Mambo 10 yanayothibitisha kwamba Mungu yupo

Tutahakikisha vipi na kuthibitisha vipi, Umetendewa hayo mambo na Mungu?

Na si imani zako uchwara tu.
 
Ibilisi yuko kazini. Ukiamini vitu vingine hashughuliki na wewe. Lakini akiona unataka kuanza kumwamini Mungu atakujaza mashaka na kukuambia hakuna ushahidi.
Ibilisi Hayupo.

Mungu hayupo.

Mungu na Ibilisi wote mmewatunga huko vichwani mwenu tu.
 
Kwahiyo wewe unataka uonyweshwe picha ya Mungu huko aliko au unataka upelekwe huko aliko?
Nataka aje mwenyewe ajidhihirishe na kujiongelea mwenyewe kama ana huo uwezo.

Sio nyie kupiga blah blah bla! Humu kumuelezea.
 
Wewe ndio unafosi Dunia iwe imeumbwa na huyo Mungu wako wa kufikirika.

Halafu ukiulizwa chanzo cha huyo Mungu ni nini, Hujui unaanza blah blah!

Thibitisha uwepo wa Mungu, Yeye kama yeye.

Sio kutumia vitu ambavyo tayari vipo kwenye existence vyenyewe, Kufosi kwamba viliumbwa na huyo Mungu wako wa kufikirika.
 
Ukitaka kuwathibitishia atheists uwepo wa Mungu watakusumbua na utakuwa unacheza muziki wao, Mungu ni wa kuaminiwa na si kuthibitishwa. Yapo mengi sana ya kutufanya tuamini Mungu bila shaka, ila atheists kwanza wanapinga imani sasa utamueleza vp Mungu nje ya imani? Yani wewe unamuamini Mungu ila wao wanataka umthibitishe Mungu nje ya imani.
 
Nataka aje mwenyewe ajidhihirishe na kujiongelea mwenyewe kama ana huo uwezo.

Sio nyie kupiga blah blah bla! Humu kumuelezea.
Kwahiyo huo ndio uthibitisho unaokusudia pale unapodai uthibitisho wa kuwepo Mungu?
 
Unataka proof gani kwa kitu ambacho hakipo?
Kitu hakiwi hakipo kwa sababu wewe umesema hakipo, mimi mbona naweza kukuthibitishia kwenye account yangu ya Yas by mix hakuna kiasi cha pesa cha milioni moja.
 
Kitu hakiwi hakipo kwa sababu wewe umesema hakipo,
Kama hicho kitu kipo, onyesha kipoje.

Sasa wewe unakataa kitu hakipo, Lakini kuonyesha kipoje huwezi.

Sasa unataka kitu kisiwepo, ilhali wewe mwenyewe umeshindwa kuthibitisha kipoje?

Sasa unataka nini?

Onyesha huyo Mungu yupoje?
mimi mbona naweza kukuthibitishia kwenye account yangu ya Yas by mix hakuna kiasi cha pesa cha milioni moja.
Kuthibitisha kwenye account yako ya "Mixx by Yas" hakuna kiasi cha pesa cha million moja, Si una onyesha balance ya account ndio tunapata uthibitisho na kuhakikisha kwamba kweli huna hicho kiasi cha millioni moja.

Sasa na huyo Mungu onyesha uwepo wake, yeye kama yeye, Yupo kwa namna gani?

Ii tuhakikishe uwepo wake.
 
Kama ni hivyo sasa humu unafanya nini?
Napinga madai yenu ya kusema kuna Mungu.

Ilhali huyo Mungu hawezi kujidhihirisha mwenyewe yeye kama yeye kwamba yupo.

Ni ninyi tu mnahangaika kumwelezea na kufosi uwepo wake.
 
Wewe umesema haiwezekani kuthibitisha kisichokuwepo ndio nimekwambia inawezekana kuthibitisha kisichokuwepo kwa mfano wa kuweza kuthibitisha kutokuwepo kwa milioni moja kwenye Mix by Yas.
 
Napinga madai yenu ya kusema kuna Mungu.

Ilhali huyo Mungu hawezi kujidhihirisha mwenyewe yeye kama yeye kwamba yupo.

Ni ninyi tu mnahangaika kumwelezea na kufosi uwepo wake.
Umejuaje hawezi kujidhirisha? Maana hapa tunajadiliana tu sisi.
 
Wewe umesema haiwezekani kuthibitisha kisichokuwepo ndio nimekwambia inawezekana kuthibitisha kisichokuwepo kwa mfano wa kuweza kuthibitisha kutokuwepo kwa milioni moja kwenye Mix by Yas.
Nimekwambia hivi, ili ithibitike kwamba huna million moja kwenye akaunti yako ya Mixx by Yas ni mpaka uoneshe salio/balance ya akaunti yako.

Usipo onyesha salio la akaunti yako haitawezekana kuthibitisha kwamba huna million moja kwenye akaunti yako ya Mixx by Yas.

Vivyo hivyo kwa huyo Mungu ukishindwa kuonyesha yupoje, Ni kwamba umeshindwa kuthibitisha yupoje.

Hivyo hayupo.
 
Kwa sababu Hayupo.

Angekuwepo angesha jitokeza kujidhihirisha na kufuta haya mabishano kuhusu uwepo wake.

Huyo Mungu angekuwepo kweli Kusingekuwa hata na haja ya kuhoji uwepo wake.

Kila mtu angejua kwa uhakika kabisa kwamba Mungu yupo.
Mbona Magufuli alikuwepo kipindi alipokuwa anatuhumiwa kuagiza kushambuliwa kwa Lissu ila hakujitokeza kujibu mwenyewe hizo tuhuma? Sasa iweje utake Mungu ajitokeze kisa sie tunabishana kuhusu yeye na kuhitimisha kuwa kwa sababu hajitokezi basi basi hayupo?

Kwa nini unaona ilitakiwa kuwa ni lazima kila mtu kujua uwepo wake? Kipi kinafanya iwe lazima iwe hivyo?
 
Ndio nimekwambia kwamba jambo la kuthibitisha kutokuwepo kwa milioni moja kwenye account ya mix by yas inawezekana, sasa wewe mbona unadai haiwezekani kuthibitisha kisichokuwepo?
 
Magufuli yupo na ilithibitika yupo.

Kwa hivyo huu mfano wako ni illogical.

Kwanza thibitisha Mungu yupo, Na si mawazo yako ya kufikirika tu na imani zako za kuaminishwa.
Kwa nini unaona ilitakiwa kuwa ni lazima kila mtu kujua uwepo wake? Kipi kinafanya iwe lazima iwe hivyo?
Magufuli alijulikana na kila mtu yupo na ilithibitika yupo, Na ushahidi wa uwepo wa Magufuli upo. Hata kaburi lake lipo.

Sasa Thibitisha uwepo wa huyo Mungu yeye kama yeye.
 
Ndio nimekwambia kwamba jambo la kuthibitisha kutokuwepo kwa milioni moja kwenye account ya mix by yas inawezekana, sasa wewe mbona unadai haiwezekani kuthibitisha kisichokuwepo?
Bila akaunti yako ya Mixx by Yas kuwepo, Hatuwezi kuthibitisha kwamba huna million moja kwenye hiyo akaunti yako ya Mixx by Yas.

Kwa hiyo kwanza lazima akaunti yako iwepo, ndipo sasa tuitumie kuthibitisha kwamba huna million moja kwenye hiyo akaunti.

Sasa huyo Mungu kwanza Hujathibitisha yupo, ila unakataa kwamba hayupo.

Sasa unataka nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…