Mambo tofauti tunayokutana nayo Madereva wa malori toka enzi

Mambo tofauti tunayokutana nayo Madereva wa malori toka enzi

mkuu endeleza hi stori tupate watu kujifunz ukisubili wabishi wamalize kubisha n wazi hutaweza kuendlea mana watu wnabishaga t hyo n kawaida yetu wnadam. lete hadithi watu tupate kujua mamb y dunia
 
Hii ni kwa ufupi juu ya mambo mbali mbali tunayokutana nayo toka enzi mpaka leo hii.....Mengine hudhaniwa ni ya kutunga mengine yanahusishwa na uchawi na ushirikina hasa kwenye makampuni ......
Basi hapa nitakuwa nampeni stori tofauti tofauti juu ya vituko na mambo ambayo si ya kawaida sana katika ulimwengu huuu.

Miaka mingi imepita tulikuwa tunasafiri kuelekea Mpanda tuna lori limekula nundu ya kutosha mixer vipeto ..unajua njaa tena.....sasa njia tuliyopita ni ya Manyoni halafu unakata kushoto kuelekea Rungwa kisha unakata kulia kuitafuta KItunda....hapa tulipishana na basi la SABENA linatoka Tabora kueleke Mbeya hii njia kwa miaka hiyo ni njia dume kwelikweli na tulikuwa tunapita nyakati za kiangazi...aidha tulikuwa tunatembea na kila kitu muhimu kwa dharura ya aina yoyote ile.....

Kwa kifupi kuna pori linaitwa Mpembampazi hapo kuna Simba wakubwa kuliko simba wote niliokwisha kuwaona pia kuna Twiga weupe....anyway .......ilikuwa majira ya kama saa kumi na mbili jioni hivi machine inaunguruma mdogo mdogo taa nilikuwa nimewasha ingawa giza lilikuwa sio zito bado kulikuwa na mwanga.....zingatia ni ndani ya msitu(pori ) nene.....mara taa za gari zikawa zinajiwasha na kujizima zenyewe kama vile zimechanganyikiwa...halafu gari likazima ghafla....kwenye gari tulikuwa watu sita..mmoja kwenye kiti kushoto..... wawili kitanda cha chini...... na wawili kitanda cha juu.....wote tukawa kimya tunatafakari....kujaribu kupiga starter hata switch on haionyeshi.....tukawa kimya kama dk. moja hivi.....mara ukapita upepo wa baridiii upepo mkali kiasi halafu kimyaaa......mara tukasikia mlia shwaa shwaaa shwaa shwaaa kama vile kuna kitu kinaji buruza....

Kuangalia mbele tulishuhudia nyoka mweupe kama maziwa hana madoa doa ni mweupe tuu unene wake ni kama sadolin yaani diameter yake.....halafu kakatiza barabara kwa mbele....wote tuko kimya tunamuangalia tu....kichwa kikapotelea chakani lakini kiwiliwili bado kinakatiza barabarani....,,na mlio shwaa shwaa shwaaa.....duuuh...sasa cha ajabu zaidi mkiani alikuwa anawaka taa...taa ya rangi ya blue..na ina mwanga wa kutosha.....yaani mkia wake ulisimama juu kama mkia wa ng'e..halafu kwa juu kuna kama kakikombe ndio kuna kama jiwe hivi ndio linalotoa huo mwanga........bahati mbaya zamani hizo tulikuwa hatutembei na kamera.....
kwa kifupi baada ya joka kupotelea kichakani gari lilikubali kuwaka na tukaendelea na safari...sasa baada ya kufika Mpanda tukawahadithia jambo tulilolishuhudia......wakafurahi sana wakatukaribisha sehemu fulani kuna wazee wanakunywa pombe za kienyeji...walituhoji na kupata uhakika kabisa kwamba huyo nyoka wanamfahamu na kumuona ni bahati kubwa sana na huonekana mara moja baada muda mrefu sana na lile jiwe linalowaka taa ni jamii ya LULU....
.....ITAENDELEA>>>>>>>>
Hata mngeekuwa na camera, mngempiga ingekataa.
 
Imani kwamba baadhi ya nyoka wanamiliki vito ambavyo huangaza usiku ni hadithi ya kuvutia inayopatikana katika tamaduni mbalimbali, ikiwemo za Kiafrika. Hadithi hii inaonyesha uhusiano wa kina kati ya binadamu, asili, na sifa za kiajabu zinazohusishwa na wanyama.

Hadithi ya Nyoka na Vito Vinavyotoa Mwanga

Katika mila nyingi za Kiafrika, inasemekana kwamba nyoka fulani wa nadra hubeba jiwe la kichawi, mara nyingi huitwa "jiwe la nyoka" au "jiwe la mwanga," lililopachikwa kwenye kichwa chao au vinywa vyao. Vito hivi vinaaminika kutoa mwanga unaong'aa, na kusaidia nyoka kuongoza njia yao usiku.

