Mambo 10 niliyoyaona kwenye Mechi ya Yanga Vs MC Alger

Mambo 10 niliyoyaona kwenye Mechi ya Yanga Vs MC Alger

Ukweli Usemwe.
Kuvuka makundi kwenye Championship sio kila timu inaweza.., timu zinajipanga na hazichezi kwa mihemko... waangalie hao MC Alger walicheza kimkakati sana. Hawakutaka kufunguka sana kz walijua mpira wa Yanga, ukifunguka sana wanakuadhibu... Aina hii ya uchezaji wa Alger ndio waliokuwa wanautumia Simba., huwaoni saaana kuwa hatari lakini wanavuka.
Yanga amewahi kucheza mechi,ila leo ndio alikutana na timu.
 
Yanga tukubali tu tangu aondoke Mayele, hatujawahi tena kumiliki mshambuliaji wa kutumainiwa na timu. Dube anaruka ruka tu uwanjani na kuanguka hovyo! Hana nguvu, hana pace!! Yaani ni tia maji tia maji tu.

Musondo naye sijui ana shida gani! Maana hata hajitumi kivile. Kocha naye naye anaonekana ni mgeni wa mashindano! Kuna mapungufu mengi ya kiufundi nayo yamechangia kuindosha timu kwenye mashindano.
 
Yanga tukubayi tu aondoke Mayele, hatujawahi tena kumiliki mshambuliaji wa kutumainiwa na timu. Dube anaruka ruka tu uwanjani na kuanguka hovyo! Hana nguvu, hana pace, hana kasi!! Yaani ni tia maji tia maji tu.

Musondo naye sijui ana shida gani! Maana hata hajitumi kivile.
Ni mpira mkuu
Tukubali matokeo
Tujipange upya
 
Shukrani sana min -me nimepokea li elfu 80 hapa la bia shukrani mwanangu
IMG_20250118_203056_502.jpg
 
Kwa Tathimini Yangu haya ndio mambo 10
1.Algers walikuja na mpango wa kuzuia kipindi cha kwanza.
Walipaki basi na Yanga wakashindwa kupress backline ya Algers.

2.Yanga hawakucheza kama team,
Kila mchezaji alitaka kuwa man of the match kitu ambacho kiliwaghalimu Yanga,Makosa ya Mzize kupiga mipira Hovyo yameikosesha Yanga nafasi muhimu.Nafikiri mzize aliagiza mzigo mpya dukani kwake.

3.Mashabiki wa Yanga hawakuitendea Haki mechi.
Mashabiki walipaswa kuujaza uwanja wa mpaka badala yake walioingia pia hawakua wkishangilia.

4.Musonda sio mchezaji wa mechi kubwa,

Musonda amefeli mapema sana leo ,sijui kwanini Kocha alimuacha akamaliza kipindi cha kwanza,Game ilimtaka Pacome zaidi.

5.Boka ni Beki wa kawaida sanaa,Lomalisa amekumbukwa leo.

Kross zake zote ziligonga mogongo ya mabeki na kutoka nje,wazili wa maji Lomalisa alikua bora zaidi

6.MC Alger na mbinu ya kupoteza muda.

Mwarabu huyu ni mwarabu upupu,amejiangusha sana,Amepoteza Muda ,zilipaswa kuongezwa zaidi ya dk 7

7.Kocha wa Yanga kutofanya Sabu.
Aucho alichoka mapema,
Duke abuya mechi ilimpasa kuingia kipindi cha pili. Kibabage alipaswa kuingia kumwaga maji zaidi ya boka.Dube mechi ilimkataa mapema chama angeiweza hii mechi.

8.Ally Kamwe ulefeli kwenye Hamasa.
Kitendo cha kushindwa kuujaza uwanja ni udhaifu wa Kamwe Ally.
Ilifika muda mpaka Manara akawa anamsaidia kupiga promo kwenye media ila hakufananya hivyo zaidi ya kujisifia yeye.Mashabiki wamezoea kwenda bureee.

9.Yanga inahitaji namba 9 aina ya Baleke,
Mipira mingi ilianguka ndani ya box la MC alger hakuwepo mmaliziaji,Nimemmkumbuka Baleke,Angewasaidia sana game ya leo.

10.Karibuni Kesho mjifunze kumfunga mwarabu nyumbani.
Kocha sijamuelewa kabisa leo, huyu Dube hapana ila kakomaa naye. Tuseme tu ni taaluma yake
 
Un

Unadhani ayo ni mashindano ya chandimu,,kwakuwa yanga kashindwa kusonga mtaongea mengi but iyo ni ligi ya mabingwa sio chandimu cup mliyopo nyie,,ubora wa vilabu vilivyopo uko ni tofauti na kwenu ivyo usitambe ukimaliza maneno!
Simba mbona walivuka miaka yote mkuu
 
Un

Unadhani ayo ni mashindano ya chandimu,,kwakuwa yanga kashindwa kusonga mtaongea mengi but iyo ni ligi ya mabingwa sio chandimu cup mliyopo nyie,,ubora wa vilabu vilivyopo uko ni tofauti na kwenu ivyo usitambe ukimaliza maneno!
Si ndio mnajisifu nayo kufika final.
 
Tofautisha CAFCL na Yale mashindano yenu ya UMISETA yaani shirikisho ni mashindano ya akina mama
Hayo mashindano ya akina mama
1. Ndiyo mashindano mnayojivunia mpaka sasa (kwenye Champion League bado hamjavunja record ya Simba)
2. Hayo mashindao ya wakinamama ndiyo mlicheza mpaka mkafika fainali
3. Hayo mashindano ya wakinamama ndiyo mpaka metegeneza documentary
4. Hayo mashindano ya wakina mama ndiyo mnazo mpaka medali zake
5. Hayo mashindano ya wakina mama ndiyo mpaka mashabiki wa Yanga na wachezaji walikula Supu Jangwani
Unafikiri kati ya Yanga na Simba hapo nani ni mama?
Hongera mwakakundi umejaribu😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛😛
 
Back
Top Bottom