Mamba asingewekwa kwenye kundi la Super Predator hastaili kabisa

Heshima ya mamba ni kwa farasi wa majini (hippopotamus), kwa lugha laini KIBOKO na tembo labda. Wengine wote halali.
Simba dume huwa anavuka kwa raha mustarehe kwenye mto wowote wenye mamba zaidi ya 200 na hawamsogelei. King lion ni habari nyingine aisee.
 
jaguar ni katili ila umbo dogo hawezi msogelea mamba. Simba ndio mtata
 
Ungejua simba jike ndiye mwenye nguvu kuliko dume usingebwabwaja hapa, usipagawe na manyoya.
Pole sana, haujui unaloongea mkuu. Simba jike ni mkali na mara nyingi ndio muwindaji, ila dume ndio mwenye nguvu, kiburi, anaejiamini na asieogopa chochote. Mara nyingi dume huingilia kati ile vita aliyomshinda mwanamke na yeye huimaliza mara moja. Hilo dubwasha huwa haliogopa chochote hapa chini ya jua aisee.
 
Kwa taarifa yako ndani ya mto hao uliowataja wote ni halali ya mamba, usicheze na ng'wena wewe.....hili nililishudia mwenyewe pale simba alipokuwa anajaribu kuvuka mto kwenda kukamata wanyama upende wa pili nilichoona ni maji tu yamebadilika kuwa damu ndani ya dakika.
 
Wewee, thubutu yako.

Simba ni mchumba sana kwa mamba.
Hakuna uthibitisha wa video au picha yoyote inayoonesha mamba akimgeuza simba dume chakula chake. Hakuna, narudia tena hakuna, na kama unayo iweke hapa tuione, sio tuongee kwa hisia tu. Simba dume ni habari nyingine aisee. Ni Tiger pekee ndo huwa na uwezo wa kupambana na hilo dubwasha, ila sio hiyo mijusi ya majini. Never.
 
Kabisa mamba ni habari na nusu,

Sent from my SM-S920L using JamiiForums mobile app
 
Mkuu kwenye maji marefu huyo simba dume anageuzwa msosi dakika sifuri na mamba, hii nimeishuhudia mwenyewe. Anaweza kumshindwa kwenye maji ya kina kifupi na siyo deep water, hadi mtangazaji akasema Simba anahitaji kujua kwamba mmiliki wa mto ni mamba.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…