Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Mkuu TAI DUME story yako ni nzuri sana na imejaa mafundisho kwa watu wa aina mbalimbali. Ila nakushauri kwamba ongea yote ila usisahau kipengele cha kula tunda kimasihara, ni kipengele muhimu sana kwa story zinazobamba hapa Jf. Ongelea hata mahusiano ya boss na PS au unda story ya aina hiyo wewe na demu wako wa kitaa au wateja wenu hapo kazini ilimradi kisikosekane tu.EPISODE 3: I learnt how to be proactive and beliving in myself in handling difficult situations.
Kwakweli nimeshindwa kupata Kiswahili fasaha cha heading hapo juu ila kuna situation unaweza kutana nazo katika mazingira ya kazi yakapelekea either uwepo wako uonekane una positive impact au ni mzigo tu. Hayo mimi yalinikuta nikiwa na mwezi mmoja tu pale ofsini chini ya Dr KJ the boss.
Nakumbuka ilikuwa ni tarehe za wafanyakazi wa pale ofsini kulipwa mishahara na mimi nilikuwa almost nakaribia mwezi pale ofsini. Boss alikuwa na utaratibu wa kwenda nao benki wafanyakazi wote na baada ya kutoa cash kila mtu alipewa chake then tunatawanyika, sikukuta mtindo wa kuwekewa pesa benki. Yaani wote mnaenda benki, mnapewa chenu kisha mnasepa na maranyingi mshahara alikuwa anaotoa tar 23. Siku hiyo ilikuwa Alhamis.
Mpaka tarehe ya mshara inafika mimi sijui nitalipwa kiasi gani. Nikasema leo ngoja nione basi tukafika mpaka benki then kila mtu akapewa bahasha yake. Kile kibahasha nilipokikadiria kilikuwa na uzito sawa tuu na alichopewa yule PS, cha mhasbu kilikuwa kimejaa zaidi ya wote pale huku yule dereva akiburuza mkia. Nikatia kibunda change mfukoni nikatawanyika mpaka magetoni. Kufika home cha kwanza ilikuwa ni kuhesabu ile cash aisee kiukweli haikuwa haba japo haikufika six digits. Kujiridhisha nikampigia Mhasibu nikavunga kutaka kujua kama hapo makato ya serikali na NSSF yamekatwa, akaniambia kaka Taidume kwa sasa wewe chukua tu hiyo pesa usiwaze. Nikataka kujua kama iyo ni salalry au posho akaniambia kwa mimi ile ni posho maana sijaingizwa kwenye mfumo wa salary mpaka nitakapomaliza probation. Nikaona afadhali kumbe kuna uwezekano kasalali kakawa hata six figures.
Ijumaa wakati naendelea na majukumu yangu kama kawaida mara boss akaniita na akaniambia anategemea kusafiri hivyo kwa siku tatu kwenda Arusha kwa mambo yake hivyo akanipa majukumu mawili matatu niyasimamie wakati yeye hayupo. Pia akania next week pale ofisini tutapata ugeni (one among the key and prominent donor wa project za pale ofsini) kutoka Ulaya. Hao wageni wanakuja kufanya evaluation nna kuangalia namna funding zao zilivyofanya kazi na wangetembelea baadhi ya field areas ili kucollect achievement stories. So akanitaka niandae walau sehemu tatu za vijijini huko tunakofanya miradi na kuwataarifu beneficiaries ili maandalizi yaanze. Yeye alisema atawahi kurudi kwamba angeondoka Kesho yake Jumamos, Jumatatu angerudi by Jumanne angekuwa Ofsini. Ratiba ya wageni ilionesha wangekuja kufanya evaluation yao Alhamis ya wiki inayofata na Ijumaa na Jumamosi ni kwenda Field. Tukakubaliana hivyo.
Kumbe bhana bosi alikuwa anaenda zake zake Samunge kwenye kikombe cha babu nae ni mmoja walioamini kombe la upako la babu lingeweza kutibu maradhi yake. Hili nilifahamu kupitia PS kwani aliniambia ofisini kwa wengine ofisini ameaga jumatatu atampelekea mtoto wake hospitali lkn ni anamsindikiza boss kunywa kikombe cha babu. Nikamtania tu naona PS unafanya kazi yako vizuri sana basi tukacheka pale tukaagana. Kumbuka boss japo alikuwa anakuja kazini lakini kiukweli afya yake ilikuwa dhoofu sana na most of his responsibilities nilikuwa nazicover mm.
