Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa

Duuuh! mkuu,mbona jamaa kaelezea vema tu kuhusu yeye kukosa ajira?
Kuna Rais anaitwa JPM alizuia ajira kwa watu wengi na hii ilianza punde tu alipoingia madarakani,na hiyo inajulikana na almost kila mtu.Nakushangaa,ambavyo unamtilia mashaka graduate wa 2015,kukosa ajira hadi sasa.
Mbona mimi nimeona kasema anamwaka mmoja tangu kawa jobless. Kumbukeni hii ni story moja so hizi epsodes zisiwapoteze mkashindwa kumwelewa rafiki yake BIG. Epsode ya kwanza kabisa kaelezea
 
Mbona mimi nimeona kasema anamwaka mmoja tangu kawa jobless. Kumbukeni hii ni story moja so hizi epsodes zisiwapoteze mkashindwa kumwelewa rafiki yake BIG. Epsode ya kwanza kabisa kaelezea
Shida ni wadau tumekuwa na maswali mengi ya mbele hadi tunampelekea jamaa avuruge mtiririko wa stori yake.


Mimi naamini haya yote angeyafikia tu kwenye stori ila maswali yetu ndo yalimfanya awahi kuelezea ya mbele.


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Shida ni wadau tumekuwa na maswali mengi ya mbele hadi tunampelekea jamaa avuruge mtiririko wa stori yake.


Mimi naamini haya yote angeyafikia tu kwenye stori ila maswali yetu ndo yalimfanya awahi kuelezea ya mbele.


Sent using Jamii Forums mobile app
Watu wanaviherehere sana. Mtu story bado inaendelea wameshaanza midomo yao. Epsode za mbeleni au labda hata ya mwisho ndio wangeelewa zaidi lakini wanajiulizisha maswali ambayo kimsingi ameyatolea utangulizi epsode ya kwanza kabisa
 
Watu wanaviherehere sana. Mtu story bado inaendelea wameshaanza midomo yao. Epsode za mbeleni au labda hata ya mwisho ndio wangeelewa zaidi lakini wanajiulizisha maswali ambayo kimsingi ameyatolea utangulizi epsode ya kwanza kabisa
Kwa kweli
Maswali yetu ndiyo yaliyomfanya avuruge mtiririko wa stori yake.
Na mbaya zaidi tunazidi kumuuliza.

Tutaharibu stori,Kuna vitu tutavikosa
Tungemuacha aflow tu kwa mtiririko alioupanga hadi mwisho.
Naamini maswali yetu yote tunayojiuloza juu yake yote yapo kwenye episodes zake ambazo zinakuja.
 
we jama kupitia andiko lako hili sina shaka hata kidogo na elimu yako...aisee mwenyezi Mungu akukutanishe na watu sahihi watakao kusaidia....

mwenyezi Mungu akupe matumaini usikate tamaa nakuona kwenye taswira ya kiongozi mkubwa sana hapo baadae...!

tukutane kwenye kilele ha mafanikio...!​
 
Watu wanaviherehere sana. Mtu story bado inaendelea wameshaanza midomo yao. Epsode za mbeleni au labda hata ya mwisho ndio wangeelewa zaidi lakini wanajiulizisha maswali ambayo kimsingi ameyatolea utangulizi epsode ya kwanza kabisa
Aya ndio yalipelekea Chizi Maarifa kukatiza story yake mwisho wasiku wakaanza kumtukana
 
Kwenye kukujibu hili swali wacha nitulize na akili yangu kabisa maana hii hoja imekuwa ikileta ukakasai kwa wengi.

