Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

Kimeshajulikana na ndiyo maana anapelekwa Jafo kupiga pasi.

Labda hujamsikiliza vizuri Rais mama Samia.

Kumbuka tu na elewa tu, Kariakoo kuna Reforms na Rebuilding kubwa zinaendelea.
Haya dada nimekuelewa. Ngoja tusubirie hizo reforms hapo kariakoo.
 
Haya dada nimekuelewa. Ngoja tusubirie hizo reforms hapo kariakoo.
Unasubiria? kweli una macho lakini hayaoni, una masikio lakini hayasikii. Hivi huelewi kuwa sasa hivi kariakoo inajengwa upya na soko la zamani sasa lipo asilimia 99? Watu wanawekwa sawa wahamie tu.

Na area nzima ya Kariakoo, kila mahali kuna Rebuilding na reforms za ajabu, haijawahi kutokea, unaishi mkoa gani?

Ikiwa huyaoni yanayoendelea basi hata kusikia husikii? utasubiri sana. Jikumbushe:


View: https://youtu.be/yx2bAloztJU?si=zqOmircmU2qo056L
 
Ukiwa biased hutoziona.

Tanzania ya leo ndiyo uliyokuwa nayo miaka 5 nyuma?

Unaziishi "Reforms" lakini huzioni, nafahamu ni "mentality" ya kitumwa uliyonayo, ya kukaripiwa karipiwa kuanzia unaanza kusoma shule mpaka kazini na bosi wako, kanisani ndiyo usiseme, mchungaji mpaka koo linakauka kwa kukaripia. Ukirudi nyumbani mumeo au mkeo kwa kuwa katokea mazingira hayohayo ya kitumwa , ya kujazwa ujinga, nae anakukaripia. Kwa kuwa umezowea hayo sasa umepata Rais wa vitendo asiyekaripia, hata mabadiliko "Reforms" kubwa anazozifanya na unaziishi lakini sikushangai huzioni.

Tazama tarehe ya hiyo hilo kongamano ukapate darsa la "Reforms" ni nini, kwa ufupi, unatakiwa wewe mwenyewe uanze kuji-"reform" ndipo utakapoziona "Reforms" kwa upana wake.
Tatizo lako unaongelea social reforms ambazo zinategema na desturi ya nchi, mambo ya kufokewa ni sehemu ya Mila za kiafrika katika maonyo. Sio Jambo la kuhitaji reforms.

Reforms ninazo ziongelea ni political na economic reforms ambazo mwisho wa siku zinaweza kubadilisha mambo mengi. Reforms sio maneno Bali matendo. Na reform ya kwanza ni Katiba mpya na Sheria. Bila kufanya constitutional reforms hakuna reforms za maana zitakazo kuja.

Ile Rasimu warioba tungeipitia na kukubali Leo Tanzania ingekuwa na reforms sio ngojera za reforms wakati hata Kodi huwezi kukusanya na bado unakopa tu. Kwangu Mimi ni constitutional reforms no reforms
 
Nchi imemshinda, ni kama mfa maji sasa hajui pa kushika. Its very unfortunate tuna kiongozi wa namna hii. Kwanza tumeshajua mwananke kazi yake kupika na kumfurahisha mumewe, hafai kuongoza nchi. 2025 asirudi, tunataka kiongozi anayejua nini anataka ili kuleta maendeleo kwa watu wake, kiongozi bold anayeweza kusimamila rasilimali za nchi, kuondoa wizi na ufisadi uliokithiri nchini.
Kweli kabisa. Tunataka Rais mwenye vision ya kuipeleka Tanzania mbele, Kama alivyokuwa Magufuli.
 
Unasubiria? kweli una macho lakini hayaoni, una masikio lakini hayasikii. Hivi huelewi kuwa sasa hivi kariakoo inajengwa upya na soko la zamani sasa lipo asilimia 99? Watu wanawekwa sawa wahamie tu.

Na area nzima ya Kariakoo, kila mahali kuna Rebuilding na reforms za ajabu, haijawahi kutokea, unaishi mkoa gani?

Ikiwa huyaoni yanayoendelea basi hata kusikia husikii? utasubiri sana. Jikumbushe:


View: https://youtu.be/yx2bAloztJU?si=zqOmircmU2qo056L

Nani kakataa. Nimesema ngoja Hilo soko lianze tuone hizo reforms na rebuilding. Ila Mimi naona hizo 4Rs ni za mchongo tu. Rs za ukweli zipo kwenye Rasimu ya Warioba.
 
