Mambo 12 yanayoipasua Tanzania vipande vipande kutoka utawala wa awamu ya 5

Wacha kutetea tumbo lako hapa!! Kama siyo nduli kwanini anamtesa Tundu Lissu kiasi hicho? Amempiga risasi 38 na 16 zikampata. Hajakamata suspect hata mmoja ndiyo maana unaamini anajua waliompiga Lissu. Amekataza wabunge wengine wasiende kumuona Lissu Hospitali, kwa nini nisimuite nduli. Amekataa kumlipia matibabu na mwisho kamnyang'anya ubunge. He is an animal, barbarian, vampire, shenanigan
 
Duh Stuxnet ama kweli umeamua kujilipua! Bado hujasikia tu hodi hapo nyumbani kwako kutoka kwa wale jamaa?
Ukikaa kimya utakufa, ukiongea utakufa pia. Bora waniue nikiwa nimeibua uovu wao ili hata nikifika huko kwenye maisha baada ya kifo niwe na sababu ya kuwaambia kwa nini nimekufa.

Dunia haiharibiwi na watu waovu, bali huharibiwa na watu wazuri ambao wanakaa kimya wakati maovu yakiendelea. (Albert Einstein)
 
Huna unachokijua unaongea matapishi tuu hapo, kaa kimya ndugu
 
Tuendelee kupaza sauti kila Mtanzania aelewe kuwa utawala huu siyo wa wanyonge kama wanvyojinadi bali ni utawala wa kifisadi na kimafia.
Tuna muamini Rais wetu wa awamu ya tano, tunapiga kazi kujenga taifa letu
 
Hiyo bei ni ya muda gani? unajuaje kama imebadilika au unaropoka ili uonekane una data kumbe mweupe kichwani
Usimjibu mpumbavu kadri ya upumbavu wake usije kuwa sawa na yeye... Mithali 26:4
 
Unajua sometimes nkisoma comments za hum ndani huwa najiuliza inakuwaje wote wanao-reply wanawaza kitu kimoja...? Hivi hizi data za kubuni mnazitoaga wapi..? Kweli umekaa ukaangalia ukajiridhisha mara BOT ipo chini ya familia moja, mara wanachukua ela muda wowote, mara magufuli ni mkabira mara uwanja wa ndege haujapitishwa na bunge, kwan miradi yote inayoendelea sasa hivi imepitishwa na bunge..?

Ndugu zangu upinzani upo na hautaisha lakini bas tujitahidi tuwe na hoja za kweli ambazo ni facts, na sio kuwachanganya watu akili kwa uongo ili mradi tu watu wamchukie kiongozi fulani.
 
Kama unakumbukumbu nzuri ata viongozi wa upinzani walikuwa wakisifia pale mwanzo kipindi cha vyeti feki na safisha safisha bandarini pale ila baada ya kuanza kudhibiti wapinzani kusema kweli mpaka yanayoendelea sasa kapoteza mvuto kwa watanzania
 
Wanaompimga Rais Magufuli Ni mafisadi na wauza madawa ya kulevya na wenye vyeti feki

Sisi Watanzania tunampenda Magufuli hao wachache wanajiangaisha
Kumbe makonda ni fisadi eeh ! si ana vyeti feki?
 
Nenda kasome Katiba kwanza ndiyo uje kuandika humu siyo kukimbia tu kwenye keyboard ya tecno na kuparaza paraza kama vile bata anakunya. Bunge ndilo lenye madaraka ya kuridhia (approve) matumizi yote ya Serikali kwa niaba ya wananchi. Serikali huomba tu kwa kuwakilisha bajeti na hili hufanyika kwenye kile kikao kirefu cha April- June.
 
Itasikitisha sana endapo hizi taarifa na shutuma zitakua na ukweli...


Cc: mahondaw
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…