Vipengele vya Kawaida vya Hadithi:

1. Madhumuni ya Jiwe:
Jiwe hili linasemekana kumsaidia nyoka kuwinda gizani au kujua njia katika mazingira yenye giza totoro, ikionyesha akili na asili ya kichawi ya nyoka.

2. Nguvu za Jiwe:
Jiwe hili mara nyingi huelezewa kuwa na mali za kichawi, kama uwezo wa kuleta ulinzi, utajiri, au uponyaji kwa mtu yeyote anayemiliki jiwe hilo.

3. Mwingiliano na Binadamu:
Hadithi nyingi husimulia jinsi watu walivyojaribu kuiba jiwe kutoka kwa nyoka, mara nyingi kwa kumlaghai nyoka kwa maziwa au kumsababisha aache jiwe hilo. Hata hivyo, majaribio haya mara nyingi ni hatari kwa sababu nyoka hulinda hazina yake kwa nguvu.

Tofauti Katika Tamaduni Mbalimbali

Afrika:

Hadithi za Wazulu: Baadhi ya hadithi za Wazulu zinasema nyoka wanaomiliki mawe yanayotoa mwanga, ambayo huaminika kuwa zawadi kutoka kwa miungu. Mawe haya yanahusishwa na uzazi, mvua, au ulinzi dhidi ya roho mbaya.

Makabila ya Afrika Magharibi: Katika baadhi ya makabila, jiwe hilo huaminika kutibu magonjwa au kuleta mafanikio kwa wale wanaolipata, lakini kulichukua kunahitaji ujasiri mkubwa na hekima.

Asia:

Hadithi kama hizo zinapatikana katika tamaduni za India, ambako nyoka wa cobra wanaaminika kuwa na "mani" (jiwe la thamani) kwenye vichwa vyao, linalohusishwa na nguvu za kiungu.

Ulaya:

Hadithi za Kati za Ulaya pia zinasimulia kuhusu nyoka wanaolinda hazina, mara nyingi wakielezewa wakiwa na vito vinavyong'aa au dhahabu, wakisisitiza jukumu lao kama walinzi wa utajiri wa kichawi.

Umuhimu wa Hadithi

1. Mwanga Gizani: Jiwe linalong'aa linawakilisha mwongozo, tumaini, na mwanga katika kukabiliana na changamoto au giza.

2. Ulinzi: Nyoka kama mlinzi wa jiwe linaonyesha wazo la kulinda hekima, hazina, au maarifa takatifu.

3. Mafunzo ya Maadili: Hadithi hizi mara nyingi zinaonya dhidi ya tamaa au kusisitiza umuhimu wa kuheshimu asili.

Ingawa hakuna ushahidi wa kisayansi kwamba nyoka wanamiliki mawe yanayong'aa, hadithi hizi zinaonyesha ubunifu na kina cha kiroho cha tamaduni zinazozisimulia. Jiwe linalong'aa linatumika kama sitiari ya sifa za kichawi na za fumbo zinazohusishwa na nyoka, na kuwafanya waheshimiwa katika hadithi za kitamaduni kote duniani.
 
😂😅 Ukiyadekeza matoto kupita kiasi yanaharibikiwa.. wafundishe skills za mikono , wafundishe kupata na kukosa, wafundishe NJAA DHIKI UMASKINI una Ladha gani?

Bila kusahau tisiwanyime mapigo wanapo kosea period!

NB.
Mifano ipo mingi ya watoto walio dekezwa kwa kupewa kila kitu na baadae yanakuja kua mateja au kuwa wasio taka kufanya kazi wanezoea (KKB)

KULA, KULALA, BUREE (KKB)
Mateja wengi ni masikini,
 
Hii ni kwa ufupi juu ya mambo mbali mbali tunayokutana nayo toka enzi mpaka leo hii.....Mengine hudhaniwa ni ya kutunga mengine yanahusishwa na uchawi na ushirikina hasa kwenye makampuni ......
Basi hapa nitakuwa nampeni stori tofauti tofauti juu ya vituko na mambo ambayo si ya kawaida sana katika ulimwengu huuu.

Miaka mingi imepita tulikuwa tunasafiri kuelekea Mpanda tuna lori limekula nundu ya kutosha mixer vipeto ..unajua njaa tena.....sasa njia tuliyopita ni ya Manyoni halafu unakata kushoto kuelekea Rungwa kisha unakata kulia kuitafuta KItunda....hapa tulipishana na basi la SABENA linatoka Tabora kueleke Mbeya hii njia kwa miaka hiyo ni njia dume kwelikweli na tulikuwa tunapita nyakati za kiangazi...aidha tulikuwa tunatembea na kila kitu muhimu kwa dharura ya aina yoyote ile.....

