Mambo ambayo biblia, Yesu, quran, Allah na Mohamed walidaganya wafuasi wao

Nimekuambia Qurani inakataza Muislam yoyote kumshukia kafiri silaha Ili amlazimishe kuiamini au kuifuata Qurani

Quran 2:256 -
Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua.


Na hayo maandiko uliyoweka hapo wagalatia wenzako wamekudanganya ndio maana wameyakata Ili wakudanganye

Ilitakiwa wakupe andiko likiwa hivi

Quran 2:190 -
Na piganeni katika Njia ya Mwenyezi Mungu na wale wanao kupigeni, wala msianze uadui. Kwani Mwenyezi Mungu hawapendi waanzao uadui.

Quran 2:191 -
Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipo kutoeni; kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri.


Waislam hawajahi kuanzisha vita ila walipigana na makafiri Ili kujilinda na kuondoa dhuruma waliyokuwa wanafanyiwa na makafiri
 
Hayo niliyoandika ni uongo ama ukweli, kama ni ukweli ndio uislamu ulivyo na ushahidi uko wazi tunauona Nigeria, Somalia, Yemen, Pakistan, Afghanistan nk.

Quran imesema na waislamu hizo nchi wanatekeleza quran inavyoelekeza
 
Hayo niliyoandika ni uongo ama ukweli, kama ni ukweli ndio uislamu ulivyo na ushahidi uko wazi tunauona Nigeria, Somalia, Yemen, Pakistan, Afghanistan nk.

Quran imesema na waislamu hizo nchi wanatekeleza quran inavyoelekeza
Nimekuuliza kwa nini unakata aya nje ya context? Unaelewa maana yake au unafata mkumbo kama wafuasi wa TB Joshua.
Umesahau kuweka Russia vs Ukraine,
Ireland kati ya wakatoliki na wasio wakatoliki, machafuko ya Congo, Ku Klux Klan kikundi cha Marekani, kikundi cha anti-balaka africa ya kati. Hayo yote ya kikristo.
Makundi yapo mengi tena wanaweka mabwana zenu wenyewe BBC na CNN.
Mlivyokuwa mazezeta mnafuata vitu kibubusa bila akili.
 
Kupewa mabikra 72
 
Israeli ipi? Hili la Wazungu wafuasi wa Ushoga na Ulawiti? Ukiangalia hii Israeli in sifa zilozoainishwa ktk Biblia? Hili ni Sinagogi la Shetani.

Labda tusikilizie Israeli nyingine lakini siyo Hilo Taifa bandia la Wazungu Mashariki ya kati.
 
Kwahiyo una amini Yesu alikuwepo?
 
Kwahiyo una amini Yesu alikuwepo?
1. Kuamini si kitu muhimu. Kila mtu anaruhusiwa kuamini anachotaka. Kiwe cha ukweli au uongo.

2. Unaposema "Yesu alikuwepo" una maana gani? Kwamba kuna mtoto alizaliwa na Mama anayeitwa Maria miaka kama 2,000 iliyopita akaishi huko pande za Israel ya leo si jambo la ajabu na kuna vyanzo tofauti na vitabu vya dini vinatueleza hilo. Josephus kaandika, history, ya Warumi, si dini. Ingawa na yeye maandiko yake yalichakachuliwa kidini baadaye.

Josephus kaeleza mpaka kwamba Yesu alikuwa na kaka yake anaitwa James. James alienda kuuawa kwa kupigwa mawe akiwa na miaka 69. Pia Yesu alikuwa na dada zake wengine wawili ambao hawajatajwa kwa majina.


Tatizo linakuja mkianza kuweka habari za miujiza, habari za Yesu kufa na kufufuka, kufufua watu, etc. That becomes a problem.

Tuangalie vitu vinavyoweza kuwa verified historically. Historia huwa inatumia misingi fulani ya kuthibitisha kama mtu fulani alikuwepo kweli, mambo fulani yalitokea kweli. Haya tunaweza kuyathibitisha, si habari ya kuamini au kutoamini.

Hii ni habari ya kuthibitisha kihistoria au kutothibitisha.

