Mambo aliyofanya Rais Samia ndani ya siku 503 za uongozi wake

Mambo aliyofanya Rais Samia ndani ya siku 503 za uongozi wake

1. Rais Samia amewezesha kuondolewa kodi (Zero rating) kwa mbolea inayozalishwa hapa nchini na mahitaji mengine muhimu ya wakulima kama vile mbegu, vifaa katika mashamba ya maua na mbogamboga n.k

2. Rais Samia amewezesha Kuondolewa kwa kodi katika malighafi zinazotumika kutengeneza mitungi ya gas hapa nchini ili kuchagiza matumizi ya nishati mbadala yenye gharama nafuu na inayotunza mazingira. 3. Rais Samia amewezesha kuondolewa kwa kodi zinazohusisha vifaa/mahitaji muhimu ya viwanda vya usindikaji wa nyama, maziwa na samaki.

4. Rais Samia amewezesha Mamalaka kama TRA kuwekeza katika teknolojia ili mambo kama kuhakiki madai ya ritani za VAT yafanywe kidijitali. Hii inalenga kuwezesha sekta binafsi kupewa stahiki za madai yao kwa wakati.


5. Rais Samia amewezesha kutambuliwa rasmi kwa njia mbadala za kifedha. Hii imelenga kuhakikisha ujumuishi katika huduma za kifedha kwa wananchi(Financial inclusion).

6. Rais Samia amewezesha asilimia 5 ya mapato ya Halmashauri kutumika kuboresha miundombinu ya wajasiriamali ili kuwawezesha wafanyabiashara ndogo ndogo kujikwamua kiuchumi. Rais Samia Suluhu amethibitisha kuwa kiongozi mwenye uwezo mkubwa na mwenye maono makubwa ya kiuongozi.

Mungu mlinde Rais wetu.
Tozo
Utitiri wa kodi
Kupanda kwa bei ya mafuta
Gharama kubwa ya maisha, etc
 
...ameweza kuweka tozo kwenye miamala ya fedha.
...ameweza kuigiza royal tour.
...ameweza kupandisha mishahara kwa asilimia 23.3 baada ya bwana yule kuwanyima haki yao watumishi wa umma.
...ameweza kuweka ruzuku kwenye nishati ya mafuta ili kupunguza ukali wa bei ya nishati hiyo muhimu.
...ameweza kurudisha wizarani mawaziri wengi waliotumbuliwa kuonewa na bwana yule.
...ameza kuleta anwani bora kabisa za makazi hadi jina langu MWANDENDEULE limepata kuwa jina la barabara hali si mtu maarufu hata nyumbani kwangu
 
Back
Top Bottom