Wakati mwingine wafadhili, ikiwa ni serikali au watu binafsi kutoka nchi za Magharibi au wazungu, wanaweza kutoa misaada kwa sababu kadhaa, na kuna mifano mingi ya jinsi wanavyoweza kunufaika au kufuatilia malengo fulani. Hata hivyo, ni muhimu kutambua kuwa HAKUNA msaada ambao ni wa bure eti jamaa wanatupenda sana. isipokuwa KILA MSAADA unakuja na malengo malengo yake kutegemeana na muktadha wake. Mfano misaaada mingi inatolewa kwa sababu zifuatazo:​
  1. Diplomasia ya Maendeleo: Baadhi ya mataifa hutoa misaada kama njia ya kujenga uhusiano mzuri na nchi nyingine. Hii inaweza kuwa njia ya kuimarisha mafungamano ya kidiplomasia na kuimarisha ushawishi wa kimataifa.​
  2. Biashara: Kutoa misaada inaweza kuwa sehemu ya mkakati wa biashara. Kwa mfano, nchi inayotoa misaada inaweza kutarajia kufungua milango kwa biashara zake au kuboresha upatikanaji wa malighafi muhimu.​
  3. Usalama wa Kimataifa: Mataifa yanaweza kutoa misaada kwa lengo la kuhifadhi amani na usalama wa kimataifa. Kusaidia katika kuzuia migogoro na kutoa misaada ya kibinadamu inaweza kuchangia utulivu wa kimataifa. na hivyo wao kunufaika kibiashara.​
  4. Kuongeza Umaskini na utegemezi: Hapa wala usishangae. Baadhi ya misaada hutolewa kwa lengo la kudumaza akili na ubunifu wa wapewa misaada ili kuendelea kuwa tegemezi tofauti na tunavyohubiriwa kwamba misaada inakuboresha hali ya maisha ya watu katika nchi maskini. umasiki wetu unaweza kuwa faida kwao kwani wataendelea kukomba rasilimali zetu kwa kubadilishana na vitu vidogo vidogo sana mfano mavazi, chakula nk.​
Hizo NGO (Shirika Lisilo la Kiserikali) zinapopokea fedha, wanaweza kuzitumia kwa njia mbalimbali kulingana na malengo yao. Mifano ya shughuli wanazoweza kufanya ni pamoja na:​
  1. Maendeleo ya Jamii: Kujenga na kuboresha miundombinu ya jamii kama vile shule, vituo vya afya, na maji safi na huduma za usafi.​
  2. Afya na Lishe: Kutoa huduma za afya, kampeni za chanjo, na programu za lishe kwa jamii zilizoathiriwa.​
  3. Elimu: Kusaidia miradi ya elimu, ikiwa ni pamoja na kutoa vifaa vya kufundishia, ujenzi wa madarasa, na kutoa ufadhili kwa wanafunzi.​
  4. Mazingira: Kushiriki katika miradi ya uhifadhi wa mazingira, kama vile upandaji miti, utunzaji wa ardhi, na kuelimisha jamii kuhusu mabadiliko ya tabianchi.​
Ni muhimu kutambua kwamba wafadhili wanaweza kuwa na malengo mazuri, lakini pia kuna sababu za kimkakati nyuma yake zinazolengwa, ikiwa ni pamoja na maswala ya utegemezi na masuala ya utawala. Kwa hiyo, ni muhimu kuwa na uwazi na ushirikiano katika utoaji na matumizi ya misaada ili kuhakikisha kuwa inaleta matokeo chanya na endelevu na pia nchi masikini zenyewe ziwe na maamuzi ni aina gani ya misaada wanayoitaka. ILA CHA MUHIMU NI NCHI MASIKINI ZENYEWE ZIAMUE KUACHANA NA UTEGEMEZI NA KUTUMIA RASILIMALI ZAO KIKAKMILIFU ILI KUJIKWAMUA.​
Nimepata elimu!
 
EPISODE 10: Get ready for unexpected

Story Interlude…….

Before sijaendelea na stori yangu naomba kusema hili. Kuna baadhi ya watu wananiuliza hapa jukwaani na wengine kunijia PM kutaka kujua kwamba inaonekana niliwahi kupata pesa nyingi kwanini sikufikiria au sifikirii kujiajiri? Najua wapo wengine wengi ambao wanajiuliza hilo swali ila wameamua tu kupita kimya kimya.

Sasa ipo hivi, kwanza kabisa katika watu ambao wanaoamini katika “be employed with a plan B” mimi ni mmoja wao. Siwezi kuzungumzia hapa kuhusu kushika pesa au kutoshika pesa lakini nitazungumzia mtazamo na uzoefu wangu katika hiyo be employed with a plan B. Kipindi nipo ajira tofauti tofauti nilishajaribu sana hizo plan B, kwamba kutengeneza kipato nje ya kazi yangu. Kama nilivoeleza na nitakavyoendelea kuelezea huko mbele kazi zangu kwa asilimia 60 zilikuwa ni za kusafiri safari sana, So fursa niliyoiona kwanza kwa haraka ni kulima kwa kukodisha au kununua mashamba huko vijijini. Naweza kusema nimelimisha sana mazao tofauti tofauti lakini kwakweli kazi ya kulima au kulimisha inataka kwanza usimamizi wa madhubuti sana. Sasa kwangu mimi ilikuwa ngumu sana kwa sababu leo nipo kesho sipo unaacha wasimamizi unaowaamini kule shamba lkn mwisho wa siku hasara tuu.

Lakini pia nilijaribu baadhi ya biashara kwa hapa mjini lakini pia usimamizi ulinigharimu. Kingine nilichogundua asee hakuna mtu anafanikiwa kwa kusomea au kuiga kuwa mfanyabiashara isipokuwa bishara ni inner motive ambayo mtu anakuwa nayo. Labda mtu akose option kabisa ya kuajiriwa ndio anaweza akaforce akawa mfanya biashara mzuri maana hana option.