Jumatatu mimi niliendelea na majukumu yangu kikubwa ilikuwa ni maandalizi ya wageni na siku hiyo ofisini nilikuwa peke baada ya dereva, boss na PS wake kusafiri yule Muhasibu naye alitengeneza excuses anazozijua yeye mwenyewe so hakuja. Jumanne mpaka mchana boss na PS wake hawajafika ofisini, nikasema jioni nikitoka nitamcall dereva nijue wamerudi au lah. Kupiga namba ya dereva haipatikani, nikajaribu tena na tena ikawa hola. Nikajaribu kumpigie PS nae hapatikani vivo hivo kwa boss, wote hawapatikani. Mpaka naingia ofsini Jumatano hakuna anayepatikana. Yule Mhasibu alikuwa hana interest nao kwakweli kwa hiyo mpaka mimi nilipomwambia hawapatikani wote siku ya pili leo ndio na yeye kuanza kuwatafuta. Ikawa hawapatikani.
Tukajiuliza wamekumbwa na masaibu gani, ila sasa kipindi kile kule Samunge kulikuwa na foleni kubwa sana na kama mankumbuka mafuriko yale ya foleni ilipelekea watu kukwama njiani hata wiki na hakukua na mawasiliano ya simu, ndio hata mawaziri wengi akiwemo waziri wa ujenzi kipindi kile (RIP Mwamba) walitumia chopa. Basi maboss zangu nao walikuwa trapped on the same situation. Wamekwama njiani foleni haiendi wala hairudi, simu hakuna mawasiliano na walikuwa sehemu ambayo hata huduma za msingi kama chakula, malazi na maji ilikuwa shida. Yule dada mhasibu hakujua kama wameenda Samunge na mimi sikutaka kumwambia kwani wenyewe hawakuaga hivyo.
Sasa mimi tension yangu ilikuwa kwa donors ambao wanakuja maana kwenye ile ofisi boss KJ alikuwa ndio kila kitu kwenye kutoa updates na mm nilikuta wale donors fund zao zimeoperate karibia miaka miwili na nusu so wamekuja kufanya kitu kinaitwa midterm project evaluation. Nikawaza nikasema hapa lazima nifanye kitu ili kuokoa jahazi na pengine inakuwa kuwa ndio best opportunity for me to show my problem solving skills in difficult and challenging sitauations.
Basi nikamuuliza mhasibu kama ana access ya email ya boss ili tuone kama kuna updates zozote kutoka kwa wale wageni. Maana hiyo ilikuwa ni Jumatano asubuhi na kesho asubuhi ndio watakuwepo ofsini, maana pia walitegemewa kupokelewa eapoti na gari la ofisi. Dada mhasibu akajibu hana access na email ya boss, huku na huku nikamwambia kwani yeye kama muhasibu si ameshawahi kuwasiliana na watu wafinance upande wa Donor hususani maswala ya financial repors au updates. Akajibu anakumbuka amewahi kuwasiliana nao so tukatafuta hiyo email tukaipata.
Ikabidi mimi niconstruct email ya kumuomba emails za watu wanaotoka Ulaya kuja Tanzania kwa ajili ya evaluation. Hiyo ilikuwa kama saa sita mchana. Bahati nzuri yule jamaa wa finance naye alikuwa ni sehemu ya wanokuja kufanya evaluation na muda huo walikuwa wameshawasii Tanzania maana waliingia alfajiri sana ya Jumatano hiyo hiyo na muda huo walikuwa wamehsafika hotelini kwa kukodi tax. Basi nikampa namba yangu ya simu kwenye email na baada ya muda akanipigia mdada mzungu ambaye ndie alikuwa team leader wao. Kiufupi walikuwa wanatuma emails kwa boss tangu Jumatatu na walikuwa hawapati response yoyote. Kuna vitu walivyokuwa wanavitaka na hasa logistics za hapa Tanzania watafika hotel, ofsini nk ila walipoona kimya wakajiongeza wakafanikiwa kufika hotel ila hawakujua kesho wanakuja vipi pale ofisini. Basi nikamuomba anifoadie hizo email corresponses ili niendelee kuzifanyia kazi.
Mimi ikabidi nijiongeze nikawaomba samahani kuubwa sana na kuwaongopea kwamba boss alipata msiba kijijini kwao na aliondoka weekend kwa matarajio kwamba angerudi Jumatatu. Nikawapa pale blabla za unajua vijiji vya Tanzania hakuna mawasiliano ya simu na ni mbali kwelikweli. Hivyo kwa dharura hiyo I will be taking a lead. Uzuri wakaelewa wao wanachotaka ni updates za kazi sio kumkuta nani ofsini. Tukaagana kwa makubaliano kwamba ratiba ina baki ile ile no mabadiliko.