Yesu kuwapo wala si issue, issue ni hayo mazagazaga ya miujiza ambayo hayawezi kuthibitishwa.
 
Kuna mengi ya kukujibu hata hivyo kwa sasa nachagua kukujibu suala moja la Mathayo 24:34.

Neno kizazi katika Biblia mara kadhaa limetumika kuonesha ubora/quality ya watu katika kumuishia Mungu.

Mfano; Mathayo 23:34-36

Kwa sababu hiyo, angalieni, mimi natuma kwenu manabii na wenye hekima na waandishi; na wengine wao ninyi mtawaua na kuwasulibisha, na wengine wao mtawapiga katika masinagogi yenu, na kuwafukuza mji kwa mji; 35hivyo ije juu yenu damu yote ya haki iliyomwagika juu ya nchi, tangu damu ya Habili, yule mwenye haki, hata damu ya Zakaria bin Barakia, mliyemwua kati ya patakatifu na madhabahu. 36Amin, nawaambieni, Mambo hayo yote yatakuja juu ya kizazi hiki.

Huo mstari hapo juu anazungumzia hukumu itakayoletwa juu ya wale anaowaita kizazi hiki kutokana na matendo waliyotenda tangu kuuawa mtu wa kwanza Habili maelfu ya miaka iliyopita.

Na Yohana Mbatizaji aliwahi kuita watu wa aina hii kizazi cha nyoka.
Mathayo 3:7. Lakini alipowaona Mafarisayo wengi na Masadukayo wanamjia ili awabatize, aliwaambia, “Enyi kizazi cha nyoka! Ni nani aliyewadokezea muikimbie ghadhabu inayokuja?

Kama ungetafsiri literally maana yake wale mafarisayo na masadukayo waliomjia Yohana Mbatizaji walizaliwa kutokana na nyoka lakini sivyo badala yake anamaanisha ni aina ya watu walio kinyume na Mungu na nyoka katika Biblia mara nyingi humaanisha Shetani.

Kwa hiyo kizazi kilichotajwa na Yesu kwenye Mathayo 24:34 ni aina ya watu waliojaa ukaidi dhidi ya kweli ya Mungu tangu enzi ya Adam na Hawa.

Hata hivyo yako mambo mengi aliyosema Yesu katika Mathayo 24 ambayo yametimia tayari. Mfano;

  • Kubomolewa kwa hekalu aliposema halitasalia jiwe juu ya jiwe. Hekalu lilibomolewa around 70AD
  • Kutokea kwa makristo wa uongo na manabii wa uongo. Hili si ajabu wengi ni mashahidi kuwa ni suala linaloendelea hata sasa hivi.
  • n.k.
 
Kitabu chochote kinachohitaji tafsiri si cha Mungu, na kitabu cha Mungu hakihitaji tafsiri.

Hivyo, ukishaanza habari za tafsiri tu, unachoniambia hapo ni kwamba unatafsiri habari za watu, si za Mungu.

Mungu muweza yote asingeshindwa kuweka habari iliyonyooka ambayo haihitaji tafsiri za kuungaunga.

In fact ukishaona habari kwenye kitabu tu, jua hiyo ni ya watu tu, si ya Mungu.

Kwa nini Mungu atumie kitabu wakati ana teknolojia ya DNA kutufikishia chochote anachotaka?
 
Mathayo 13:34 - 35
Hayo yote Yesu aliwaambia makutano kwa mifano; wala pasipo mfano hakuwaambia neno; ili litimie neno lililonenwa na nabii, akisema, Nitafumbua kinywa changu kwa mifano, Nitayatamka yaliyositirika tangu awali.

Hiyo elimu ya kusema kitabu kinachohitaji tafsiri si cha Mungu umeitoa wapi? Ni Mungu gani alikupa hiyo elimu? Yani unampangia Mungu jinsi ya kufikisha ujumbe kwa watu aliowaumba yeye mwenyewe?
 
Ni logical consistency tu.

Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote akiwapo, atawapa viumbe wake namna bora kabisa ya kumjua yeye Mungu. Mungu huyo pia ataondoa utata wowote kwenye suala la kumjua yeye ili watu wake wasipate kupotoka.

