Doctor Mama Amon
Platinum Member
- Mar 30, 2018
- 2,311
- 3,513
Bunge la Umoja wa Ulaya limezitaka mamlaka za Tanzania kufanya mambo yafuatayo:
- Kukomesha msako unaoendelea dhidi ya wakosoaji wa serikali,
- Kukomesha ukamatwaji holela wa raia,
- Kukomesha vurugu za kisiasa zinazofanywa na vyombo vya dola,
- Kukomesha mashambulizi na unyanyasaji dhidi ya wanachama wa upinzani,
- Kukomesha unyanyasaji dhidi ya watetezi wa haki za binadamu, zikiwemo haki za kisiasa, kiuchumi, kijamii na kijinsia kwa kila kundi lenye wasifu wa kijinsia unaotambulika kisayansi.
- Kukomesha unyanyasaji dhidi ya watu wa asili kama vile Wamasai wa Ngorongooro,
- Kukomesha unyanyasaji dhidi ya waandishi wa habari wanaoikosoa serikali,
- Kukomesha unyanyasaji dhidi ya mashirika ya kiraia yanayoikosoa serikali,
- Kufanya uchunguzi huru kuhusu ukiukaji wa sheria unaofanywa na polisi yakiwemo matukio ya watu kupotezwa na watu wasiojulikana,
- Kuheshimu utawala wa sheria,
- Kuheshimu uhuru wa kujieleza,
- Kuheshimu uhuru wa vyombo vya habari,
- Kuheshimu uhuru wa vyama na mikutano yake, na
- Kuheshimu uhuru wa mahakama,
- Kuwianisha sheria za uhalifu wa mtandaoni za Tanzania na sheria za kimataifa za haki za binadamu,
- Kuwianisha sheria za vyombo vya habari za tanzania na sheria za kimataifa za haki za binadamu
- Kuheshimu haki za vyama vya siasa, na
- Kuhakikisha chaguzi huru na za haki;