Mambo muhimu ya kufanya pindi tu unapopokea taarifa za msiba wa mzazi wako au ndugu yako wa karibu

Maandika yanatuasa kuwa tayari ,maana hatujui siku wala saa
Binadamu tunajisau sana tuwapo duniani .Hasa wenye uhakika wa kula na kuvaa ,kulala pazuri na kufanya mambo ya kidunia kama wapendavyo.

Watu husahau kabisa kwamba kuna mauti ,watu wako busy na mishe kila kukicha na malengo mia zaidi,hawajui kabisa kwamba kuna kuondoka siku yoyote.
Watu hawana habari kabisa na Mwenyezi Mungu,watu huishi kama vile walijileta duniani,wana kejeri kwa wenzao,dharau ,wenye kudhihaki,wasio thamini wengine,wenye kiburi,waongo na wasio mtumainia Mwenyezi Mungu.

Mauti yapo na tunatembea nayo.watu tumtumainia mwenyezi Mungu inabidi kujitayarisha kwa yajayo,yawe mema au mabaya.

Mtu mwenye imani thabiti haogopi kifo ,mana tupo ili tufe,na pale jambo baya linapo kufika yabidi umtumainie mwenyezi Mungu mana hauna uwezo wa kubadili kuwa vile unataka wewe.

Mwenye imani hofu na mashaka huwa havipo ,tunahofu na kifo mana hatuna wema ndani yetu.tulishajikatia bima ya uhai wa hapa hapa duniani,watu hawataki kuondoka duniani,na akiona wa karibu yake kaondoka atalia hadi kamasi, kugalagala chini,kufuru kama zote na anamalizia na kuzimia,
Akiamuka tena analia hadi anavua nguo na kutamka maneno yasiyo kuwa na matumaini.

Alichosema mtoa mda yupo sahihi kabisa ,kujiandaa ki roho ni bora zaidi ya yote.Tusiwe kama wasio na imani,
Kama tukiishi twamishia Mungu, na kufa kwetu ni faida.kila kukicha yatupasa kusali na kutambua ya kuwa mauti ipo na hakika ipo siku tutakufa na wapendwa wetu wataondoka .
Basi tufe kifo chema na chenye matumaini,tusiishi kama wanyama wasio na akiri

Wapumzike kwa amani walio tutangulia.
 
Hili suala limekaa kiimani sana Kumuombea marehemu apumzike salama..hii naona haina mantiki yoyote
Ya ni kweli mkuu, wengi wameongea hivi na hata mimi naamini hivyo, lkn hili ni swala la kufarijiana sana.

Kwani mfiwa anapomuombea baba yake, mama yake au ndugu yake fulani huhisi kama amemfanyia flavour fulani ambayo pengine inaweza japo kumsaidia huko alipo.

Ndio pale utasikia watu wanasema RIP, Pumzika kwa amani au ulazwe mahali pema peponi nk.
 
Mkuu umeandika maneno ambayo yamenigusa sana moyo wangu. Hakika ulichoandika kinamantiki kubwa ndani yake, na mwenye akili anapaswa kukizingatia.

Anaeongea maneno ya Mungu kwenye mitandao kama hii anakuwa ameisaidia jamii kubwa iliyomsahau Mungu na kumkumbatia shetani. Huu ni ukumbusho wenye faida kwa kila anaeamini uwepo wa Mungu.

I hope wenye macho wamesoma na kuelewa, na wenye akili wamezingatia na kuyafanyia kazi.
Baraka za Mungu zikushukie popote ulipo.
 
Huyo Mungu huwezi kuthibitisha kwamba yupo.
 
Huyo Mungu huwezi kuthibitisha kwamba yupo.
Mkuu umesoma vizuri lkn hapo chini ya uzi wangu, au umekimbilia kuandika kabla ya kusoma thread yote?
Hii ni kwa wale tunaoamini uwepo wa Mungu, bila kujali dini ya mtu. Ila wasioamini uwepo wa Mungu naomba wasome tu lakini wasiandike chochote kuharibu uzi huu.

Karibuni ndugu zangu.
Mimi nilijua kama watu kama nyinyi hamkosekani ndio maana nikatoa angalizo mapema.
 