Sasa tukaanza kuumiza kichwa na mhasibu pale, ubaya kwamba yule muhasibu alikuwa hajui chochote kuhusu implementation za project ile sijajua kwa nini wakati yeye ndio alikuwa anaahold program budget. Nilichomwambia ni kwamba anipe financial report ya ile program ambapo angalau nikaweza kujua kipi kimefanyika so far kwa maana activity gani pesa ilitoka. Lakini pia ikabidi niingie kwenye mafaili kuanza kutafuta reports mbali mbali nilifanikiwa kupata in details kipi kimefanyiak. Nikajisemea mbona hawa nitawamudu tu at zile key points ninazo. Kingine nikamwomba mhasibu ampigie mama mmoja hivi ambae alikuwa ni member wa bodi nilimfahamu kwa sababu alikuwa amewahi kuja pale ofsini kama mara mbili hivi na niliona boss alimpa kazi ya kweda kupresent kwenye mkuta kwa niaba yake, niliona huyu anaweza kutujoin na kuongeza nguvu. Alipopigiwa nilimpa situation yetu akasema atakuja na mzee mwingine memba wa bodi pia ambae nae ni wa siku nyingi na anaijua miradi ya pale. Mpaka hapo nikaona hii ngoma tunaenda kotoboa.
Kwa kule field ikabidi niwapange wale trainees wangu wa Kilindi na Handeni ili wajiandae maana nao kama beneficiaries wanakuwa na sehemu yao. Niliamua kuwapeleka Kilindi na Handeni kwa sababu nilishiriki ile activity na ingekuwa rahisi kwangu kutoa majibu ya kuridhisha. Sasa ngoma ikawa fedha maana tunatoaje fedha bila approval ya boss na yule mhasibu alikuwa strict sana kwenye hizo taratibu. Maana wale wageni ilipaswa kukodi noa ya kutupeleka na kuturudisha dar lkn pia logistics za hapa mjini kwa wageni. Ikabidi nimpigie yule mama member wa bodi ambaye pia alikuwa ni signatory akakubali fedha itolewe ya kufacilitate hilo maana hao ndio wanaoleta pesa sasa kushindwa kuwapeleka site italeta picha mbaya, kwanza boss hayupo si itaonekana tunawakwepa? Mwisho wa siku mzigo ukatolewa wa kutosha.
Basi Alhamisi yake wageni nikawatumia usafiri wakafatwa na kuletwa ofisini, nashukuru Mungu kikao nilikiongoza vizuri na kilienda vizuri sana. Wale board members walisaidia kutoa ufafanuzi to rescue the situation. Then kesho yake tukaondoka nikiwa kiongozi wa msafara, pamoja na member wa board mmoja, muhasibu pamoja na wageni wetu wanne kwenda field. Kiufupi wale wageni walifurahi sana. Over the weekend wakawa wamerudi zao kwao by Jumatatu wakanitumia report yao ambayo ilikuwa nzuri tu kwetu. Kiufupi walikuwa very impressive na implementation ya projects na feedback tuliyowapa. Na walijicommitt kuongeza funding ili kufukia fukia magape ambayo yalihitaji more funding dadeki. It was a big experience for me and I was very proud of myself kwa kuhandle ile situation. Tuliposoma ile report na yule mhasibu pale ofisini tulipiga kelele za furaha utafikiri machizi.
Ilipofika Jumatano usiku kwenye saa 4 usiku hivi nikiwa nipo pahala nafatilia boli chama langu the gunners mara naona simu ya bosi inaita kwa fujo. Nikasogea pembeni kupokea maana mimi huwa napenda kucheki boli sehemu zenye vibe sana, ile kupokea boss akawa anaiuliza maswali mfululizo yasiyo pangiliwa vizuri kutaja kujua kama wageni walija? Walisemaje? Wameondoka? Wapo wapi? Yaani anauliza maswali sijajibu hata moja yeye ameshauliza kumi. Nikamwambia boss calm down ukitulia nipigie nikueleze vizuri nikawa namsikia anahemea juu juu simu yake ikakatika.
