Mama yangu na kaka yangu ni wachoyo sana, wanafunga friji wafanyakazi wasile, lakini ni washika dini sana

Kule kwenye dini wamejificha tu,na ni asilimia kubwa sana ya wanaojifanya wako deep sana na dini ilaukichunguza mambo yao ni ya ajabu na ndiyo yanayosababisha hata watu kupuuza kufuatilia kwenda Makanisani/Misikitini
Hapo ndiyo ukamalie Dini sana!! kwa sababu shetani amekita miziz ili akuteke kirahisi!! hao unaoona makatili siyo wao bali ni mashetani wamejigeuza kwa sura zao!! ili wew usiwe mwana dini km wao…

lkn pia chakula si ni chao wana haki ya kukitunza wanavo jisikia ni salama kwao! km weye unaona vepe si utafute chako? Friji ya nani kwanza yako au?? ...nyumba ya nani? yako au!! hao wafanya kazi nani kawaajili? si wana lipwa mishahara? au....

ukiwasema wanajifanya wako deep hapo ndo unapotea Mazimaaa!! unataka wakae wapige story na weye Shetani? Kwa nini uwachunguze wao na si walevi km weye??
HAPA KUNA KITU KIZITO MWENYE AKILI ATAGUNDUA
 
Dah... nimejikuta nina maswali kuliko kukushauri

1: una umri gani samahani lakini
2: kaka yako pia Ana umri gani
3: kwanini mpaka Leo wewe na kaka yako mpo hapo nyumbani ilihali mnajieelewa hasa kaka yako ??

USHAURI:
swala la kushika dini na tabia ya mtu wala zisikushangaze kuna watu wapo ivo na wengi watu wadizain hiyo siyo watu wazuri sana (samahani nimemjumuisha na mama) nasema ivi kwasabu watu wanao watumikia ukisha onesha ubinafsi flani anaweza hata kukuwekea sumu kwwnye chakula ...sasa basi kama umeliona hilo wewe kama wewe jaribu kushea na hao wafanyakazi kwa kidgo utakacho pata ...ova
 
Mama yako na kaka yako wameshika dini yani wameshika sheria za dini...

Hivyo ni tofauti na waliompokea YESU KRISTO kama Bwana na mwokozi wao.

Na hili linawasumbua wengi kwani limefanya watu wasimuamini YESU/MUNGU...

Ifike mahali watu waache kufia dini na waweke imani kwa YESU na sio dini, maana dini ni njia ya kukufundisha...

Hata hivyo watu wengi wabaya wamejificha katika dini, kama mama na kaka yako yani wachoyo lakini wanajifanya ni wakristo.

Watu wengi hawampendi Mungu kweli ni wanafki, wanakumbatia dhambi...

Mithali 8:17

Nawapenda wanipendao na wanitafutao kwa bidii wataniona...
 
Mkuu amino nakwambia. Kuna uhusiano mkubwa kati ya ulokole na uchoyo plus roho mbaya. Chunguza uone. Hata kwa mapadre unaweza fukuzwa kazi kwa kula papai la bustanini hata kama lilidondoka
 
Kuna watu uchoyo Upo damuniπŸ€£πŸ™Œ
 
Ni kweli na hii inasimaa kwa mmoja mmoja, Mara kadhaa nimeshuhudia viongozi wangu wa kiroho wakirumbana na kushikana mashati na sisi tunawaona hao kama kioo chetu, viongozi wetu tunaona tamaa za ngono "zinawadrive" na kufanya zinaa na waumini wao.
Haya maswala ya imani yanasimama na mtu binafsi na kumuomba Mungu haswaa atubadilishe maisha yetu.
 
huyo sasa ana PhD in Uchoyo na Roho mbaya
 
Alafu sijui Kwann uchoyo na uroho huwa vinaambatana na unafiki
 
Tena ni makombo aisee, mimi nmeshuhudia mahali nkaumia sana . Hawa wadada wakazi ukiwaskiliza kwa umakini utagundua kuwa hakutarajia kuwa hivyo. Huwa ni maisha yanaenda mrama tu .
Kweli kabisa zuleykha ,huwa naumia Sana kuona hawa watu wananyanyaswa,nao ni binadamu kama wengine na ni KAZI kama zingine pia.

Halafu unajua ni hatar Sana,unamnyanyasa mtu ambaye anakupikia chakula,hivi hauwazi Tu kuwa anaweza kukufanyia chochote kupitia Hicho chakula?
 
Utu hakuna tena
 
Kuna maisha ambayo sometimes uchoyo ni lazima ,mfano watoto wa majirani wanakesha kwako kila siku kwenye tv, wa kwako haendi kuzunguka huko.

We unapambana unarudi na 5,000 . Unanunua unga ,mafuta mboga na ndizi 4 ya mtoto hela imeishia hapo . Sasa bajeti ya mtoto wako ufanye ndogo ale kwa shida wakati hao watoto pia wana wazazi wao?

Hivo hivo mtu anakupiga sound ya kukopa we unamhurumia unajinyima mwisho wa siku halipi anakupiga chenga.

Kuna wakati nilikuwa chuo nakaa na jamaa ,yeye hela zake hapiki , kuchanga hataki ,umeme halipi hata matunda mawili ya kuzugia kwamba leo mle pamoja ,we mwenye hitaji utaweka yeye akirudi anajimegea,hela zake zinaishia kwa malaya na pombe ,mwisho wa siku unamlisha mtu mzima ,friji ya kwako umeme unalipa wewe kama siyo upuuzi ni nini?
Mtu mwenye shida anasaidiwa na unajua huyu anastahili na amekwama lakini siyo wapuuzi ambao wanatumia advantage ya udhaifu wako.
 
Tulipokuwa form six kuna jamaa mmoja bahili balaa , kila siku bwenini yeye anaomba sukari ya uji ,sabuni anagongea, kama haitoshi ataomba hata povu afulie , hata kujihurumia hana , kila siku tunabebana kama washikaji ,mwisho wa siku tunafunga shule watu wamemwibia 400,000 ya pocket money aliyodunduliza tangu shule inafunguliwa. Anaanza kulia oooh nilijibana ,sili ,sifui halafu napigwa.
 
Watu mnaowashambulia washika dini ni wazi hamjui how things work.

Hizo ni tabia za asili, unakuta mtu kazaliwa kazikuta, hivyo hata akiamua kuokoka au kuwa swala tano, haziwezi toka siku moja.

Ni sawa na kuhisi mtu akijiunga chuo tayari kahitimu..mtu kutoka kwenye hizo tabia inahitaji muda na kujikita kwenye mafundisho ya Mungu.

Wengi mnajisifu kuwatafuna washika dini, si jambo la kushangaza, hao sio malaika, tofauti yao na wewe usieshika dini ni kwamba wao wameamua kumgeukia Mungu na kubadilika so wapo kwenye process.

Ni ajabu sana sikuizi watu kukushambulia eti kisa umeshika dini.

Tubadilike
 
...Kaka Yake!... [emoji3][emoji3]
 
Hakika mkuu ni lazima uuamue toka ndani ya moyo kumtumikia Mungu kwa maana swala la Wokovu ni la mtu mmoja
 
πŸ€£πŸ€£πŸ€£πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ‘
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…