Mkuu, nashukuru kwa sehemu kukubaliana na kutokubaliana. Lakini Mkuu umeona mahali popote nimeingiza Dini? Nimekupa facts ambazo hazikataliki, Hamas is religous organization, hilo halipingiki. Nimekupa narrative yangu, angalau kuanzia 1947, na wewe umeleta ramani za mgao wa UN hapo mahali, nimeandika angalau matukio ya Vita ambayo yamefanya expansion ya Wayahudi.
Ni kweli mkuu, lazima uwe na huruma tunachoona kinatokea Gaza na Israel pia! Mtu mwenye akili timamu huwezi kushabikia mauji yoyote yale, Middle East especially swala la Waarabu na Wapelestina ni complex mno! Lina dini, lina historia, lina interests za mataifa ya nje, Waarabu na Marekani, sio leo from Second World 2. Ukichanganya hayo yote, ni vigumu kulitatua.
Kumbuka kuna mikutano mingi mno ya kimataifa imeshindwa! Hata Waarabu wenyewe kuna mahali wanatofautiana kabisa, in actually sense kuna ushahidi huwa wanauza siri za Palestine Kwa Israel...Ni confusion tupu mkuu!
Mimi mtazamo wangu ni kuwa Wote Waarabu na Wayahudi wana historical attachment hapo! Hilo halipingiki! Dini zao Islam na Judaism zina mambo kwa sehemu zinashabikiana, ingawa tena radically zinatofautiana kabisa, akili za Mwarabu ziko radically different, Mwarabu anaongozwa kwa Jazba, Myahudi anakaa na kutakari (Mtazamo wangu) Hii inachangai mno katika kutatua ugomvi huo.
Hivyo let me pause here kwenye hii Mada, labda tuone hii cease fire italeta nini. Thanks to engage with you.