Kidogo PS wake ananipigia ndo kuniambia kwamba wamefika sehemu ambayo angalau kuna network na bosi alipanda kwenye kilima kidogo ili kupata network nzuri. Akaniambia yaani boss amejuta kwenda kwa babu maana walinasa njiani kwa siku mbili katikati ya safari wakilala kwenye gari. Akanipa pale situation yakule ilivokuwa worse ila chazaidi boss kilichomchanganya ni hao wageni. Mara kidogo nikasikia sauti ya boss kwa mbali inamwambie muulize wageni walikua. Basi nikatoa mrejesho wote jinsi ilivokuwa na jinsi walivoturecommend kwenye ile report yao angalau boss mcheche ukamuisha kabisa. Boss akaniomba nimfoadie ile report maana hakuiona kwenye email yake, na mm nikakumbuka kwamba wale wazungu ile report walinitumia mimi tu hawakumcopy mtu mwingine – sijui ilikuwaje lakini haikua kesi.
Basi ijumaa yake asubuhi sana boss aliwahi sana ofsini ili kufanya kikao na sisi na ile pia nimpe full picture. Kiukweli alikuwa ameedhoofika gafla sana sasa sjui sababu ya shurba za njiani kwenda kule kwa babu au mambo mengine. Basi nikatakiwa nitoe mrejesho pale na kwa mara kwanza nikaona tabasamu la boss ofisini. Aliisoma ile report ya wazungu mara mbili mbili. Na hapo hapo akaniuliza kama mkataba wangu wa kazi nilishasaini nikamwaba bado. Akaniuliza kwa nini nikamwambia bado sikuuelewa kwahiyo nilikuwa nasubiri muda mwafaka wa mimi nayeye kujadili vipengere ambavyo sijavielewa. Basi akawaruhusu wengine watoke nje mimi nayeye tukabaki. Akanitaka nimweleze kingere ambacho sikukielewa. Nikamwambia mwanzo nilikuwa nataka anieleweshe majukumu yangu lkn nashkuru kwa sasa nimeyaelewa ila kipengere cha remuneration hakipo kwenye mkataba. Akaniambia alikiacha makusudi kwa sababu hakuwa na uhakika wa anilipe kiasi gani kwani yeye analipa kutokana na utendaji kazi wa mtu. Pale pale akaniambia kutokana na utendaji wako kwanza nakuandikia barua ya kumaliza probation period na nitakulipa nusu ya mshahara wangu. Nilikuwa siju boss analipwa sh ngapi nikajisemea cha muhimu ni angalau kufikisha 6 figures bhana kwenye cheque – hahaaa. Basi niakprintiwa mkataba mwingine pale nikaanguka signature bila kuwaza.
TUKUTANE USIKU WA LEO.
NB: Wakuu bado nasisitiza naandika uzi huu ili kushea yale niliyopitia na kujifunza katika mlolongo wa mambo mengi kwenye harakati zangu za kuajiriwa sehemu mbali nikiamini yanaweza kuwa na faida kwa wengine.
So far sina ajira kwa muda wa mwaka sasa na mimi nipo kwenye kundi la wanaosaka ajira. Kama kuna mdau ana connection kulingana na uzoefu, skills na knowledge yangu tunaweza kuwasiliana maana huku mtaani sio poa. Kwa sasa inaweza kuwa mapema kujua skills na experience nilizo nazo tuendelee kuwa pamoja huko mbele kuna uzoefu mwingi zaidi. Mpaka sasa nimeshea uzoefu niliopata katika ajira yangu moja tu wakati zipo tatu zaidi nilizopanga kushea nanyi.
Nimerudi sasa😂😂Unaenda wapi kwani[emoji23][emoji23] wakati kushaanza kunoga
Kwahiyo unataka atudanganye siyo? 🤣Mkuu TAI DUME story yako ni nzuri sana na imejaa mafundisho kwa watu wa aina mbalimbali. Ila nakushauri kwamba ongea yote ila usisahau kipengele cha kula tunda kimasihara, ni kipengele muhimu sana kwa story zinazobamba hapa Jf. Ongelea hata mahusiano ya boss na PS au unda story ya aina hiyo wewe na demu wako wa kitaa au wateja wenu hapo kazini ilimradi kisikosekane tu.
Asante.
Comment bora ya kufungia mwaka..Mungu baba naomba umuepushe huyu kijana na “njaa” Mungu najua fika ni kijana mdogo awezi kujua maana ya njaa na ninakuomba usimpitishe kwenye njaa kamwe…kwa huyu atakufa mapema sana!
Mungu nakuombe huyu umfundishe kwa njia nyingine sio njia ngumu hasa ya kumpa njaa …ni maneno tuu wala haijui njaa bali ana tania tuu!
Amen!
