimpotezee kivipi sasa

Cosmas : Aaah wewe mpigie huyo bwana wake uongee nae aje kumchukua demu wake tu.

 Ali : hilo suala siwezi kulifanya hata kidogo ebu jaribu kuvaa uhusika wa jamaa huko alipo now yupo vipi, inawezekana yeye ndo kamtumia nauli nasra aje dar es salaam alafu Nasra aonekani alafu baada ya siku kadhaa nasra aende kwa jamaa aseme tu maneno yasiyo eleweka si ndo nitakuwa namuweka mtoto wa watu kwenye mazingira magumu zaidi, kwanza jamaa anaweza akamtimua naa.

Cosmas : daaah kweli

Ali : ila sikia nina shida mmoja naomba unisaidie, naomba nasra akae kwako japo siku mbili hivi ili nifanye utaratibu kwa arudi kwao kwa sababu pesa ya kulala guest kwa sasa sina.

Cosmas akanitazama akanijibu: hapana hilo siwezi kukusaidia

 Ali: why sasa hauwezi kunisaidia na wakati ulisema mwanzo kuwa nikitaka kusepa nikuachie nasra

Cosmas : nilikuwa nakutania, kwanza dogo anaonekana mgonjwa akizidiwa tena au likitokea la kutokea nampeleka wapi , cha pili wewe unamjua mwenye nyumba yule bi mkubwa jau kichizi mtu wa dini dini, kuna mpangaji juzi tu kaamisshwa kisa kaleta demu mchana kweupe na bi mkubwa kamuona huyo demu wa jamaa. kwahiyo wewe force force dogo harudi kwao tu.

ITAENDELEAAAA.....
Ntarudi
 
CHAPTER 6

Ali : ila sikia nina shida mmoja naomba unisaidie, naomba nasra akae kwako japo siku mbili hivi ili nifanye utaratibu kwa arudi kwao kwa sababu pesa ya kulala guest kwa sasa sina.


Cosmas akanitazama akanijibu: hapana hilo siwezi kukusaidia


 Ali: why sasa hauwezi kunisaidia na wakati ulisema mwanzo kuwa nikitaka kusepa nikuachie nasra


Cosmas : nilikuwa nakutania, kwanza dogo anaonekana mgonjwa akizidiwa tena au likitokea la kutokea nampeleka wapi , cha pili wewe unamjua mwenye nyumba yule bi mkubwa jau kichizi mtu wa dini dini, kuna mpangaji juzi tu kaamisshwa kisa kaleta demu mchana kweupe na bi mkubwa kamuona huyo demu wa jamaa. kwahiyo wewe force force dogo harudi kwao tu.


INAENDELEAAA.....


Naa baada ya kupigwa dripu zote tatu na kupata nafuu kidogo ikabidi nirudi nae lodge lakini kumbuka mda wote hapo natumia pesa ya ada na hapo teyali nishaiteketeza kama laki 3 na 70 hivi na shilingi shilingi hivi.


Ikabidi nimdanganye kuwa jamaa yako bado hajanitafuta nadhani jamaa mzinguaji sana yule. Lakini mwanzo nipo hospital pale nakumbuka kuna mda yule jamaa yake naa alinipigia simu.


Akaniuliuliza " yule msichana aliyekuazima simu yuko wapi au alishuka wapi"


Nikamwambia" aaaah kiongozi sijui maana mimi nililala sasa inawekana alishuka kwenye gari wakati amelala so itakuwa mtihani kidogo kujua yupo wapi au alishukia wapi ? "


Jamaa alilalamika sana yani sana 😂😂😂😁. Kuwa Naa mjini mgeni alafu jamaa likawa nalo linanidanganya eti ni mdogo wake.


Mae mdogo wako unaweza kumuoa kumuweka unyumba.
LWakati naendelea kuongea na Naa ikabidi sasa nimshawishi arudi kwao tu.


Ali: Sikia Naa ujue maisha aya yana misukosuko mingi sana ila yote ya yote matatizo yanapotokea tunatakiwa tujifunze kupitia matatizo na sio kulaumu watu au kujilaumu sisi."