Ukiwa na inner motive ya kufanya biashara hakuna kitakachokuzuia hata kusafiri kikazi hakuwezi kuwa tatizo sana lakini kwa mimi vingi nilivyojaribu vilikufa au ilikuwa ni loss tuu. Kwahiyo kama wewe umejaaliwa hiyo inner motive na umeajiriwa unaweza kuwa na mafanikio sana kwa sababu kipato unachopata kwenye kuajiriwa kinabust biashara zakko.

Kwahiyo ndugu zangu this is not an excuse lakini tunakumbushana tu binadamu tumeumbwa tofauti sana lakini pia tumelelewa kwenye mazingira tofauti. Nyie wenyewe mashahidi, hata humu ndani kuna nyuzi zinaanzishwa mtu ana milioni 100 lkni hajui afanye biashara gani wakati huo huo kuna watu wana nyuzi humu wanatafuta laki2 mtaji ili waimplement project zao watoboe maisha. Pia Hapa JF nyuzi kibao zimeanzishwa kushangaa hao viongozi wanaotuimbia mahuburi kila siku watu wafikirie kujiajiri na wakati wenyewe wakitumbuliwa hawajiari ila wanatega kunyenyekea teuzi zingine. Hapo utaona kwamba sio kwamba watu hawajui umuhimu wa kuwa na plan B lkini ile inner motive ni tatizo. Ni mtazamo tuu huu jamani. Kwa hiyo wandugu bado natafuta ajira hahahaa

OK, The chill time's interlude done, let's switch it up and get down to business. Nilisema hapo juu expect the unexpected eeh? Yes, ujue kwenye haya maisha sometimes mtu unakuwa unapanga mipango yako na kuwa namategemeo makubwa sana lakini unachokuja kukutana ni kinyume kabisa na matarajio yako. Wewe unapanga hili lakini unapigwa na kitu kizito ambacho huku tarajia kabisa.

Kama nilivodokeza huko juu kwenye maelezo yangu kwamba pale ofsini ukifauru probation unapewa mkataba wa miaka miwili ambao unaweza kurenewkila baada ya miaka miwili kulingana na uhitaji wa ofisi. Mashirika mengi tu haya makubwa yasiyo ya kiserikali wanafanya hivi hata haya international. Na kwa taratibu za pale ofisini ilikuwa ukifauru kurenew mkataba mara mbili yaani ufanye nao kazi kwa miaka minne na kuendelea huwa wanakupa zawadi nzuri tuu ya fedha nadhani ilikuwa ni motivation ya kuwafanya watu wabaki pale kwa muda mrefu japo kutimuana kulikua nje nje kama usipoenda sawa na taratibu za ofisi.

Basi mimi nashukuru Mungu nilipiga mzigo kwa muda wa miaka minne yaani nilifanikiwa kurenew mkataba mara moja. Sasa kuna kipindi nikaona huku kwenye ma NGO ni kama job security inakuwa ndogo sana, maana unaweza mwenyewe ukajidamka asubuhi, ukanyoosha, ukafika job ukakuta barua kutoka kwa HR kwamba kazi basi. Kwahiyo nikaanza kufikiria kutafuta kazi serkalini kwa kuamini kwamba kule kuna pensionable employment yaani ajira ya kudumu. Halafu yale mazingira very hectic ya kazi nikawa naona kama watu wa government wanakula sana shushu basi nikawa nawatamani sana. Maana mtu unakosa hata muda wa kusimamia mambo yako muhimu hata ujenzi unawea ukajikuta kwa sehemu kubwa ubawaacha mafundi wanajenga bila uwepo wako. Basi bhana Kwa kuwa sikuwa na presha basi nikawa natafuta kazi huku sina haraka kihivyo nikawa navizia zile nafasi ambazo naona nazihitaji ndio naaply.

Mungu wa mbinguni asivyo Athumani na wala haishi Kigamboni, ikatokea kwamba miezi miwili kabla ya kurenew mkataba wangu yaani nimalize miaka minne ili kama menejiment wataridhika na mimi basi nindelee nitimize miaka sita nikapata mchongo serikalini tena kwenye hizi idara ambazo zinajiendesha zenyewe mfano wa TRA, TPDC, TCRA, TBS, BRELA etc. Kuna moja hapo ndio nilipata tena ilikuwa ni kitengo cha elimu kwa umma ni shavu ambalo lilikuwa na safari nyingi maana ilikuwa ni kuzunguka mikoani kuelimisha watu maswala yanayohusiana na idara husika. Kwakweli ilikuwa na nafasi nzuri sana ambayo sikujiuliza mara mbili.

Nikaitaarfu menejimenti kwamba sitarenew tena mkataba. Nakumbuka line meneja wangu alisikitika sana maana mimi nilikuwa ni kati ya majembe yake aliyokuwa anayategemea katika kurescue challenged situation. Hapa nimekumbuka ishu moja nakumbuka kuna siku nililala au nilitoka ofsini saa kumi alfajiri kisa kurescue situation.