🔥☺EPISODE 4: Avoiding taking sides amongst staff conflicts made me a hero and profesional
Maisha ya kazi pale ofisini yaliendelea huku nikiendelea kuzoeana na watu pale ofisini. Ofisi ile ilikuwa na only 5 employed staff yaani Mr KJ the boss, mimi, Mhasibu, PS na dereva. But most of the tasks involved external outsourcing. Maisha yaliendelea miezi ikakatika na ndipo nilipozidi kuzijua pia tabia za watu pale ofsini, na uhakika hata tabia zangu pia zilianza kufahamika na wengine.
Sasa nikaja kuthibitisha kwamba PS na Mhasibu ni paka na panya. Hili nilihisi siku nyingi lakini nilikuwa bado kuthibitisha. Basi wale madada kila mmoja kwa wakati wake akipata time ya kuongea na mimi basi ni kumkandia mwenzake. Kiufupi wale madada walikuwa kila mmoja anataka niwe upande wake. Yaani nilikuwa siulizi jambo la mtu ila najikuta nimeambiwa, at first nikajua ni mambo ya wanawake tu lakini as time went on nikarialize wale wadada wana biff kubwa sana. Therefore I was finding the proper moment to make it clear that I was there to work and I didn’t want to get involved in office politics.
Nilipofanya upelelezi nikaja kugundua kwamba wale watu kila mtu alikuwa na strength anazoringia pale ofisini hivyo kujiona anaweza kumvimbia mwenzake. Nilikuja kugundua kwamba yule PS alikuwa ni zaidi ya boss pale ofisini kwani maamuzi mengi ya uendeshaji wa ofisi yeye alitia mkono wake. Siku niliyokuja kujua kumbe hata ule mshahara wangu ambao ni nusu ya mshahara wa boss yeye ndio aliyemtaka boss anipatie nilipigwa ganzi ya mwili. Yaani yule PS akitaka ubaki ofsini unabaki, akitaka utimuliwe kazi unatimuliwa. Unaambiwa wengi waliopita pale kwenye position yangu na madereva waliondoka kwa sababu PS hakuwapenda hususani madada nilivosikia. Kuna hawa service providers kama ishu za internet, usafi, stationaries nk ilikuwa ili wapate kazi pale ofsini basi kwanza walimridhishe PS ndio wanapata tender.
Kwanza yule PS alikuwa PS kweli, ile pisi ilikuwa inafanana na toto za Kinyarwanda zenye mibinuko maridadi kwa nyuma halafu mavazi yake ya ofisini ukikutana nae usiku unaweza sema anaenda kujiuza. Sijui alimpa nini bosi wangu mpaka akawa ni mshauri wake mkuu unaambiwa, bora ukosane na boss unaweza kusavaivu kuliko ukosane na PS, imekula kwako.
Kwa upande wa yule Mhasibu nikaja kujua kwamba anabond kubwa sana na asilimia kubwa ya donors wa pale ofisini na aliaminika sana na board members. Yaani yule dada alikuwa ameiva kwenye kazi yake na akajijengea uaminifu mkubwa sana kwa wafadhili kiasi kwamba linapokuja swala la finance wafadhili na board members huwaambii kitu kwake yaani kauli yake ni kama sheria kwenye kusimamia mambo ya fedha. Nilisikia kuna kipindi alipigwa zengwe na PS aondoke, wafadhili baadhi wakatishia kusitisha kuprovide fedha zao endapo mhasibu yule angeondoka mpaka watakapopewa sababu genuine za kueleweka. Ngoma ikawa nzito ikabidi abakishwe. Sema yule dada hakuwaga na vinyongo na watu wengine waliopita kwenye position yangu au watu wa tendering labda uwe mbadhilifu wa fedha anakuchoma moja kwa moja sio kwa boss bali kwa wafadhili. Kifupi yule mhasibu ni kama aliwekwa pale na wafadhili ili kusimamia upigaji, so there was no way majungu ya PS yangeweza kumfukuzisha kazi.
Imagine upo kwenye situation kama iyo ambapo kila upande unataka uungane nao ili kuimarisha kambi yake. Hii niliichukulia kama changamoto kubwa sana kwangu na ukiangalia ilikuwa ni ajira yangu ya kwanza na mimi lengo langu pale lilikuwa ni kugrow ili kupata weledi wa kazi. Nikajiapiza siwezi pale kwamba siwezi haribu carrier future yangu kisa hawa madada wawili. Pale ilikuwa onikichoose upande wa PS basin i wazi Mhasibu atanifanya adui nap engine kuniharibia hata kwa wafadhili kwa mbinu yoyote maana hili nililiona liko wazi japo yeye hakuwahi kunitamkia. And viceversa, nikichagua kambi ya Mhasibu basi automatically nitamjua PS ni nani maana nitapigiwa zengwe kwa boss mpaka niseme.