Nani kakataa. Nimesema ngoja Hilo soko lianze tuone hizo reforms na rebuilding. Ila Mimi naona hizo 4Rs ni za mchongo tu. Rs za ukweli zipo kwenye Rasimu ya Warioba.
Ungoje nini wakati mambo motomoto, unaziishi Reforms, unasikitisha sana kuwa huzioni.
 
Umejitaidi kugeuza geuza hoja zionekane mbaya ila pumba tuh umeandika ,,hoja kama ya rais kujua tra wanaiba asa hilo c kila mtu anajua ulitaka awe mnafki asiseme ?
Wakati Rais Samiah akiwaapisha Viongozi Jana , Kuna mambo matano aliyasema kwenye hotuba yake ambayo yalinisikitisha.

1. Jambo la kwanza Rais kadai mikopo inaifanya Tanzania inyayasike

Nimehuzunika Rais anapokiri ya kwamba mikopo tunayokopa inatufanya tunyanyasike. Huyu ni udhaifu mkubwa wa Rais wa Nchi kukiri hadharani ya kwamba anapoenda kukopa huko nje huwa ananyanyasika. Kwa maana nyingine Rais amekiri kwamba hii mikopo Ina masharti magumu kabla ya kukopa na hata baada ya kukopa yanayoifanya nchi inyanyasike Kama alivyosema Rais.

Pia kwenye muktadha huo, Rais kadai tunakopa nje na kunyanyasika kwa sababu watu hawalipi Kodi. Kwa maana nyingine Rais alikuwa anajua Kodi hazilipwi ila akawa anafidia kwa kukopa mikopo huko kwa wanyanyasaji, Sasa unyanyasaji umekidhiri kaamua kudai Kodi ilipwe.

Swali langu kwa Rais kwanini unakubali nchi inyanyasike kwa mikopo mnayokopa?. Na hayo manyanyaso ni yepi tuyajue, isije kuwa Kuna masharti magumu yanayoingilia uhuru wa Taifa wa kiuchumi, kisiasa, kisheria na hata kitamaduni. Tuweke wazi kwenye hili.

2. Jambo la pili Rais kadai Pale Kariakoo kuna siasa nyingi.
Rais amedai ya kwamba alituma wajumbe wake kwa Siri kule kariakoo na kugundua ya kwamba Kuna wafanyabiashara wengi walikuwa wanafungua maduka au kuingia kwenye mgomo bila ya kujua sababu ya mgomo.

Nimeshangaa kwa kauli hii ya Rais. Maana mwaka Jana wafanyabiashara wa Kariakoo walifanya mgomo na mwisho wanafanya kikao na Waziri Mkuu pamoja na Waziri wa Fedha, na walieleza sababu nyingi Sana za kwanini wanagoma Tena live kwenye vyombo vya habari.

Inakuwaje Tena hao hao wafanyabiashara ndani ya muda mfupi wadai hawajui kwanini wanagoma? Ok, tufanye hawajui wanachogomea, ni kwanini Serikali ilisitisha baadhi ya kanuni kwa muda? Kama vile matumizi ya EFD na Faini ya kutotumia receipt kwa wafanya biashara wa Kariakoo?. Ina maana Rais pamoja na kupata taarifa ya wafanyabiashara kutojua wanagomea nini bado aliendelea na kusimamisha kanuni?.

Naona Kama Rais amejichanganya au anatuchanganya kwenye hili eneo, au yeye ndio analeta siasa kwa kudai wanaogoma hapo kariakoo hawajui sababu kwanini wanagoma na bado serikali ikasimamisha kanuni hapo kariakoo.

Swali langu ni kwamba je wale wafanyabiashara hawakuwa na sababu za kugoma? Na ni kwanini Serikali imeukubali kutii baadhi ya malalamiko ya watu ambao inajua hawajui wanachogomea?.

3. Jambo la tatu, Rais kaingiza mambo ya jinsia kwenye kazi za Serikali
Wakati anamtambulisha Waziri mpya wa viwanda na biashara, Ndugu Suleiman Jaffo, Rais kadai amaemua kumteua Jaffo maana pale kariakoo Kuna mikikimikiki mingi ambayo Dr Ashatu Kijaji asingeiweza kwa sababu ni mwanamke. Nikajiuliza kwanini alimteua kwenye nafasi hiyo Kama alijua kwa mikiki iliyopo kwa Waziri mwanamke hataiweza?.