Ilikuwa hivi, boss kubwa la pale ofsini alienda Canada kweny meeting na donors sasa kwa kuwa ile ofisi yetu ilikuwa ni moja ya shirika linalofanya vizuri basi wakamwalika boss kubwa aende huko kutoa presentation namna gani tuanvofanya kazi mpaka kutoa matokeo makubwa. Sasa boss kubwa yeye alikuwa amejiandaa zile issue strategic zaidi kumbe wale donors walikuwa wanataka vitu ambavyo kwa boss kubwa vilikuwa ni minor sana nap engine vingempa shida kuvijibia kikamilifu labda kama angesoma maripoti ya miaka ya nyuma.

Sasa alipomaliza presentation yake inaonekana nwakamshooti maswali ambayo yalihitaji zaidi mtu anaeenda sana field ili kutoa majibu ya uhakika. Bosikubwa akamcheki line meneja kama vipi amwandalie baadhi ya majibu. Sasa muda huo ilikuwa ni muda wa kama saa moja ousiku watu ndio tunajiandaa kutoka ofsini na wengine wameshaondoka. Nadhani kwa kule Canada ilikuwa ndio asubuhi watu ndio wanaaza majukumu yao ya kikazi. Mara line manager akanipa simu niongee na bosskubwa jamaa akanielekeza pale ishu anazozitaka nimwandalie then nimtumie kwa email. Mimi nikamtumia fasta nikawa naondoka. Wakati nimshafika nje ya ofisi mara naona bosskubwa ananipigia wasapu kupokea ananiomba nimtafutie tena baadi ya taarifa. Nikalaani sana kwanini nilikuwa hewani wasapu hahaaa ila nikageuza sikuwa na jinsi. Sasa ile nitumie taarifa hii mara ile ikawa haiishi uzuri zile data mimi nilikuwa nazo. Basi nikamwambia bosskubwa kama vipi waniunge mimi kwa skype nikiwa pale ofsini ili tusaidie kuwajibu. Boss kubwa akaniuliza kama nina uhakika sita mwangusha, nikamwambia kwani hizo info si ndio mimi ambazo ninampatia, lakini nikashindwa tu kumwambia mbona wewe unajikanyaga kanyaga tuu huko hahaha. (Jokes, ofcourse I respect the na amekuwa role model wangu sana na alishalamba uteuzi serikalini mda mrefu tuu) kwenye ministerial level)

Basi akanicoonect pale yale majamaa meupe yakaanza kunishoot maswali pale nikawa nawajibu, wakawa wanataka kueleshwa kwa undani sana maana walikuwa ni wawakilishi wa wafadhili ambao ilikuwa walete mpunga mrafu sana ofisini. Basi pale nikajikuta naenda nao mpaka session yote aliyopangiwa bosskubwa ni kama bosskubwa alitumia akili kuwaambia kuwa kuna ofisa alimwandaa kutoka Tanzania (yaani mimi eti) kushiriki ule mkutano kwani alitaka kuonyesha pale ofsini tunacollective working style, basi ile pia ilimpa crediti sana. Basi mimi nikajikuta natoka pale saa nane yaani kama inaenda inaenda saa kumi. Uzuri ile ofisi ilikuwa karibu na breakpoint pale posta basi mda wa wao wakibreak kula mimi naingizia zangu breakpint nagonga msosi. Basi mwisho bosskubwa akanipa likizo ya sikumbili nipumzike kufidia ile kazi ya kutoboza usiku.

Basi wakati naaga menejiment wakanishawishi sana nibaki lakini ikashindikana na nikawapa sababu naenda serikalini basi ikabidi tuu waelewe na kunitakia kila lenye heri. Kwakuwa nilimaliza miaka mine pale basi nikapewa mshiko wangu wa pongezi na wiki ya mwisho wakandaa farewell cake tukatata pale ofisi nzima then nikamalizia vimeo vyangu kisha nikakabidhi ofisi nikaondoka kuanza majukumu mapaya.

Sasa kule serikalini baada ya kupokea offer letter kilichobaki ni kusaini tu mkataba. Kwa kuwa tulikuwa watu kama 10 hivi tuliopata ajira pale kwenye hiyo position ilibidi tusubiriane ili wote tuanze siku moja. Kwa hiyo mimi tangu nilipoacha kazi nilikuwa na kama mwezi mmoja hivi wa kupumzika ndio nikaanze kazi serikalini. Niliona afadhali na nilifurahi kupata hilo gap kwa sababu huo muda niliutumia kupumzika na familia nyumbani kwa sababu kipindi hicho ndio kwanza nilikuwa nimetoka kuoa na nina katoto ka kwanza. Basi maisha yakawa poa tuu huku nikiendelea kusikilizie muda ufike nikaanze mzigo serikalini.

