Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike

Mama yangu mzazi aliwahi kuniambia bora nife tu apumzike

CHAPTER 6

Ali : ila sikia nina shida mmoja naomba unisaidie, naomba nasra akae kwako japo siku mbili hivi ili nifanye utaratibu kwa arudi kwao kwa sababu pesa ya kulala guest kwa sasa sina.


Cosmas akanitazama akanijibu: hapana hilo siwezi kukusaidia


 Ali: why sasa hauwezi kunisaidia na wakati ulisema mwanzo kuwa nikitaka kusepa nikuachie nasra


Cosmas : nilikuwa nakutania, kwanza dogo anaonekana mgonjwa akizidiwa tena au likitokea la kutokea nampeleka wapi , cha pili wewe unamjua mwenye nyumba yule bi mkubwa jau kichizi mtu wa dini dini, kuna mpangaji juzi tu kaamisshwa kisa kaleta demu mchana kweupe na bi mkubwa kamuona huyo demu wa jamaa. kwahiyo wewe force force dogo harudi kwao tu.


INAENDELEAAA.....


Naa baada ya kupigwa dripu zote tatu na kupata nafuu kidogo ikabidi nirudi nae lodge lakini kumbuka mda wote hapo natumia pesa ya ada na hapo teyali nishaiteketeza kama laki 3 na 70 hivi na shilingi shilingi hivi.


Ikabidi nimdanganye kuwa jamaa yako bado hajanitafuta nadhani jamaa mzinguaji sana yule. Lakini mwanzo nipo hospital pale nakumbuka kuna mda yule jamaa yake naa alinipigia simu.


Akaniuliuliza " yule msichana aliyekuazima simu yuko wapi au alishuka wapi"


Nikamwambia" aaaah kiongozi sijui maana mimi nililala sasa inawekana alishuka kwenye gari wakati amelala so itakuwa mtihani kidogo kujua yupo wapi au alishukia wapi ? "


Jamaa alilalamika sana yani sana [emoji23][emoji23][emoji23][emoji16]. Kuwa Naa mjini mgeni alafu jamaa likawa nalo linanidanganya eti ni mdogo wake.


Mae mdogo wako unaweza kumuoa kumuweka unyumba.
LWakati naendelea kuongea na Naa ikabidi sasa nimshawishi arudi kwao tu.


Ali: Sikia Naa ujue maisha aya yana misukosuko mingi sana ila yote ya yote matatizo yanapotokea tunatakiwa tujifunze kupitia matatizo na sio kulaumu watu au kujilaumu sisi."


Kama kitu kimetokea ndo kishatokea , mimi kesho nasepa shule nakaa hostel na kesho pia ndo tunafungua shule nakushauri urudi kwenu tu kwenu ni kwenu jiji la dar es salaam gumu sana kuna matukio mengi sana ya kutisha unaweza ukauliwa alafu kwenu wasijue hata kama umekufa sasa mimi nataka nikupe msaada mmoja nataka nikukatie tiketi ya bus la mkoa X urudi kwenu".


Naa alikuwa ananijibu kwa kutikisa kichwa yani dogo alikuwa anaumwa anaumwa kweli tofauti ya mwanzo alikuwa kazidiwa sana lakini baada ya zile dripu kidogo alipata uafueni.


utaratibu wangu maisha ambao nilijipangiaga mimi mwenywe week ya kwanza kufunguliwa shule siende na hata dada yangu alikuwa anajua, mara nyingi nilikuwa najitete week ya kwanza ni week ya usafi usafi tu hakuna masomo.


