Mambo ambayo ukifanya watu hawatasita kukuua. Bila kujali Sheria zipo au hazipo, Mungu yupo au hayupo

f) Uasi Jeshini.
Wewe ni Mwanajeshi, labda ukaona Jambo Fulani linaenda ndivyo sivyo. Ukaamua kushawishi wenzako wenye mtazamo kama wako. Kaa ukijua Mchezo unaoenda kuufanya ni vita ya Kifo na uhai. Kuuawa ni njenje.
Ukiweza kufanikiwa kuikwepa mifumo ya ulinzi ndani ya Jeshi, unaweza ukaasi vizuri sana mkuu..

Kwa nchi za dunia ya tatu, hii itahitaji zaidi msaada kutoka nje ya nchi, hususan kwa wazungu..
 
Mtibeli umesahau Uchawi
Ukidhibitika wewe ni Mchawi na umeiletea madhara jamii inayokuzinguka watakuua bila kujali Sheria za jaji ibrahimu juma
 
KISIASA,
a) Uhaini, kufanya mipango ya kumuua Mfalme au Rais, kuratibu au kushiriki mipango hiyo. Kwa namna yoyote Ile.
Watakuua nakuhakikishia, kama wewe ulivyopanga kumuua au kumpindua mfalme Basi tegemea matokeo makubwa ya Hatari yatakayokurudia.
Mbona Mbowe hakukuuwawa? Odinga pia alishiriki kumpindua Moi ila hakuuwawa?
c) Kuungana na Adui wa Nchi.
Mfano, Korea Kaskazini na Kusini. Wewe ni Mkorea Kusini lakini unaunga Mkono Korea Kaskazini au kinyume chake. Watakuua mchana kweupe.
Mbona Trump anamhusu Putin na hamna kitu amefanywa? Nadhani ungesema nchi za kiafrika ila huko nje sio kweli. Mbona Prince wa saudia alifanya peace na Israel ila hajauwawa?
Kuipasua nchi.
Mfano nchi ya Tanzania, ufanye Njama igawnyike Mapande Mapande kama vile Sudan Kusini na Sudan Kaskazini. Watakuua nakuhakikishia. Labda uwe na bahati Sana uchoropoke. Au uwe umewazidi mipango, mikakati na mbinu.
Sio kweli, Nyerere alisupport Biafra ili wajitenge na Nigeria ila hakuuwawa. Same to Ali Hassan Joho alitangaza 2018 kuwa Mombasa inajitenga na Kenya na akawa anadai referendum ila hakuuwawa.
 
Unapotosha mkuu, labda ungesema ina depend political influence yako ndio inapimwa. Huko DRC mbona wanasiasa wengi tu waliunga mkono Kivu ihamishwe Rwanda na hakuna aliyeuwawa?. Au kule Ukraine wapo wengi tu walimuunga mkono Donbass kujiunga na Russia ila mbona hawakuuwawa?
 
Wizi
Kukwepa madeni makubwa
Kulawiti watoto wa watu
Ukandamizaji
 
Pumba tupu.
 
Hayo mengine mnajitungia tu. Mungu alipiga marufuku mambo 10 tu, kwa mujibu wa biblia.
 
Hayo mengine mnajitungia tu. Mungu alipiga marufuku mambo 10 tu, kwa mujibu wa biblia.

Nafikiri Biblia huijui vizuri.

Yale mambo 10 ni muhtasari tuu ambao umefafanuliwa kwenye Biblia nzima, Quran na Sheria za kila Nchi
 

Hivi hiyo vita inayoendelea hapo Congo na Huko Ukraine maelfu ya watu wanavyokufa unafikiri ni Jambo gani linapelekea vifo vyao kama sio Masuala ya mipaka ya ardhi?

Vita ya Kagera unajua Moja ya sababu zake ni uvamizi wa maeneo ya Tanzania yaliyotaka kuporwa na Amin
 
Watu wanafanya Kazi alafu wewe unapuliza tunguli kila siku mambo ya wenzako hayaendi.

Au mtu anafanya Kazi kwenye kampuni Fulani alafu kumbe kuna mfanyakazi au rafiki anamfanyia Fitna afukuzwe Kazi. Utauawa nakuambia
nakazia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…