Sasa kipindi kile ilikuwa ndio kipindi Magufuli ameingia ofisini, nadhani wote mnakumbuka speed aliyoingia nayo madarakani. Advertise ya kwanza Mkurugenzi wa ile idara ambayo nilipata kazi akatumbuliwa. Hiyo haikuwa big ishu kwangu sana maana ilikuwa hainiathiri moja kwa moja. Advertise ya pili mzee baba akastopisha ajira zote mpya serikalini until further directives. Hapo ndo nilipopigwa na kitu kizito, askwambie mtu ile taarifa uliifurahia au kuona ya kawaida kama tu ilikuwa haikugusi moja kwa moja ila kwa sisi ambao ilitugusa asee!!!

Sasa nikajipa moyo sisi tayari tunaofa letter so itakuwa haituhusu. Nikatamani kuwapigia wengine ambaop nao walikuwa wamepata iyo kazi lakini binafsi nikawa siwajui kwani nilisikia tu pale idarani wanasema nitakuwa na wenzangu wengine kama 10 hivyo tunasubiriana ili tuanze wote pamoja. Basi nikatimba pale idarani kwenda kuulizia mstakabalim utakuweje. Niliulizwa tuu umekuja na ile barua ya ofa? Nikajibu ndio, wakaniambia iache hapo kwa sekretari mpaka utakapopewa taarifa nyingine kwa muda ule maelekezo yalikwa ndio hayo. Daa pale pale nihisi nguvu zinaniishia lkn nikajikaza basi nikaiacha ile barua pale kwa secretary lakini nikaitoa kopi, na nikamuomba namba yule sekretari ili niwe nafatilia. Katika kipindi ambacho nilikuwa nafatilia taarifa ya nabari basi ni kipindi kile maana nilikuwa nataka kujua mzee baba ataruhusu lini kuendelea na michakato ya ajira pale ilipoishia.

Hahaaa ni kama ilikuwa kusubiria mawe yanayochemshwa eti yataiva, mzee baba alikaza. Nilikuwa nampigia simu yule sekretari wa pale serikalini kufatilia maendeleo nadhani mpaka alinichoka maana kuna siku akaniambia kaka sasa naona tu nikutafutie namba ya katibu wa ikulu ili uwe unampigia mwenyewe moja kwa moja. Dah nikaona hapa nishachokwa sasa, lakini nikasema hata kama ningekuwa mimi ningefanyaje. Kwakweli Nilikuwa frustrategy sana kipindi hiki ila sikujilaumu kuacha kazi kule nilikokuwepo maana sikukurupuka ni vile mipango imekwenda ndivyo sivyo. Basi ikabidi nikubaliane na hali halisi. Siku moja line manager akanipigia simu kuniuliza kama lile sekeseke limenikuta na mimi nikamweleza pale na mimi miongoni mwao akaishia tu kuniambia yaani mwezi uliofata tu baada ya mimi kuondoka walikuwa wameshapata mtu mwingine. Nilichomwambia tu asjali ila nitamweka awe referee wangu kwenye CV yangu maana niko mbioni sasa kutafuta sehemu ningine.

Hivi ndivyo ilivyokuwa na msala wangu wa kuhamia serikalini. Hapo nilijifunza kitu kikubwa sana wakati mungine sio kila plan unayoitegemea inakuja kama ilivyo, therefore, you better get ready for the unexpeceted outcomes. Ila badae nikaja kumwelewa na nikamkubali sana Rais Magufuli, ilikuwa ni nadra sana kutomfatilia hotuba zake kwenye vyombo vya habari labda niwe sina nafasi.

See you to the next episode tuone ilikuwaje. Thank you.
Pole sanaa mkuu!! Daaaa...very painful
 
Ume nikumbusha mbali mkuuu mambo za meza kupinduka, kazi tuliwahi pata taasisi Fulani ya serikali tulingia Kwa maelekezo project ilikuwa kama pailot tukaona tume tusua aseeee tukapewa mikataba baada ya muda watu walimtisha boss juu ya hiyo project kumbe walikuwa wameandaa watu wao ,boss akazama king tukala za uso mkataba ukasitishwa wajuba tukakaa benchi shushu ilikuwa tamu sana.
Polen sanaaa
 
EPISODE 11: Nilijifunza kuacha kuwahurumia kabisa watu wenye ulemavu

Hii experience najua itawashangaza wengi au labda watu kutokunielewa kabisa. Kabla ya kujifunza kwamba sipaswi kabisa kuwahurumia watu wenye ulemavu namimi pia nilikuwa ni mmoja wa watu katika kundi ambalo nawaonea huruma sana watu wenye ulemavu.