Kama kitu kimetokea ndo kishatokea , mimi kesho nasepa shule nakaa hostel na kesho pia ndo tunafungua shule nakushauri urudi kwenu tu kwenu ni kwenu jiji la dar es salaam gumu sana kuna matukio mengi sana ya kutisha unaweza ukauliwa alafu kwenu wasijue hata kama umekufa sasa mimi nataka nikupe msaada mmoja nataka nikukatie tiketi ya bus la mkoa X urudi kwenu".


Naa alikuwa ananijibu kwa kutikisa kichwa yani dogo alikuwa anaumwa anaumwa kweli tofauti ya mwanzo alikuwa kazidiwa sana lakini baada ya zile dripu kidogo alipata uafueni.


utaratibu wangu maisha ambao nilijipangiaga mimi mwenywe week ya kwanza kufunguliwa shule siende na hata dada yangu alikuwa anajua, mara nyingi nilikuwa najitete week ya kwanza ni week ya usafi usafi tu hakuna masomo.


Naa akakubali fresh kurudi kwao sasa kidume nikawa nawaza nafanyaje lakini mda uo mfukoni nina kama laki 1 na 30- hivi, nikasema aaaah acha niitumie alafu nitapiga vizinga kwa dada na bro watanipa tu.


jumatatu jioni nikatoka nae nikaenda nae ubungo nikamkatia tiketi ya kwenda kwao ilikuwa ni shilingi elfu 45. jumatano ndo alikuwa anasafiri.


jumatano imefkia nikamsindikaza mpaka stand nikampandisha gari nikampa na elfu 30 ya kula njiani hapo kidume nazidi kula pesa ya ada tu.


lakini nadhani hapa kwenye kumpandisha gari alafu mimi nikasepa nadhani nilifanya kosa mmoja kubwa sana maana miaka kama miwili mbele nilikuja kuoanana tena na Naa akiwa na mtoto tena mtoto mwenyewe wa yule jamaa wa mbezi mwisho.


ilikuwaje kuwaje mpaka nikakutana nae na ilikuwa wapi na nilifata nini. tuendelee kusoma story.


Naa akapanda bus mimi nikasepa kwa dada kumbuka natakiwa kwenda shule na nilipe ada siku hiyo hiyo jioni mama akanipigia simu akaniuliza umeshalipa ada nikamjibu ndio mama nishalipa ada yote hapo mfukoni nika kama elfu 55 tu .


sema baada ya kumjibu ndio hakuniuliza kitu maana mama yangu alikuwa hana kawaida ya kuulizia ulizia mambo ya risiti.


Sasa kidume nikawa nawaza hii pesa nairudisha vipi. nimemfata sister kumwambia nina shida ya elfu 50 kuna kitu nataka kununua akanitolea nje sijui hana pesa akili yake haipo sawa mambo ya upatu yanamchanganya.


hapo kichwa kinaniuma balaa nikaona hapa kwa sister hapanifai. not safe ninja naweza nikajinyonga mda wowote 😂😂😂


Kipindi nasoma form five na six nilikuwa nimepanga ghetto na marafiki zangu kama watano hivi mitaa ya Kurasini kule sasa wakati naenda ghetto nikawa na mawazo sana.

marafiki zangu wawili walikuwa wanabet sana
kuna rafiki yangu mmoja akauliza vipi mbona una mawazo sana ikabidi nimwambie tu kilichonitokea chote.

Akaniambia "Daaah wewe MSE#@₹E ni jambazi alafu umeyakanyaga yani umejipiga kisu cha kiuno wewe mwenyewe sasa hapo itabidi tubet tu".

nikamwambia " sasa tunafanyaje nitengenezee mkeka"

akaniuliza " kwani haujui kubet "

nikamwambia " mimi sijui " .


akanitengenezea mikeka miwili mkeka wa kwanza anakitengenezea mikeka miwili mkeka wa kwanza ulikuwa wa elfu 20 mwengine wa elfu 10.

Mkeka wa elfu 20 mapema tu ukachanika. ukabaki wa mkeka wa pili wa elfu 10 ukabaki nao niliubettia team moja ya kwanza dakika 40 za kwanza tu teyali ilikuwa ishafungwa goal tatu.
ikabidi nizime simu mda uo jasho linanitoka ikabidi nizime simu nilale kwanza.

Gusa hapa kupata muendelezo 👇👇👇👇
Post in thread 'Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike' Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike
 
Back
Top Bottom