Mambo ambayo ukifanya watu hawatasita kukuua. Bila kujali Sheria zipo au hazipo, Mungu yupo au hayupo

Sijaona mtu kupasuliwa yai.
 
Kweli kabisa Mkuu, mazoea ni mabaya sana hata Mimi mtaani kwangu kuna vijana wengi sana lakini niliowazoea kama 10 tu tena kwa sababu maalumu
Kwa kifupi ni kwamba wanaume serious hawapendi mazoea.

Hata humu, walio kando wakiona huyu serious wajinga wajinga wanataka kuwaletea mazoea. Utaona wana ku-quote mpotezee huyo taahira.

Sasa wajinga-wajinga uwa hawaelewi hilo somo.
 
Mungu hazai bali Mungu huumba....zinaa au tendo la ndoa ndio ya pekee ya Mungu kupitisha uumbaji wake.......hivyo Mungu anawajibika na anahusika katika uumbaji na sio uzalishaji


Uwajibikaji wa khiyari ni ule ambao uhusika wako juu ya jambo haupo moja kwa moja.....na uwajibikaji wa lazima ni ule ambao uwajibikaji wako ni wa moja kwa moja kwenye jambo husika......umehusika kwenye kumtongoza mwanamke na ukapanga miadi ya kuzini naye lazima uwajibike kwenye matokeo yake........


Kwa mimi nijuavyo urithi ni lazima kwa mtoto.....kwa kuwa urithi anarithiwa aliyekufa......
 
Nilitegemea hiyo namba 1 iwe ukiipinga CCM
 
Mungu hazai bali Mungu huumba....zinaa au tendo la ndoa ndio ya pekee ya Mungu kupitisha uumbaji wake.......hivyo Mungu anawajibika na anahusika katika uumbaji na sio uzalishaji
Mungu anahusika na suala la uombaji, ukuzaji, Mpaka mtoto anazaliwa

Mimba haiwezi kutungwa bila Ruhusa ya Mungu.
Ila mtu anaweza kufanya ngono kwa matakwa yake ila hawezi kuzaa kwa matakwa yake.

Alafu tendo la ndoa sio Njia pekee ambayo Mungu anaweza kuitumia kufanya uumbaji au kuleta Duniani watu wake.

Hili sijakataa.
Ila suala la Urithi na Baraka sio jukumu la lazima la mzazi kwa mtoto.
Hata aliowalea sio lazima awape Urithi au Baraka.
Urithi na Baraka ni suala y hiyari(mapenzi) ya mzazi kwa Mtoto.


Kwa mimi nijuavyo urithi ni lazima kwa mtoto.....kwa kuwa urithi anarithiwa aliyekufa......

Urithi sio lazima kwa mtoto
Urithi ni hiyari(mapenzi) ya mzazi kwa mtoto ambaye anampenda na aliyependezwa naye.

Ndio nikakuambia, Mungu mwenyewe anahiyari ya wewe ukizaa watoto wakurithi sura yako au maumbile yako au wasikurithi ni hiyari yake yeye anayeumba sio lazima.
Ndio maana unaweza ukazaa watoto na usifanane nao,

Kwenye Urithi wa kimazingira, Kama Mali, mzazi anaweza asikurithishe chochote kile na isiwe kosa kwake.

Nafikiri somo la HAKI bado linawapiga wengi Chenga.

Baba hutoa Urithi kwa watoto kwa hiyari, kwa mapenzi. Na sio wajibu wake kufanya hivyo. Yaani hakuna sheria popote iwe ya kiroho au ya dunia itakayomuwajibisha.

Ndio maana huwezi kwenda kwa Babaako kumdai Urithi wako, au kudai Baraka zako.
Ila utadai mahitaji ya msingi kama chakula, sehemu ya Kulala, mavazi na siku hizi Elimu.
Na hapo ni ukiwa mtoto.

Ukiwa Mkubwa mzazi wako Hana wajibu wowote kwako, ndio maana hawezi kukuamulia Maisha yako, Yale aliyokufundisha unahiyari ya kuyafuata au kuyapuuza.

Urithi mtu anaweza kukupa hata Akiwa HAI.
Anaweza kukwambia nikiondoka wewe ndiye utakuwa mmiliki wa hii nyumba,
Hivyo nyumba Ile umerithishwa tangu Mzee Akiwa hai kwa sharti itakuwa yako siku atakapokufa.

Najua ukweli huu wengi hawautaki ila ndio iko hivyo, Mtoto wa nje, ambaye hujamlea, hujaishi naye hawezi kuwa mtoto wako kimazingira. Na huwezi kumbariki na Baraka zako zikashika.

Baraka za wazazi haziishii tuu mdomoni Bali zinategemea zaidi connections kutoka rohoni baina ya mtoto na mzazi.

Kumbuka mtoto ambaye hujamkuza wewe au hajakuzwa na Baba Hana connection(bond) mapenzi na Baba yake.
Halikadhalika na upande wa mtoto ambaye hajakuzwa na Mama yake.

Baraka sio tuu kumtamkia Mtu.

Kuna swali watu wengi wanauliza, kwa nini waafrika wengi hawawezi kuendeleza Mali walizoachiwa na Baba au Babu Zao. Jibu lake lipo katika Mada hii.

Huwezi kurithi au Kupata Baraka ambayo huna connection nayo
 

Anayerithiwa ni yule aliyekufa sio Kwa walio hai.....na aliyekufa hana chake duniani Bali kwa waliokuwa hai ndio maana upo utaratibu wa kidini au wa kisheria za nchi za mgawanyo hizo mali alizoacha marehemu.......

Huwezi kwenda kwa Baba yako udai urithi angali yupo hai......

Hapa suala la msingi sio bond baina ya Baba na mtoto suala la hapa ni kuwa wewe ndio kisababishi cha huyo mtoto kuja duniani....na kama wewe ndio Baba kwanini ukwepe kuwajibika kwenye maamuzi yako au matokeo ya kitendo chako......??

Kama ni muadilifu na mjuzi wa kukimbia wajibu wako kwanini umefanya uchafu na kukileta kiumbe ambacho hakijakuomba ukilete.....??

Kama unaipenda familia yako kwanini unashindwa kujidhibiti na kusababisha mateso kwa wengine kwa matendo yako maovu....??

Hata kama mama mtoto analeta ugumu na mtoto anahitaji huduma yako basi tumia mbinu nyingine kufikisha huduma na sio kutafuta sababu ya kukimbia wajibu wako.....

Mtoto kuwa hakuletwi na mazingira bali kwa uthibitisho wa kinasaba pekee kama kuna sintofahamu baina ya wewe na mama yake.........

Kama umeruka ruka na kusababisha ujio wa kiumbe hapa duniani basi niwajibu wako kuhangaika na hatima ya hicho kiumbe chini ya jua.......

Iwe umemlea au hujamlea as long as wewe ndio kisababishi cha uwepo wake duniani basi ana haki kwako.....na kama unadhani kuwa ni kero basi jidhibiti matamanio yako hali ya kuwa una na watoto........
 
Mgema akisifiwa sana tembo hutia maji, Sasa umeanza kujiandikia tu ilimradi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…