Naa akakubali fresh kurudi kwao sasa kidume nikawa nawaza nafanyaje lakini mda uo mfukoni nina kama laki 1 na 30- hivi, nikasema aaaah acha niitumie alafu nitapiga vizinga kwa dada na bro watanipa tu.


jumatatu jioni nikatoka nae nikaenda nae ubungo nikamkatia tiketi ya kwenda kwao ilikuwa ni shilingi elfu 45. jumatano ndo alikuwa anasafiri.


jumatano imefkia nikamsindikaza mpaka stand nikampandisha gari nikampa na elfu 30 ya kula njiani hapo kidume nazidi kula pesa ya ada tu.


lakini nadhani hapa kwenye kumpandisha gari alafu mimi nikasepa nadhani nilifanya kosa mmoja kubwa sana maana miaka kama miwili mbele nilikuja kuoanana tena na Naa akiwa na mtoto tena mtoto mwenyewe wa yule jamaa wa mbezi mwisho.


ilikuwaje kuwaje mpaka nikakutana nae na ilikuwa wapi na nilifata nini. tuendelee kusoma story.


Naa akapanda bus mimi nikasepa kwa dada kumbuka natakiwa kwenda shule na nilipe ada siku hiyo hiyo jioni mama akanipigia simu akaniuliza umeshalipa ada nikamjibu ndio mama nishalipa ada yote hapo mfukoni nika kama elfu 55 tu .


sema baada ya kumjibu ndio hakuniuliza kitu maana mama yangu alikuwa hana kawaida ya kuulizia ulizia mambo ya risiti.


Sasa kidume nikawa nawaza hii pesa nairudisha vipi. nimemfata sister kumwambia nina shida ya elfu 50 kuna kitu nataka kununua akanitolea nje sijui hana pesa akili yake haipo sawa mambo ya upatu yanamchanganya.


hapo kichwa kinaniuma balaa nikaona hapa kwa sister hapanifai. not safe ninja naweza nikajinyonga mda wowote [emoji23][emoji23][emoji23]


Kipindi nasoma form five na six nilikuwa nimepanga ghetto na marafiki zangu kama watano hivi mitaa ya Kurasini kule sasa wakati naenda ghetto nikawa na mawazo sana.

marafiki zangu wawili walikuwa wanabet sana
kuna rafiki yangu mmoja akauliza vipi mbona una mawazo sana ikabidi nimwambie tu kilichonitokea chote.

Akaniambia "Daaah wewe MSE#@₹E ni jambazi alafu umeyakanyaga yani umejipiga kisu cha kiuno wewe mwenyewe sasa hapo itabidi tubet tu".

nikamwambia " sasa tunafanyaje nitengenezee mkeka"

akaniuliza " kwani haujui kubet "

nikamwambia " mimi sijui " .


akanitengenezea mikeka miwili mkeka wa kwanza anakitengenezea mikeka miwili mkeka wa kwanza ulikuwa wa elfu 20 mwengine wa elfu 10.

Mkeka wa elfu 20 mapema tu ukachanika. ukabaki wa mkeka wa pili wa elfu 10 ukabaki nao niliubettia team moja ya kwanza dakika 40 za kwanza tu teyali ilikuwa ishafungwa goal tatu.
ikabidi nizime simu mda uo jasho linanitoka ikabidi nizime simu nilale kwanza.

ITAENDELEAAAA...
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]hapo kwenye kubeti umenikumbusha mbali
 
Khaaa yaani nasoma napata feelings kama mimi hivi
 
Mkeka wa elfu 20 mapema tu ukachanika. ukabaki wa mkeka wa pili wa elfu 10 ukabaki nao niliubettia team moja ya kwanza dakika 40 za kwanza tu teyali ilikuwa ishafungwa goal tatu.
ikabidi nizime simu mda uo jasho linanitoka ikabidi nizime simu nilale kwanza.😃😃😃😃😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
 
Mkeka wa elfu 20 mapema tu ukachanika. ukabaki wa mkeka wa pili wa elfu 10 ukabaki nao niliubettia team moja ya kwanza dakika 40 za kwanza tu teyali ilikuwa ishafungwa goal tatu.
ikabidi nizime simu mda uo jasho linanitoka ikabidi nizime simu nilale kwanza.😃😃😃😃😂😂😂🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣🤣
Ambao hawajawahi kupitia magumu hawataelewa, ubaya ukiingia kwako hata ukicheka unajing'ata ulimi
 
Back
Top Bottom