I remember one day ilikuwa ijumaa, ofsini siku hiyo nilikuwa mimi na PS tu, boss na mhasibu walienda kwenye meeting wakatawanyikia huko huko. Sasa hiyo siku kuna washkaji zangu flani watatu nilipiga nao Olevel wakawa wananipigia sana tukutane maeneo ya breakpoint sio mbali na ofisi. Kipindi hicho pale breakpoint ya posta ilikuwa inabamba sana siku za ijumaa kwa sababu wafanya kazi wengi wa posta ilikuwa ni sehemu yao ya kula bata. Basi PS akaniambia nay eye anataka kwenda akale ili asepe. Mimi nilikuwa sipendi kabisa mazoea kama hayo ya kufatana fatana naye ila aling’ang’ania sana nikaona sio kesi wacha twende.
Nakumbuka vizuri sikuhiyo PS alikuwa amevaa kijigauni kifupi ambacho kilimbana na kilichora umbo lake matata sana. Wakati tunashuka pale breakpoint (PS alikuwa anadrive jamani hahahaa nilisahau kuwaambia) kwenda kule ndani nikawa aibu naona mimi maana watu walikuwa wanatukodolea balaa nahisi mafisi ya mjini yalisema hichi kibwamdogo kinapata wapi uwezo wa kula ile mashine. Na kweli kimuonekano PS alikuwa ni wa level za juu sana ukilinganisha na mimi hahaaa.
Basi tukajoin na washkaji pale wale jamaa zangu walishoboka sana na PS. Uzuri pia PS ni mtu wa kujichanganya sana yaani dakika 0 tu ugeni umeisha na anazigida pombe vizuri tuu. Kile kikao kimeenda mpaka kama saa mbili hivi usiku ikaja proposal watu tuhame. Sasa mimi nilivoona PS amewaka kimtindo nikaona hawezi kuendesha huyu hivyo nikamshauri ndinga akaache ofisini ili tutumie usafiri wa wale jamaa zangu maana sio salama. Akanipa key nikapeleka gari yake kisha tukasepa. Kiufupi siku ile wale jamaa zangu wa mgodini walikuwa na pesa sana walikuja mjini kula bata.
Kufika mida ya saa nane usiku mimi nimechoka sasa nikawa namlazimisha PS achukue bajaji aende kwake wale jamaa wakawa bado wanataka kampani yake na PS ndio haelewi anataka aendelee kula bata. Japo alikuwa ni mtu mzima lakini nikaona siwezi kumwacha na wale majamaa ya mgodini imani yangu sikui iliwaza nini kutowaamini. Sasa PS kuna namba za nyummbani kwake ilikuwa inampigia mara kwa mara nahisi ni dada wa kazi yule alikuwa anampa maelekezo kuhusu mtoto. Lkn kuna namba nyingine ilikuwa ikimpigia anasogea pembeni anaongea kisha anarudi tunaendelea na mambo. Sasa kuna muda akawa ametoka kuongea na simu akanipa mimi nimshikie simu zake yeye akawa bize na story. Kidogo mimi nikaanza kumlazimisha tuondoke nikampandishe bajaji akalale. Kweli nikafanikiwa sasa wakati nampa zile simu zake kuna moja nikaona ipo hewani yaani alipomaliza kuongea haikukatwa na zilikuwa zimepita kama dk 40 hivi. Basi nikaikata na kila mtu akashika njia yake.
Asubuhi ya saa 12 Jumamos nikiwa nina mausingizi kibao maana nilichelewa sana kulala nikasikia simu ya boss ikiita. Kucheki nikakuta missed 3 za boss nikampigia. Alichoniambia ni maneno matano tu – Tukutane Ofisini Leo Saa2 Asubuhi. Akakata simu. Baada kama ya nusu saa PS ananipigia simu kuniambia boss kasema tukutane ofisini asubuhi na wewe ila mimi nimemwambia siendi nimechoka. Nikamwambia mimi pia kaniambia ila wewe unapata wapi ujasiri wa kumkatalia boss wako bila sababu. Nikamshawishi akakubali maana nilimwambia pia inabidi akachukue usafiri wake. Basi ikawa hivyo mimi nikajiandaa faster nikaanza kuelekea ofsini. Kwa kuwa ilikuwa Jumamosi nikapiga zangu pensi, sendo na Tshirt tu sikuwaza sana kutoka kioficial na nikajisemea some times its better to expose your few characters.
