Mstoiki
JF-Expert Member
- Oct 9, 2020
- 4,365
- 8,384
Nashukuru kwa majibu, Kulingana na maelezo yako ni kwamba Mungu ndiyo chanzo cha sisi na ulimwengu kuwepo si ndiyo?OK. Kwa ufupi, Mungu ni Muumba wa mbingu na dunia. Yeye ni mmoja tu, mwenye nguvu zote, upendo usio na kipimo, na mwenye haki. Mistari hii ya Biblia itakusaidia zaidi kujua Mungu ni nani:
Kama unapenda Mungu akuokoe sawa sawa na andiko hilo la Yn 3:16 fuatisha sala hii kwa dhati:
- Mwanzo 1:1: "Hapo mwanzo Mungu aliumba mbingu na dunia."
- 1 Yohana 4:8: "Mungu ni upendo."
- Isaya 45:5: "Mimi ni Bwana, hakuna mwingine, hakuna Mungu mwingine ila Mimi."
- Mfalme 1:18: "Bwana ni Mungu wa wote, na hakuna mwingine ila Yeye."
- Yeremia 10:10: "Bali Bwana ni Mungu wa kweli; Yeye ni Mungu aliye hai, Mfalme wa milele."
- Yohana 4:24: "Mungu ni Roho, na wale wamwabuduo Yeye lazima wamwabudu katika roho na kweli."
- Isaya 46:9: "Kumbukeni mambo ya zamani, maana mimi ni Mungu, wala hakuna mwingine, mimi ni Mungu, wala hakuna kama mimi."
- Yohana 3:16. "Kwa maana jinsi hii Mungu aliupenda ulimwengu, hata akamtoa Mwanawe wa pekee, ili kila aaminiye katika Yeye asipotee, bali awe na uzima wa milele."
Omba hivi:
"Ee Mungu, nimetambua wewe ni nani. Natubu dhambi zangu zote na kuziacha. Naamini wewe ndiye uliyeniumba na wewe ndiye uliyemtuma Yesu aje duniani atuokoe. Naamini kuwa Yesu ni Bwana na Mwokozi wetu. Nampokea Yesu sasa hivi kwa imani ndani ya moyo wangu atawale maisha yangu kuanzia leo. Katika Jina la Yesu Kristo. Amen"
Kama umeomba sala hiyo kwa dhati. Mungu amekusamehe na sasa unayo ahadi ya kuingia katika uzima wa milele. Ili ujifunze zaidi habari za Mungu na kazi zake, jiunge na kanisa lolote linalokiri wokovu na kufundisha utakatifu. Mungu akubariki. Nakutakia heri ya mwaka mpya.
Sasa Ningependa usichoke kunijibu maswali zaidi sababu nataka kujua;
1. Ikiwa Mungu ni mwenye upendo na mwenye nguvu zote kama ulivyoandika hapo kwa nini kuna dhiki na maumivu duniani?
2.Je, unaweza kuelezea kwa nini Mungu aliruhusu maovu kutokea, Wakati Yeye anapenda uzuri na ni mwenye haki?
3. Kwa nini watu wana imani tofauti kuhusu Mungu na dini, ikiwa Mungu ni mmoja tu?
4. Je, Mungu anajua kila kitu kinachokwenda kutokea? kwanini hua hadhibiti mapema mambo mabaya yanayokwenda kuwatokea watu wake mfano vimbunga, matetemeko, ajali, magonjwa n.k?
5. Je, alitokea wapi? Na kwasasa yuko wapi?