Kikawaida nilikuwa nikiona au nikikutana na mtu mwenye ulemavu wowote kama vile wasioona, wanaotambaa, wenye magongo, viziwi au hata albino nilikuwa nawahurumia sana Nilikuwa nafikiria ni watu wenye shida sana na wanahitaji kuhurumiwa na kupewa misaada hivyo nilikuwa najitoa sana hasa hasa kwa wale ombaomba wa barabarani. Nakumbuka kuna omba omba alikuwa anatega kituo ambacho mimi ndio ilikuwa nashukia au napita kwenda na kurudi kwenye mihangaiko yangu, yule jamaa alikuwa anatembelea mikono (ni kama anatambaa vile) basi nilikuwa mara kwa mara namsapoti na kiasi kidogo cha pesa mpaka akanizoea yule mlemavu.

Yaani ilikuwa hawa omba omba wa wenye ulemavu mitaani hususani wanawake nilikuwa mara nyingi sana nawapa vijisenti kidogo maana nilikuwa nawahurumia sana. Hali hii iliendelea kunitawala sana na ilifikia hatua kama nikipata nafasi ya kuongea na mtu mwenye ulemavu basi ilikuwa ni yale maongezi ya kumpa moyo yaliyotawaliwa na majonzi. Yaani niliona hawa walemavu ni kama vile wanahitaji kufarijiwa kila mara na kama Mungu anawatumia kutukumbusha wengine ukuu wake.

Sasa bhana baada ya kuona kule serikalini hakuna tena dalili ya kurejeshwa job (maana niliachishwa kazi kabla sijaanza kuifanya hahaha) nikajikita kwenye kutafuta mchongo mwingine ili maisha yasije kunipiga mjini hapa. Huku na huku nifanikiwa kupata kazi kwenye shirika moja ambalo lenyewe lilikuwa linadili na maswala ya kuwainua watu wenye ulemavu na mambo mengine yanayohusiana na haki zao.

Pale niliajiriwa kama Program advocacy coordinator hivo ilikuwa ni managerial position ambacho kwenye idara yangu nilikuwa na staff kama wanne hivi ambao walikuwa wanareport kwangu direct, na pia nilikuwa naingia kwenye vikao vya menejimenti, hapa nilipanda ngazi katika career yangu. Sasa kwenye organization unadili moja kwa moja na watu wenye ulemavu ambapo wengi tulikuwa nao pale ofsini kama staff wenzangu nawengine walikuwa ni wanufaika wa program mbali mbali za pale ofsini.

Kama ilivyokawaida kazi zangu pia zilikuwa zinahusisha sana safari za mikoani katika kutimiza majukumu mbaalimbali ya program za pale ofisini. Basi ilikuwa katika zangu watu ambao na-engage naokwa asilimia kubwa walikuwa ni wenye ulemavu. Ilikuwa nikienda mikoani nakutana na walemavu, nikifanya seminars workshops basin i walemavu, nikialikwa kwenye mikutano basin i walemavu yaani ilikuwa ni walemavu walemavu kila kitu.

Sasa baada kufanya kazi na watu wenye ulemavu tena wa aina tofautitofauti kwa muda mrefu na mimi nikaaza kuwafahamu tabia zao kwa undani, lakini pia niliweza kujifunza mambo mengi sana yanayohusiana na watu wenye ulemavu. Niliweza kuzielewa hisia zao, mitazamo yao, mahitaji yao na mikakati mbali mbali ambao walikuwa nayo kibinafsi, kisera au kiprogamu yenye lengo la kutetea haki zao na kuwainua kujikwamua na hali ngumu za maisha.

Kwanza kabisa nikaja kugundua kumbe hawa jamaa ni binadamu kama binadamu wengine despite their disabilities. Kwamba mapungufu yao ya kimwili au kiakili hayawafanyi wasiwe na hisia, matamanio au mipango katika maisha yao ya kila kitu. Kikubwa sana katika hilo nikaja kuelewa kwamba watu wenye ulemavu hawataki kabisa kuonewa huruma. Yaani vile nilivyokuwa nikiwachukulia kama watu wenye kuonewa huruma na kuongea nao kwa lugha flani hivi ya kuwasikitia hicho wenyewe walikuwa hawaki kabisa.

Nakumbuka wakati naanza kufanya kazi pale ilikuwa kila kitu nafanya kwa kuwapendelea watu wenye ulemavu. Mathalani kwenye mikutano kwa kuwa mimi ndio nilikuwa organizer na facilitator mkuu basi nikatoa maagizo labda waaanze kwanza kula watu wenye ulemavu, au naweza agiza malipo waanza kulipwa wenye ulemavu, ukiniuliza sababu nakuwa sababu yenye mashiko isipokuwa ni kasumba tuu ya kuona kama wanahitaji zaidi sympathetic treatment. Nakumbuka wengi wao walikuwa hawapendi hizi privilege nilizokuwa nawapa. Nakumbuka kuna siku jamaa wawili wenye ulemavu waliniita chemba na kunichana live kwamba nakosea sana ninavyowapa upendelea wa wazi mambo mengine ambayo hayana athari moja kwa moja napaswa kuwachukulia kwa usawa na watu wengine ambao hawana ulemavu.

