Analyse
JF-Expert Member
- Jan 19, 2014
- 17,637
- 47,413
Bado nipo nafanya ziara huku mikoani. Bado nipo Songea, ila nimeexperience mambo ambayo yamenishangaza.
1. Kupanda gari inabidi huwe na namba ya dereva au kondakta.
-->> Ili sio kosa lao, maana imesababishwa na uhaba wa usafiri. Nilikuwa nataka kufika kijiji kimoja kinaitwa Subira, nilisubiria sana gari hadi nilipopewa taarifa kuwa inabidi niwasiliane na dereva kujua wako wapi.
2. Kushuka toka kwenye daladala, kwenda dukani au nyumbani then wanarudi kuendelea na safari.
-->> Hii ilinishangaza sana. Nipo ndani ya hiace ya Mshangano, tumefika sehemu kuna wamama wakashuka na kuingia kwenye nyumba kama ya 2 toka barabarani. Nikashangaa kuona gari haindoki, namuuliza dereva vipi? Suka nae anamcheki konda "Oya waambie wafanye fasta"
-->> Wamama waliporudi safari ikaendelea. Yani najiuliza eti kule Dar umfanyie hivyo konda wa tandika, manzese au k/koo?
3. Kuomba kupunguziwa nauli kwenye daladala.
-->> Hapa wanaume wa mikoani mliniacha Hoi. Najua nikawaida nauli kupelea. Ila nipo ndani ya gari namsikia konda anamwambia yule jamaa kuwa hiyo hela siwezi kupokea, subiria gari nyingine. Ikabidi nimwambie konda amruhusu jamaa aingie, hela iliyopungua nitaongezea mimi.
-->> Baada ya jamaa kupanda, namuuliza konda, jamaa anashilling ngapi ili nimuongezee? Konda ananiambia jamaa ana Tsh 100 tu. [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
-->> Wanaume wa mikoani kuweni serious basi.