Maandiko ya kwenye vitabu yana matatizo mengi ya utata, tafsiri etc.

Hatujaondolewa maandiko yenye utata wala kupewa njia isiyo na utata ya kumjua Mungu.

Hivyo, Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote hayupo.

Angekuwepo, angetuondolea njia zote zenye utata kumjua, na angetupa njia isiyo na utata kumjua.

Ukielewa logical contradiction ni nini, utaelewa nilichoandika.

Kama huelewi, unaweza kusoma mara mia usielewe.
 
Mi naona we ndo hauna akili, kwa sasa unawaza namna ya kupara bwana tu sawa na maagizo ya papa wenu.
 
Mi naona we ndo hauna akili, kwa sasa unawaza namna ya kupara bwana tu sawa na maagizo ya papa wenu.

Sasa hasira za nini mzee?
Wewe unaambiwa mbinguni kuna mto wa pombe isiyolewesha[emoji28] na wewe unakubali tu kama zombi. Kwamba kuna mabikra 72 wana macho kama vikombe. Huko peponi mnaenda kucheza X? Upuuzi mtupu
 
Mi naona we ndo hauna akili, kwa sasa unawaza namna ya kupara bwana tu sawa na maagizo ya papa wenu.

Sasa hasira za nini mzee?
Wewe unaambiwa mbinguni kuna mto wa pombe isiyolewesha[emoji28] na wewe unakubali tu kama zombi. Kwamba kuna mabikra 72 wana macho kama vikombe. Huko peponi mnaenda kucheza X? Upuuzi mtupu
 

Kama ambavyo Mungu muweza wa yote hawezi kufanya maisha yako yawe marahisi katika utafutaji mpaka upambane, ndivyo ilivyo katika mafundisho yake.

Maandiko yanaagiza kumtafuta kumjua sana Mungu na ndipo mema yatakapokujia. Hivyo huwezi kukaa tu kizembe ukamjua/ukamuelewa Mungu. Lazima ufundishwe, usome na ukubali kujifunza.
 
Ukishasema Mungu muweza yote hawezi kufanya maisha yangu yawe rahisi katika utafutaji, umeshakubali Mungu muweza yote hayupo.

Unaelewa hilo?

Unaelewa contradiction uliyojiingiza katika kuandika maneno uliyoyaandika?

Hebu kuwa serious kidogo.

Mungu muweza yote halafu hapo hapo hawezi tena?
 
Ujumbe wa Mungu kupitia Biblia ni simple.
  • Mungu alimwumba mwanadamu kwa ukamilifu
  • Mwanadamu alitumia uhuru na utashi wake kumuasi Mungu
  • Mungu aliandaa taifa ili amlete mwokozi wa mwanadamu
  • Yesu alikuja, akafanya kazi ya wokovu
  • Imebaki kwa mwanadamu kumwamini na kumpokea Yesu ili apokee wokovu
Sasa Biblia nzima imeelezea namna gani Mungu ametekeleza mpango wake wa wokovu, kupitia vitabu vya manabii, vitabu vya wafalme, vitabu vya hekima kama Mithali na nyimbo kama Zaburi n.k.

Ukisoma Biblia kama mtu mwenye elimu ndogo kabisa unaweza kumjua Mungu, na ukitaka kusoma Biblia kwa undani na kufahamu mambo mengi zaidi pia utamjua Mungu.

Inawezekana yako mambo machache yanayohitaji ufafanuzi hilo sio shida ndo maana kuna watu wanasoma Biblia na Theology mpaka level za PhD kwa lengo la kuwasadia wengine na kuimarisha Imani zao. Lakini hauhitaji Degree ya Biblia au Theology kumjua Mungu kuwa na uhusiano binafsi na yeye.

Unachohitaji ni kuwa na moyo wa kujifunza na unyenyekevu ndivyo utakavyo saidika. Lakini ukiamua kuwa mkaidi hata kama kila kitu kingekuwa as plain as possible bado utamkataa Mungu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…