Dah nimesoma mpaka mwili umesisimka... Eee Mungu naomba uwalinde wazazi wetu πŸ€”πŸ€”
 
Mkuu umesoma vizuri lkn hapo chini ya uzi wangu, au umekimbilia kuandika kabla ya kusoma thread yote?
Mimi nilijua kama watu kama nyinyi hamkosekani ndio maana nikatoa angalizo mapema.
Imani ni kitu cha faragha yako, fanya kwako, msikitini, kanisani etc.

Ukiileta imani in the public sphere, umealika uchambuzi.

Huko mtu akikuingilia, hata mimi nitatetea haki yako ya kuamini unachotaka bila kuingiliwa.

Ukileta imani yako JF, umeianika ichambuliwe.

Nakwambia hivi, huyo Mungu wako mwenyewe ni wa hadithi tu, hayupo.

Ndiyo maana huwezi kuthibitisha yupo.

Kama unabisha, thibitisha yupo.
 
Umejaza tu Kumuomba Mungu kumuomba Mungu lkn hutoi solution ya maana, kuomba sio solution kma akiki yako bado haijakaa sawa,

Suala la kwanza ni saikolojia yako, hili ndilo jambo la msingi kuliko yote hapo, kuomba Mungu kunafuata baada ya akili yako kutengamaa na kukubaliana na ukweli pia kuwa na uwezo wa kuhandle machungu, usipokuwa vzr kisaikolojia hata uombe/uombewe vipi ni kazi bureeee...
 
Mkuu ndomaana nikasema kama kuna mungine anaeweza kujazia jazia kama hivi ajazie ili watu wengi waendelee kujifunza kupitia uzi na comment.
Shukran kwa mchango wako wenye faida na manufaa kwa wasomaji.
 
Dah nimesoma mpaka mwili umesisimka... Eee Mungu naomba uwalinde wazazi wetu πŸ€”πŸ€”
Ndo hivyo mkuu, hili ni swala ambalo haliepukiki katika maisha yetu.

Mungu awalinde wazazi wetu na atupe mwisho mwema.
 
Uchafu gani wakati wa msiba mkuu???
 
4) Jambo la nne tumia muda mwingi kumuombea marehemu ili apate makazi mema au Mungu aipokee roho yake na kuiweka katika roho za walio wema.
Kumuombea marehemu ni kupoteza muda tu. Mtu mwenyewe alipokuwa hai hakurekebisha mambo yake na Mungu afe ndiyo watu baki mumuombee makazi mema na roho yake kupokelewa mbinguni/akhera?

Ukifia dhambini ndiyo imetoka hiyo; na faili lako limefungwa. Tujitahidi kurekebisha mambo yetu na kuwa na mahusiano mema na Mungu tukiwa hai πŸ™πŸΏ

 
Ndo mana tukasema inategemea na mtu. Ila ukiwa unamuomba Mungu kwamba siku likitokea tukio la aina hiyo akuongoze katika haya manne, basi uwezekano wa kuyafanya kupitia Mungu upo.
Mungu atutie nguvu na atuepushe na vifo vyenye maumivu makali.
 
Asante mkuu kwa ujumbe huu kupitia biblia takatifu. Nina imani wengi watajifunza kupitia andiko hili.
 
Omba upate fedha za kutosha kutoka kwa marafiki usitumie akiba Yako isipokuwa kwa mahitaji maalumu
 
Msiba ukikufika hutakumbuka hata moja hapo,tena unaweza shtuka wiki imepita mlishazika ndo wewe unarejewa na utimamu, siku zote 7 unakokotwa tu
 
Msiba ukikufika hutakumbuka hata moja hapo,tena unaweza shtuka wiki imepita mlishazika ndo wewe unarejewa na utimamu, siku zote 7 unakokotwa tu
Wapo ambao wanakumbuka mkuu, inategemea mtu na mtu.
Msiba unauma, lkn ni jambo ambalo huwa haliepukiki na kila mmoja wetu anakubaliana na jambo hilo. Hakuna mtu asiekubali kuwa kuna kufa au kufiwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…