Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

Kimeshajulikana na ndiyo maana anapelekwa Jafo kupiga pasi.

Labda hujamsikiliza vizuri Rais mama Samia.

Kumbuka tu na elewa tu, Kariakoo kuna Reforms na Rebuilding kubwa zinaendelea.
Haya dada nimekuelewa. Ngoja tusubirie hizo reforms hapo kariakoo.
 
Haya dada nimekuelewa. Ngoja tusubirie hizo reforms hapo kariakoo.
Unasubiria? kweli una macho lakini hayaoni, una masikio lakini hayasikii. Hivi huelewi kuwa sasa hivi kariakoo inajengwa upya na soko la zamani sasa lipo asilimia 99? Watu wanawekwa sawa wahamie tu.

Na area nzima ya Kariakoo, kila mahali kuna Rebuilding na reforms za ajabu, haijawahi kutokea, unaishi mkoa gani?

Ikiwa huyaoni yanayoendelea basi hata kusikia husikii? utasubiri sana. Jikumbushe:


View: https://youtu.be/yx2bAloztJU?si=zqOmircmU2qo056L
 
Tatizo lako unaongelea social reforms ambazo zinategema na desturi ya nchi, mambo ya kufokewa ni sehemu ya Mila za kiafrika katika maonyo. Sio Jambo la kuhitaji reforms.

Reforms ninazo ziongelea ni political na economic reforms ambazo mwisho wa siku zinaweza kubadilisha mambo mengi. Reforms sio maneno Bali matendo. Na reform ya kwanza ni Katiba mpya na Sheria. Bila kufanya constitutional reforms hakuna reforms za maana zitakazo kuja.

Ile Rasimu warioba tungeipitia na kukubali Leo Tanzania ingekuwa na reforms sio ngojera za reforms wakati hata Kodi huwezi kukusanya na bado unakopa tu. Kwangu Mimi ni constitutional reforms no reforms
 
Kweli kabisa. Tunataka Rais mwenye vision ya kuipeleka Tanzania mbele, Kama alivyokuwa Magufuli.
 
Nani kakataa. Nimesema ngoja Hilo soko lianze tuone hizo reforms na rebuilding. Ila Mimi naona hizo 4Rs ni za mchongo tu. Rs za ukweli zipo kwenye Rasimu ya Warioba.
 
Nani kakataa. Nimesema ngoja Hilo soko lianze tuone hizo reforms na rebuilding. Ila Mimi naona hizo 4Rs ni za mchongo tu. Rs za ukweli zipo kwenye Rasimu ya Warioba.
Ungoje nini wakati mambo motomoto, unaziishi Reforms, unasikitisha sana kuwa huzioni.
 
Umejitaidi kugeuza geuza hoja zionekane mbaya ila pumba tuh umeandika ,,hoja kama ya rais kujua tra wanaiba asa hilo c kila mtu anajua ulitaka awe mnafki asiseme ?
 
Kwanza usipotoshe watu, hakuna waziri aliyetolewa, wamebadilishwa kazi tu.

Usiloloijuwa ni usiku wa kiza, hizo ndiyo ukisikia unaziishi "Reforms" bila kujijuwa.

Nchi nzima imefanya nini?
Wewe dada, sio Mimi niliyesema ni Rais mwenyewe ndio kasema. Kwamba Dr Kijaji hapaawezi pale kariakoo kisa ni mwanamke. Hivyo kaamua kumuweka mwanaume ili apambane na mikikimikiki ya Kariakoo. Wewe hapo huoni Kuna tatizo?

Halafu elewa maana ya kuondolewa na kubadilishwa. Hivi unaweza kubadilishwa nafasi bila kuondolewa?. Dr Kijaji kabadilishiwa Wizara baada ya kuondolewa kwenye Wizara ya mwanzoni.

Halafu ni jibu swali moja, hivi hizo reforms unazozitaja, msingi wake unatokea wapi?. Kwenye sheria, sera, katiba au utashi wa Rais.
 
Kumhamisha tu hiyo, na sabau kazotowa alipokuwa anamuasa Jafo, su hujamsikiliza Rais mama Samia?
Sijakataa kwamba kamuhamishia, ila amemuondoa Wizara ya Biashara na kumhamishia Mazingira na Muungano.
 
Na wengi maana yake "wote"?

Ukishaelewa jibu, kamsikilize upya Rais mama Samia utaelewa alichokisema.
Wengi ni zaidi ya nusu au nusu ongea mmoja au theluthi mbili.
 
Umeniita juha. Juha sio neno la staha kwa mwanamke Kama kulitaja. Ni ushauri tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…