Rais akaendela kudai ya kwamba ameamua kumteua Dr Ashatu Kijaji kuwa Waziri wa Mazingira na Muungano, ili ashughurikie mambo ya nishati ya gesi ya kupikia. Akadai amemteua yeye pamoja na Naibu Katibu Mkuu mawanamke maalim kwaajili ya kushughulikia gesi ya kupikia. Na akadai kwasababu wao ni wanawake amewateua makusudi na wakishindwa atashangaa wanashindwaje na wao ni wanawake.

Swali langu la msingi ni je Kuna Wizara zinazowafaa wanawake tu? na Kuna Wizara zinazowafaa wanaume tu?. Na Kama zipo ni Wizara zipi hizo?. Na kwanini Rais anazijua na bado amateua jinsia tofauti kwenye Wizara husika?

4. Jambo la nne Rais kadai kuwa Wafanyakazi wa TRA walifanya sherehe Kidata alipohamishwa TRA
Rais kwenye hotuba yake kadai kwamba taarifa za kuhamishiwa zilipofika TRA, wafanyakazi wengi walifurahia Sana na kuamua kufanya sherehe. Kwa maana nyingine Kidata alikuwa very strict kwenye kazi yake lakini bado Rais akamuondoa.

Kwenye muktadha huo huo Rais kadai Kidata hakuoendwa na TRA na pia hakuoendwa na Ikulu maana alikuwa mchapa kazi Sana na amenyooka. Sasa ikamwa najiuliza Kama una Kamishna mkuu wa TRA anayejituma na kusimamia taratibu, inakuwaje unamtoa hapo?. Unadai atakuwa mshauri wako, kwanini awe mshauri wako ilhali alikuwa anasimamia taratibu na anajua kazi?.

Swali langu ni kwamba Kama Kidata alikuwa amenyooka mpaka kuchukiwa na Ikulu pamoja na wengine , inakuwaje Rais kamtoa? Rais anahitaji mtu wa aina gani mwingine?. Kama Kidata hakuwa Mtendaji mzuri kwanini Rais adanganye?.

5. Jambo la mwisho, Rais kamuomba Kamishna Mkuu wa TRA kutoshirikiana na TRA kuiba
Kwenye hili Rais kakosea Sana kuliweka alivyoliweka. Maana kauli yake ni kwamba anathibitisha ya kwamba TRA Kuna wezi. Sasa Kama kiongozi wa nchi unajua Kuna wezi ndani ya TRA kwanini huchukui hatua?. Na kwanini umewaacha wezi qanaendelea kuiba na Wala huwa kamati mpaka unamshauri Kamishna mpya wa TRA asishirikiane na wezi waliopo ndani ya TRA.

Swali langu ni kwamba hawa wezi ndani ya TRA ni akina nani?

By Econonist.
 
Kwanza usipotoshe watu, hakuna waziri aliyetolewa, wamebadilishwa kazi tu.

Usiloloijuwa ni usiku wa kiza, hizo ndiyo ukisikia unaziishi "Reforms" bila kujijuwa.

Nchi nzima imefanya nini?
Wewe dada, sio Mimi niliyesema ni Rais mwenyewe ndio kasema. Kwamba Dr Kijaji hapaawezi pale kariakoo kisa ni mwanamke. Hivyo kaamua kumuweka mwanaume ili apambane na mikikimikiki ya Kariakoo. Wewe hapo huoni Kuna tatizo?

Halafu elewa maana ya kuondolewa na kubadilishwa. Hivi unaweza kubadilishwa nafasi bila kuondolewa?. Dr Kijaji kabadilishiwa Wizara baada ya kuondolewa kwenye Wizara ya mwanzoni.

Halafu ni jibu swali moja, hivi hizo reforms unazozitaja, msingi wake unatokea wapi?. Kwenye sheria, sera, katiba au utashi wa Rais.
 
Kumhamisha tu hiyo, na sabau kazotowa alipokuwa anamuasa Jafo, su hujamsikiliza Rais mama Samia?
Sijakataa kwamba kamuhamishia, ila amemuondoa Wizara ya Biashara na kumhamishia Mazingira na Muungano.
 
Hujatukanwa unaona umetukanwa, je ukitukanwa si utaona umeshushiwa nyundo ya kichwa.

Sasa naona unahaha, mara kahamishwa mara kaondolewa.

Hiyo ndiyo maana ya halisi ya Resilience, Reforms na Rebuilding kama huelewi.

Kwenye tatizo panafanywa kuwa fursa.
Umeniita juha. Juha sio neno la staha kwa mwanamke Kama kulitaja. Ni ushauri tu.
 
Back
Top Bottom