Nilishangaa sana inakuwaje mimi nawapa upendeleo halafu wao wanakataa? Basi ikabidi nianze kuwasoma sasa kwa ukaribu zaidi. Nikaja kugundua yafuatayo:

kwanza, Watu wenye ulemavu hawataki kuonewa huruma pasipo sababu za msingi. Kwamba wanataka kama hakuna umuhimu na sababu yoyote ya maana basi wewe wachukulie ni kama watu wengine tuu na sio kama kundi spesho. Mimi nimesafiri nao sana, nimeenda nao sana maeneo ya mitoko na kupitia hayo n imejua tabia zao nyingi sana. Wanapenda kubishana mpira, wanajichanganya kwenye starehe, wanapenda kuabudu na kufanya kazi. Hiyo ni mifano michache tuu niliyoianisha.

Nakumbuka kwenye moja ya safari zangu nilisafiri na jamaa mmoja ambaye yeye alikuwa hana miguu kabisa. Sasa kwenye hizi safari ujue mnakuwa na mda mwingi wa kufanya mambo mengi pamoja kwenye tripp kama vile kula nk. Sasa yule jamaa nikaja gundua ni mtu wa kupenda sana kutoka usiku kwenda kwenye viwanja vya starehe. Sasa siku moja nikasema ngoja nitoke na mshikaji nikampe kampani. Basi tumefanya mambo yetu pale mara jamaa akaopoa demu mmoja mkare sana. Yule manzi alikuwa pisi kwelikweli na jamaa aliondoka naye. Asubuhi nikawa namtania namtani kaka ile pisi hata mimi niliielewa jamaa akacheka sana akaniambia zile ndio pigo zake na anazo nyingi tuu na nikisema tushindane Taidume huwezi kuwin. Ila nilichokuja kugundua jamaa alikuwa ni muhongaji mzuri sana dadeki.

Pili, Watu wenye ulemavu wanakereka sana kuona wenye ulemavu wengine wanavyoomba omba mitaani kwani wanadai wanawadhalilisha. Pale ofsini kulikuwa na program ambazo zilikuwa zinawakutanisha walemavu wanaoomba omba mitaani ambazo zilikuwa zinakuwa na lengo la kuwekana sawa na kupeana mikakati ya kujiinua. Kwenye vile vikao nilikuwa naingia na wale omba omba walikuwa wanatoa shuhuda kwamba wanapata pesa nyingi sana. Akikupigia hesabu sometimes kiwango cha chini mtu anaondoka hata 50k kwa siku. Sasa wakawa wanapeana makavu wenyewe kwa wenyewe kwamba kama mtu umeomba omba kwa mwaka mmoja tu si unakuwa na pesa za kutosha na hata kuwa na uwezo wa kuanzisha biashara ya heshima tuu. Hapo nikaja gundua kwamba wale omba omba wa mitaani wengi wao ile wameishaifanya ni ajira na hawawezi kuacha.

Hii ikanifanya nikumbuke siku moja kipindi cha nyuma wakati nipo nafanya kazi kwenye lile shirika la kugawa ruzuku, nilipita pale Rombo green view shekilango kula ilikuwa ni kama saa saba hivi mchana. Basi wakati nasubiri msosi pale liliingia kundi la omba omba wasioona kama nane wakiwa na wale watoto wanaowaongoza. Basi mimi kwenye akili yangu nikawa nawaza pale leo tumevamiwa ila nikawa nimetenga buku wakipita mezani kwangu pale niwape. Gafla nikaona kuna meza ni kama zilikuwa reserved wakaenda wale ombaomba kukaa na vitoto vyao. Haikuchuka hata dakika 10 nikaona misosi ya maana ya inapekwa kwenye zile meza zao nikama wametoa oda na ndivyo ilivyokuwa. Maana nilipoletewa msosi wangu nilimuuliza yule muhudumu mbona wale ombaomba wameletewa chakula haraka je mnawasaidia kuwapa na misosi. Akanijibu kwamba wale ni wateja wao wakubwa na huwa wanakulaga pale lunch. Nikashangaa sana pale na bei za misosi rombo ya kipindi kile zilikuwa zimesimama. Kwa wale ombaomba sikutegemea kama wangemudu kula pale.

