Mambo ambayo mwanaume akifanya Mwanza/ Usukumani, jamii yote itamshangaa

View attachment 3664234
Ngoja nikwambie mambo ambayo huko Mwanza ulikuwa ukiyafanya unaonekana wa ajabu...!

1. Mwanaume kula viazi mchana kama chakula... mwanaume kama alikuwa anakula viazi basi viwe vimechomwa 😂

2. Kupika dagaa wana vichwa..

3. Kwenye msiba watu kula majurijuri... majurijuri ni wale watoto wa sangara..ilikuwa dalili ya umaskini wa kutupwa

4. Kwenye sherehe watu kula na maharage bila kaugali na nyama 🤣😂 hii itaingia kwenye rekodi ya sherehe mbaya 😂🤣

5. Kumuuliza mgeni kama hajala umpikie.... aisee atasimuliwa na kutangazwa kijiji kizima

6. Mwanaume kuuliza mke wake kama ile mboga aliyoleta asubuhi imekwisha... hii ilikuwa dalili ya gubu na uchoyo 😂🤣

7. Kula maharage kama mboga... maharage yalikuwa yanaliwa kama snacks tu wakati mnasubiria chakula 🤣😂

Hebu tuambie huko kwenu ni mambo gani mtu alikuwa akifanya anaonekana wa ajabu...!?
Mengi ya uliyoandika yalikuwa ya ajabu pia UJITANI.
10. Kumtuma mwanamke akanunue kitoweo lilikuwa jambo la ajabu sana na lisilowezekana.
 
View attachment 3664234
Ngoja nikwambie mambo ambayo huko Mwanza ulikuwa ukiyafanya unaonekana wa ajabu...!

1. Mwanaume kula viazi mchana kama chakula... mwanaume kama alikuwa anakula viazi basi viwe vimechomwa 😂

2. Kupika dagaa wana vichwa..

3. Kwenye msiba watu kula majurijuri... majurijuri ni wale watoto wa sangara..ilikuwa dalili ya umaskini wa kutupwa

4. Kwenye sherehe watu kula na maharage bila kaugali na nyama 🤣😂 hii itaingia kwenye rekodi ya sherehe mbaya 😂🤣

5. Kumuuliza mgeni kama hajala umpikie.... aisee atasimuliwa na kutangazwa kijiji kizima

6. Mwanaume kuuliza mke wake kama ile mboga aliyoleta asubuhi imekwisha... hii ilikuwa dalili ya gubu na uchoyo 😂🤣

7. Kula maharage kama mboga... maharage yalikuwa yanaliwa kama snacks tu wakati mnasubiria chakula 🤣😂

Hebu tuambie huko kwenu ni mambo gani mtu alikuwa akifanya anaonekana wa ajabu...!?
Kule kwetu mwanaume upate jando alafu eti wazee waache kukutengenezea mchanganyiko wa damu mbichi na maziwa mtindi labda hao wazee ni aibu ya ukoo mzima.
 
Nimekula sana wanawake wa kisukuma na viushanga vyao
 
pia ni mwiko usukumani ndume kuoga kila siku bila sababu za msingi!
 
Huko kwetu ilikuwa kula ugali ni dalili ya umasikini na maisha kuwachapa sana. Ila kwa sasa ugali na wali ndio kimbilio migomba imenyauka ndizi bei hazishikiki kwa sasa watoto wa kizazi hiki wanapenda ugali kuliko ndizi maana wameuzoea.
Bila shaka ni mkoa wa Kagera
 
Back
Top Bottom