Mambo matano aliyosema Rais Samia jana yaliyonisikitisha

..Samia amedai Dr.Kijaji ameshindwa majukumu yake ya Uwaziri wa biashara kwasababu ni mwanamke.

..pia amesema moja ya sifa iliyomfanya amteue Dr.Jafo Waziri wa biashara ni kuwa na " mdomo mwingi. "
haaaaaaaaa haaaaaaaaa haaaaa!
 
..pia Samia alisema amemteua Kamishna mpya wa Tra kwasababu anajua vichochoro vya wizi ktk Tra, na huenda hata yeye Kamishna mpya aliwahi kushiriki wizi alipokuwa mtumishi wa Tra huko nyuma.
Aiseeeh! Kwa hivyo Rais hajui vichochoro ila Kamishna ndio anajua vichochoro vyote.
 
..huyu Mama hapaswi kuzungumza chochote tofauti na alichoandikiwa na wasaidizi wake.

..mambo aliyoyaongea jana yanadhihirisha kwamba hana upeo na uelewa wa kuwa ktk nafasi ya Mkuu wa nchi.
Alijivua nguo Jana. Hasa kwenye mikopo ya IMF alionesha kwamba serikali haina plan.
 
Kama ulimsikiliza alisema jana kwamba kidata mpaka baadhi ya watumishi wa ikulu na viongozi wa serikali walikuwa hawampendi itafakari vizuri hyo kauli.
Kweli mkuu. Kuna jambo limejificha.
 
Job Ndugai aombwe TU samahani hadharani. Manake kila siku mnademka na kauli yake kwa style tofauti tofauti, lakini mantiki ni ile ile
Tatizo la ndugai alifanya ujinga mwingi kabla ya kauli yake. Hivyo anaonekana mnafiki tu.
 
Tatizo kubwa la Tanzania ni matumizi ya hela au kodi wanazokusanya. Kuna watu wanakula ruzuku kubwa sana. Na hao watu wanajificha nyuma ya uraia wa Tanzania. Hawa wafanyabiashara wengi wakubwa wenye asili ya Asia wanachota sana ruzuku zetu. Mfanyabiashara au Mwekezaji mzawa hawezi kupewa hizo nafasi kwa sababu wazawa hawatoi gawio kubwa kwa walio kwenye Mamlaka. Wapo wanaomiliki mashamba ya. Mkonge, wanao-agiza mafuta na wanaosambaza mbolea ruzuku wanazokula hawa jamaa aisee. Ukizunguka mitaani na mitandaoni kutwa tunajadili Simba na Hanga. Bongo fleva na Bongo movie . Halafu unakuta mtu ana kiwanda huku amepanga apartment upanga. Ukienda Pakistani,India na U.A.E ana mahekalu utadhani anafanya biashara Marekani. Kusumbuana kote huku ni uhaba wa dola. Mikopo inabidi ulipe kwa Dola .Dola itakaaaje hapa nyumbani wakati Biashara kubwa zinazohitaji dola zinamilikiwa na watu wenye prime interest nje ya Tanzania. Unataka dola iwepo wakati uagizaji wa mafuta, bandari kavu, uagizaji wa mbolea n.k tenda umewapa watu wenye asili ya nje. Kumbuka hizi bishara hazizalishi dola bali zinahitaji dola toka ndani iende nje. Mimi sio mbaguzi ila jamani tujionee huruma kuna bilionea kahamisha familia U.A.E na huyu ndio ana tenda ya kusambaza mbolea nchi nzima na ni mwekezaji wa mkonge. Unadhani faida kubwa anayopata inabaki Tanzania au anaiwekeza nje ?
 
Alijivua nguo Jana. Hasa kwenye mikopo ya IMF alionesha kwamba serikali haina plan.

..hata suala la kusema Dr.Kijaji aliishindwa wizara ya biashara kwa sababu ya jinsia yake ni kauli ya kudhalilisha wanawake. Kumbuka kwamba Ashatu Kijaji ni Daktari wa falsafa, sasa mwanamke aliyeelimika mpaka ngazi hiyo bado ananyanyapaliwa kwa jinsia yake. Bado anaambiwa kuna kitu amepungukiwa ktk kutumikia serikali kwasababu ya jinsia.
 
Hizo tafsiri zako umejitungia kwa ujuha wako tu. Hapo Rais mama Samia Suluhu katumia falsafa ya "mkono wa juu ni bora kuliko mkono wa chini" ambayo wewe huifaham.
Punguza matusi wewe mwanamke usiye na adabu. Kama huna la kusema Kaa kimya. Kuna ujuha zaidi ya kumuhamisha Waziri Wizara kisa ni mwanamke?
 
Mikikimikiki ya Kariakoo imemuondoa mwanamke kwakua haiwezi na kumuweka mwanaume sasa niseme hivi hiyo ni midogo zaidi ya ile iliyopo hapa Nchini Tanzania.
Kwahiyo nishauri hivi kama Nchi tunahitaji mtu anaeweza kumudu mikikimikiki pia [emoji123]

Sent from my SM-G970U using JamiiForums mobile app
 
Kweli mkuu. Kwa kauli yake ya Jana ni kama Hana maamuzi kwenye mambo mengi. Kwa mfano kwenye suala la Kariakoo alikaa kimya ila Jana ndio kaka kuongea huku maamuzi yaliyotolewa yako kinyume na kauli yake.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…