Guasa Ambonii
JF-Expert Member
- Aug 13, 2015
- 8,545
- 10,283
Pamoja sana ndugu yanguasante kwa nyongeza mkuu
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Pamoja sana ndugu yanguasante kwa nyongeza mkuu
Jina lako mwanzo nlilikosea kulisoma mkuu,samahani lakini.Naiona JF ya miaka ya nyuma inarudi kwa vitu nondo had nakubali.
Nimefundishia leoo watu huu uziMfahamu J. Edgar Hoover kachero aliyeogopeka zaidi katika historia ya Marekani.
1. Jina lake halisi ni John Edgar Hoover lakini alipenda kujulikana zaidi kama J. Edgar Hoover. Ni Kachero aliyeheshimika na kuogopwa zaidi ndani ya FBI na Marekani kwa ujumla, ni mtu aliyekuwa na matukio mengi ya kutatanisha.
2. Ndio muasisi wa Shirika la Upelelezi nchini Marekani ( FBI ) baada ya kutoa wazo la kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1935. FBI ilianzishwa ikichukua nafasi ya Bureau Of Investigation ( BOI ) ambapo J. Edgar Hoover pia alikuwa ni Mkurugenzi wake kuanzia mwaka 1924 mpaka 1935. Lengo la kuanzishwa kwa FBI ilikuwa ni kuongeza ufansi katika kupambana na uhalifu ndani ya Marekani.
3. J. Edgar Hoover ndio Mkurugenzi wa kwanza kabisa wa FBI akidumu kwenye cheo hiko kuanzia mwaka 1935 mpaka 1972 alipofariki Dunia akiwa na miaka 77 ( Alifia Madarakani ). Alidumu kama Mkurugenzi wa FBI kwa miaka 32, hakuna Mkurugenzi aliyekaa muda mrefu zaidi kama Hoover. Jengo la Makao Makuu ya FBI limepewa jina lake na linajulikana kama " J. Edgar Hoover Building "
4. Katika miaka yake 32 kama Mkurugenzi wa FBI, Edgar Hoover alihudumu kwa Marais 6 tofauti na hakuwa na mahusiano mazuri na Marais hao. Marais hao ni Franklin D. Roosevelt, Harry S. Truman, Dwight D. Eisenhower, John F. Kennedy, Lyndon B. Johnson na Richard Nixon. Rais Richard Nixon aliwahi kusema alikaribia kumfukuza kazi Edgar Hoover lakini alimhofia Hoover angemharibia mambo yake ya kisiasa. Huku Rais Harry S. Truman akisema Hoover aliifanya FBI kama jeshi lake la siri.
5. Inasemekana Edgar Hoover aliogopwa zaidi ndani ya Marekani kutokana na kuwa na mafaili machafu ya watu maarufu na hata Marais. Ndio maana Marais 6 katika vipindi tofauti tofauti walishindwa kumfukuza kazi wakihofia usalama wao zaidi. Mbinu mojawapo aliyokuwa akiitumia Edgar Hoover ni kurekodi mawasiliano ya Marais waliokuwa madarakani na kutumia kama kinga ya kujihami asitumbuliwe. Mfano Rais John F. Kennedy alirekodiwa maongezi yake ya kimapenzi na mrembo matata wa miaka hiyo Marylin Monroe.
6. J. Edgar Hoover aliogopwa pia ndani ya FBI kwani alitumia mbinu chafu katika kuhakikisha hakuna mtu maarufu zaidi yake ndani ya Shirika hilo. Mfano ni kuwastaafisha kazi au kuwaua baadhi ya maofisa waliokuwa wanataka kumzidi umaarufu na kutishia usalama wa nafasi yake kama vile Kachero Melvin Purvis ambaye alisifika sana ndani ya FBI miaka ya 1930's kwa kudili na Majambazi. Lakini Kachero Melvin Purvis aliacha kazi ghafla na kufariki kifo tata.
7. J. Edgar Hoover alisifika kwa kuwashughukia wahalifu wakubwa waliovunja na kuiba katika Mabenki nchini Marekani katika kipindi cha World Economic Depression miaka ya 1930's. Baadhi ya wahalifu sugu waliokamatwa au kuuwawa kipindi hiko ni John Dillinger, Baby Face Nelson, Pretty Boy Floyd na wengineo.
Pia inasemekana aliratibu baadhi ya mauaji ya wanaharakati kama vile Martin Luther King Jr.
8. J. Edgar Hoover hakuwahi kuoa, kuwa na mwanamke wala kupata mtoto katika maisha yake Duniani. Ni bachela wa muda mrefu sana, na kuna tetesi ziliwahi kuvuma kuwa ni shoga lakini hakuna aliyethibitisha hilo. Kuna wanaosema kazi yake ilimfanya awe bize zaidi na kusahau mambo ya muhimu kama kuoa.
9. Mtu pekee Edgar Hoover aliyemuamini katika shirika la FBI ni secretary wake bi Helen Gandy. Mama huyu alikuwa ni mtu wa karibu sana wa Edgar Hoover walifanya kazi kwa pamoja kwa miaka 54 na ndiye aliyekuwa anatunza siri nyingi za Edgar Hoover. Kama ilivyo kwa bosi wake, Bi Hellen Gandy hakuwahi kuolewa wala kupata mtoto. Alichoma moto nyaraka muhimu za bosi wake punde tu baada ya kifo chake ikiwa ni sehemu ya kiapo chake. Alistafu kazi ndani ya FBI siku moja baada ya kifo cha J. Edgar Hoover.
10. Kwa kuhofia asije akajitokeza mtu mwingine mwenye mawazo kama ya J. Edgar Hoover, serikali ya Marekani kwa kutumia Bunge lake ilitengeneza sheria ya muda wa ukomo wa madaraka kwa Mkurugenzi wa FBI, ambapo anatakiwa asizidi miaka 10 madarakani. Kwani walijifunza kutokana na Hoover kukaa madarakani miaka 32 na kufanya shirika la FBI kama mali yake hivyo kuwatesa Marais wengi.
![]()
Ikooo pouuuwaaa sanaBi Hellen Gandy naye hakuolewa wala kupata mtoto.
Hii kazi nyingine nazo.
Nawe unaweza kuwa hivyo au?Ikooo pouuuwaaa sana
[emoji1] [emoji1] [emoji1]Nawe unaweza kuwa hivyo au?
Vitu vingine ni changamoto[emoji1] [emoji1] [emoji1]
HaswaaaaaaaaVitu vingine ni changamoto
Jamaa kafa. Hajaacha mtoto.Haswaaaaaaaa
Ni kuchagua tuJamaa kafa. Hajaacha mtoto.
Pia alichagua kuwa hivyo
Lakini kachemka kwa DB Cooper!
Db ni Nan maana kumsikia mara ya kwanza kwenye prisonbreakLakini kachemka kwa DB Cooper!
Nahisi hata kifo cha Rais Kennedy atakuwa anahusika ila hawatasemaHuyo bwana kwa maelezo hayo inaonesha alikuwa mtu hatari sana mbaka kufikia kutishia uhai wa marais, ila hiyo namba 8 inatia mashaka kidogo