Pale ofsini kama tulitanguzana tuu na PS coinsidencily na yeye alikuwa amevaa kipensi kipedo cha blue kama pensi yangu ila juu alivaa zile makenzie enzi hizo ndio zinatoka toka tuu. PS alikuwa ni mtu wa kwenda sana na fasheni. Basi ile tunaingia tuu ofsini tunamkuta boss amekaa kwenye ofisi yangu anatafuta tafuta sijui nini kwenye desk yangu. Alipotuona tuu akakasirika sana na kutuuliza kwa hiyo mmeona kulala pamoja haitoshi mkaona mmechishe na nguo kabisa halafu mnakuja ofsini kama ofisi ya babaenu sindio? Kwanza sikumuelewa lkn ikabidi kwa nijiangalie mavazi ndio kujua wote tumevaa shorts na zote za jinsi za bluu. Nikaona leo hapa wahaya wamepanda kichwani.
Siku hiyo boss alinifokea sana kwa nini namuingilia kwenye anga zake. Kiufupi zile simu ambazo PS alikuwa anaenda kupokelea pembeni zilikuwa ni za boss. Sasa sijui alikuwa anamdanganya yupo wapi mana alikuwa alikuwa anapokelea kwenye ukimya. Sasa ile simu ambayo PS hakuikata kumbe ilikuwa ni ya boss na alivorudi palena kunipa mimi nimshikie boss alisikia na kurekodi kila kitu. Mpaka mimi navomwambia tuondoke mpaka nilivokuwa nabagain bajaj bos anasikia, so alijiaminisha mimi naingilia anga zake na jana nimekula mzigo. Duuh unajua nilipagawa sana. So akaniambia ameshaniandalia barua ya kuachishwa kazi nilipomuuliza ana hoja gani akasema wazi eti nimeshindwa kushawishi menejeiment kipindi nipo kwenye probation.
Kipindi hicho chote boss anafoka PS yupo kimya. Mimi namwangalia kwa yale macho ya kuuliza mbona upo kimya si umueleze ilivokuwa? Ni kama alinisikia. PS akamwambia tena kwa kumuita kwa jina lake huku akimlegezea sauti “KJ njoo ofsini kwako mara”. Boss wangu masikini ukali wote ukaisha akaelekea ofsini kwake kama ngamia anavoelekezwa kibla. Basi mimi nikawa nimekaa tu nimejiinamia reception wao wapo ofsini kwa boss. Wamekaa huko kama dakika 40 nzima mara PS akatoka akaniita. Nikaingia kwa hofu sana. Chaajabu boss alikuwa mpole sana na akaniomba msamaha kwa kunifikiria vibaya na eti ananishukuru kwa kuwa muungwana kwa PS wake. Akaongea mambo mengi lakini kubwa na msisitizo alinipiga mkwara mzito kwamba hawezi hata siku moja kukubali pusi yoyote (alitumia neon hilo hilo pusi) kuingia kwenye 18 zake kwa huyo PS. Na akasema tuongee tu kama wanaume yeye huyo PS wake amemgharimia vitu vingi sana ikiwemo mjengo (ambao umeshakamilika lkn PS bado hajaamia), usafiri na bills zote za mjini. Na akanambia ananiambia hayo kwa sababu anaamini mimi nipo smart kichwani hivyo hataki kuniopoteza na anamini nitakuwa na msaada kwenye ile ofisi. Ingekuwa mimi ni kama pusi wengine asingesubiri hata tuonane ofisini kunipa nafasi ya kujitetea angenitimua job kwenye simu tuu kama alivowafanyia wengi tuu waliopita.
Basi kikao kikaisha hivyo sasa sijuiPS alimwambia nini kule ndani wakati mimi sipo. Mimi nikaaga pale nikaondoka zangu wao nikawaacha. Ila nilikuwa na mawazo sana kwa sababu nikaona pale ofsini panatakiwa uishi kwa akili sana yaani vibiff vya ajabu ajabu sana na kila mtu anataka uwe upande wake. Maana wakati nimetoka boss alinitumia meseji iliyosomeka “nimekusamehe wewe endelea kufanya kazi kwa bidii na kama sipo ofisini nataka umchunguze …….. (PS) mienendo yake kisha unijulise”. Nikaona huu sasa sio weledi I have to do something about this.
Kwa kawaida pale ofsini kunakuwaga na Monday briefing sessions ambapo kama boss akiwepo tunapeana updates za wiki iiyopita na plan for the due week. Bahati nzuri next Monday since hiyo saga yangu ya PS na boss itokee tulifanya hiyo meeting. Tulipeana updates pale na plan za wiki then kwenye ile session ya mengineyo nikanyoosha mkono nikaruhusiwa, Nikasema leo liwalo na liwe.