Tatu, Watu wenye ulemavu hawahitaji kuhurumiwa bali kutengenezewa mazingira mazuri yatakayowafanya waweza kujumuika pamoja na raia wengine katika shughuli mbalimbali. Nilikuja kugundua watu wenye ulemavu ni very potential. Wapo wenye vipaji na vipawa vikubwa katika field mbali mbali lakini wengi vipawa vyao wanashindwa kuvionesha na kuwanuifa kwa sababu tuu wengi wetu tumeishia tuu kwenye kuwaonea huruma badala ya kuwatengenezea mazingira wezeshi ili waweze kuonesha uwezo wao. Tena kwenye hili nina idea nzuri sana ya tv program yenye kuhusisha watu wenye ulemavu, ambayo nina uhakika itabamba sana. So kama kuna wadau wa hizo connection tuwasiliane nishee hiyo idea na kama wana uwezo wakaifanyie kazi, mimi sitaki hata kumi hapo – nipo siriasi.

Amini ama usiamini kwamba mazingira wezeshi (accessibility) plays a crucial role in empowering people with disabilities to showcase their talents and contribute to economic empowerment. By removing barriers and creating an inclusive environment, society can tap into the diverse skills and abilities of individuals with disabilities. Kwa kutowekeza katika mazingira wezshi tuapote viongozi wazuri, tunapoteza wafanyabiashara wakubwa, tunapoteza wasanii mahiri kabisa, tunapoteza wasomi wabobevu kisa tu wamezaliwa na ulemavu au kupata ulemavu katika hatua za ukuaji. Sio fair kabisa

Kwahiyo katika maana hiyo nikaachana kabisa na tabia ya kuwaonea huruma watu wenye ulemavu na badala nikajikita kushiriki kikamilifu kutengeneza mazingira ili kuwawezesha kwa nafasi nilizokuwa nazo. Mfano sasa hivi kuna wale watu wanaowatumia watoto wenye ulemavu kuomba omba mitaani. Asee siku hizi nakuwa mkali sana kwanini yule mtoto asikazaniwe kupelekwa shule instead ya kuzungushwa kwenye jua muda wa kusoma. Nimekuwa nikiwakkaripia wengi sana kuachana na tabia hizo na mara nyingi sitoi pesa ila naweza nikamnunulia chakula.

Nakumbuka hata yule mlemavu aliyekuwa anaomba omba pale kituo cha daladala mtaani kwangu kuna siku moja nikaongea nae na kumshauri kwavile lile eneo analokaa pale kituoni kumechangamka sana nikamwambia aanzish biashara yoyote. Akadai nimpe mtaji, nikamchana live kwamba nikimpa mtaji mimi au mtu mwingine hawezi kuwa na uchungu na biashar. Nikamwambia wewe anzisha biashara yoyote hata kuuza pipi mimi nitakuwa mmoja wa wateja wako na nitakuletea wateja. Ikawa kila nikipita namkomalia ishu ya biashara. Kuna kipindi nikawa nimesfairi kama wiki hivi. Nilivyorudi nikakuta ameanzisha biashara ya kuuza maji ya kandoro anauzia kwenye ndoo. Huwezi amini alipata wateja wengi sana hususani madereva na makonda wa daladala. Hapo usiniulize kama nilikuwa nanunua ama sinunui ila nakumbuka nilimfanyia mpango nikamuunganisha na jamaa yangu mmoja alikuwa anafanya kazi tigo wakampa mwamvuli na benchi. Nilihama ile mitaa lakini naamini aliiendeleza na kukuza biashara yake.

Kabla sijamaliza hii episode ngoja niwapeni shule ndogo. Tunatakiwa sana kuheshimu utu wa mtu mwenye ulemavu. Watu wengi sana wanawadhalilisha watu wenye ulemavu bila kujua kupitia au kutokana na majina tunayowaita mitaani kila siku. Ni kawaida sana kusikia mtu akimwita mtu mwenye ulemavu kipofu, kiwete, kilema, asiyesikia, zeruzeru nk. Ndugu zangu haya ni baadhi tuu ya majina yanayotweza utu wa mtu mwenye ulemavu.​
  • Usahihi upo hivi, kwanza unapotaka kutaja majina ya walemavu anzia na neno “mtu” au “watu”.​
  • Mfano,​
  • Mtu asiyeona badala ya kipofu. Ukiita kipofu wenyewe hawataki watakupiga na zile fimbo zao.​
  • Mtu mwenye ulemavu wa viungo/miguu badala ya kiwete. Ukiita kiwete wenyewe wanakuwa wakali kweli kweli.​
  • Mtu kiziwi badala ya asiyesikia. Ukiita asiyesikia wanasema wao sio watukutu maana mitoto mitukutu ndio huwa haisikii.​
  • Mtu mwenye ualbino badala ya zeruzeru.​
  • Mtu mwenye ulemavu badala ya kilema/vilema.​
Nadhani nimetoa shule kidogo hapo. See you next episode hakutakuwa na arosto jamani.​

Muendelezo soma Mambo muhimu niliyojifunza katika maisha yangu ya kuajiriwa
 
Back
Top Bottom