Kwanza niliwashukuru kwa kunipokea pale kazini na ushirikiano walionipa kwa kipindi chote hapo kazini. Boss aliposikia hiyo hiyo intro akashtuka sana akaniuliza “Taidume unataka kuacha kazi sababu ya mambo yale ya jana?” ni kama aliropoka. Hii kauli ilimfanya mhasibu ashangae na kuuliza kwani jana kilitokea nini boss? Kabla hajajibu boss mimi nikaendelea. Hapana boss siwezi kuacha kazi kwa sasa kwani bado napenda kufanya kazi hapa ila nataka tu kuweka msimamo wangu sawa ili kuweka mazingira yangu ya kazi mazuri. Boss akaniuliza una maana gani? Nikamjibu, kwanza boss jana nimefurahi sana kwa kunielewesha ukweli na hii imenifanya kuwa huru. Haya maneno niliyaongea makusudi mbele ya mhasibu kwa sababu ni zaidi ya mara tatu aliwahi kuniambia anatafuta timing nzuri awachane PS na boss waache kuchanganya mambo ya mahusiano yao na kazi, yaani kama wanamahusiano wawe na mipaka kwani imefikia hatua PS ana maamuzi unprofessional yanayoathiri shirika.
Basi nikaendelea. “Najua mhasibu wewe unafahamu mahusiano ya PS na boss, najua pia boss unafahamu biff la chini chini lililopo baina ya PS na Mhasibu, lakini pia najua wote PS na Mhasibu mnajaribu kunishawishi ili niwe upande wake, na pia najua ni kwa nanmna gani PS alivo na ushawishi kwako bosi. Sasa haya mazingira kwakweli yananifanya mimi kufanya kazi kwenye mazingira magumu mno. Natamani kufanya kazi kwenye mazingira ambayo yatawezesha mimi kuendelea kujifunza na kufanya kazi kwa kushirikiana.
Nikaanza kumsifia mmoja mmoja pale mchango wake katika ufanyaji kazi wangu pale. Nikaanza na boss. Nikamwambia boss wewe unajua ulikonitoa nilikua hapa nikiwa sina skills zozote lakini leo hii angalau ninaweza kujimudu katika majukumu yangu na CV yangu imeboreka. Bado nahitaji kujifunza vitu vingi sana kutoka kwako kwani wewe umekuwa role model wangu kwa vitu vingi sana professionally. Kwa mHasibu nikamwambia napenda sana jinsi anavopangilia mambo yake ya kazi kwani uko very smart. Kwako wewe A ni A na B ni B umenifundisha kunyooka na kusimamia weledi kwenye kila jambo hata likiwa dogo. PS naye nikamwambia asione yeye kama hana msaada kwangu may be hajui tuu. Nikamwambia impression aliyonipa siku ya kwanza jinsi alivonipokea ilinifanya njione pale ni nyumbani. Nikamwambia ule muda anaotumia kunisaidia kuchakua chakua kule kwenye mafaili kama kuna taarifa nazitafuta unaiokolea mambo mengi sana na muda. Niliongea kwa hisia sana siku ile vitu vinavyonikwaza mpaka kupelekea mhasibu na PS kulengwa lengwa na machozi. Mwisho nikawaambia as for me I will never choose any side for personal interest, but I will always be cooperative to the team for organization interests.
Boss akaniangaliaaa mwisho akasema mwingine mwenye dukuduku. Asee yule mhasibu alivunja ukimya alifunguka mambo mengi sana mpaka alilia sana tukaanza kubembeleza. Tena aliyembembeleza sana alikuwa ni PS walikuambatiana wakalia hapo huku mimi na boss tunawaangalia tuu. Badae wakaombana misamaha pale, sasa sijui ilitoka moyoni au midomoni. Mwisho boss aliuliza nini kifanyike ili kuboresha utendaji wa ofisi. Tukatoa toa proposal pale tukakubaliana tufanyie kazi mikakati tuliyojiwekea. Kwenye kufunga kikao boss alinishukuru sana kwa kuibua hoja hiyo na kwa kuwa kikao kikao kilitumia muda mrafu mpaka mchana boss akaoendekeza tukale lunch nje ya office. Iilkuwa poa sana maisha baada ya hapo kama kulikuwa na usnitch basi ni ule wa chini chini sana.
Don’t miss episode 5, to see how honesty na kutokuwa na tamaa kulivonipa another job connection
😂😂👐Huyo jamaaa mzito sana badala yeye achukue mhasibu amuachie boss PS dah [emoji91][emoji91]
Sent from my Pixel 4a (5G) using JamiiForums mobile app