Kwa kifupi kuna pori linaitwa Mpembampazi hapo kuna Simba wakubwa kuliko simba wote niliokwisha kuwaona pia kuna Twiga weupe....anyway .......ilikuwa majira ya kama saa kumi na mbili jioni hivi machine inaunguruma mdogo mdogo taa nilikuwa nimewasha ingawa giza lilikuwa sio zito bado kulikuwa na mwanga.....zingatia ni ndani ya msitu(pori ) nene.....mara taa za gari zikawa zinajiwasha na kujizima zenyewe kama vile zimechanganyikiwa...halafu gari likazima ghafla....kwenye gari tulikuwa watu sita..mmoja kwenye kiti kushoto..... wawili kitanda cha chini...... na wawili kitanda cha juu.....wote tukawa kimya tunatafakari....kujaribu kupiga starter hata switch on haionyeshi.....tukawa kimya kama dk. moja hivi.....mara ukapita upepo wa baridiii upepo mkali kiasi halafu kimyaaa......mara tukasikia mlia shwaa shwaaa shwaa shwaaa kama vile kuna kitu kinaji buruza....

Kuangalia mbele tulishuhudia nyoka mweupe kama maziwa hana madoa doa ni mweupe tuu unene wake ni kama sadolin yaani diameter yake.....halafu kakatiza barabara kwa mbele....wote tuko kimya tunamuangalia tu....kichwa kikapotelea chakani lakini kiwiliwili bado kinakatiza barabarani....,,na mlio shwaa shwaa shwaaa.....duuuh...sasa cha ajabu zaidi mkiani alikuwa anawaka taa...taa ya rangi ya blue..na ina mwanga wa kutosha.....yaani mkia wake ulisimama juu kama mkia wa ng'e..halafu kwa juu kuna kama kakikombe ndio kuna kama jiwe hivi ndio linalotoa huo mwanga........bahati mbaya zamani hizo tulikuwa hatutembei na kamera.....
kwa kifupi baada ya joka kupotelea kichakani gari lilikubali kuwaka na tukaendelea na safari...sasa baada ya kufika Mpanda tukawahadithia jambo tulilolishuhudia......wakafurahi sana wakatukaribisha sehemu fulani kuna wazee wanakunywa pombe za kienyeji...walituhoji na kupata uhakika kabisa kwamba huyo nyoka wanamfahamu na kumuona ni bahati kubwa sana na huonekana mara moja baada muda mrefu sana na lile jiwe linalowaka taa ni jamii ya LULU....
.....ITAENDELEA>>>>>>>>
Madereva wa malori tunawajua, usikute mlikuwa mshavuta mibangi yenu ikawaletea wenge.
 
Hzo story za majoka nikweli kabisa,,Kuna sehemu moja hv pori lakwenda na Kenya Kuna nyoka pia mkuubwa ye mkiani anakitu Kama chungu ana mayai yana waka usiku..pia kuna mwingine yuko huko upareni..ye kichwani ana kitu Kama jiwe linawaka usiku sana ukibahatisha kulichukua umetoboa sema ndokimbembe..pia kuna mahali kijijini huko ndanndani Kuna joka mkubwa akikatiza barabara nimpaka amalize kupita ndo mpite ukimruka tu umekwisha..maana anapopita anakuwa Kama amezungukwa na mvuke mvuke,,Kuna mgeni mmoja alienda kutembeleaga huko akajitia kichwa ngumu ,,naharaka zake akamruka akaenda zake..joka lilivomaliza kupita kwenda mbele wana mkuta kakatamoto amekaa chini ya mti..so ushukuru gari ilizima maana Kama mnge mpita huyo nyoka mbele mngepata ajali ndokwisha yenu..
Mkuu endeleza story tujifunze
Uwe unaweka sukari, chai bila sukari ni mateso.
 
Chai bora, Kilele cha ubora
Ni chaguo, La watanzania
Kutokana, na ubora wake
Na inavyoburudisha zaidi
Kwenye kununua, Usiseme chai tu
Bali sema, Naomba chai boraaa
 
ujuaji wako ni wa kishamba kusema hakuna pori linaitwa mpembampazi kisa eti ww hujawai lisikia hio haimaanishi halikuwahi kuwepo kwani inategemea umezaliwa lini..ukute mtoa mada anasimulia mapito yake ya miaka 1970-80 huko zamani alafu ww unabishia wakati umeijua dunia kuanzia miaka ya 2000 ukute hilo pori sahivi lina jina lingine ambalo ndio ww unalijua ila zamani lilikywa hilo alotaja mleta mada kwani majina ya maeneo mengi ya zamani yamebadilika kutokana mabadiliko ya vizaz..au ww unafikiri humu JF kila mtu unalingana nae kiumri wenzako wanatoa stori zao za miaka 20- 30 iliyopita ila ww unasoma kama vile ni mwezi uliopita lazima useme ni chai tu sababu unaona maisha yalianza baada ya ww kuzaliwa..penda kujifunza usiyojua
Kwahiyo tukubaliane kuna nyoka mweupe mwenye upana wa sadolin na mkia unaosimama kama wa ng'e wenye jiwe linalotoa mwanga wa blue!? Tumia akili yako vema.
 
Mateja wengi ni masikini,
Utaweza kumudu kununua heroin au cocaine Kama ni maskini..?!

Mpaka kua mteja/mateja ni PROCESS sio Jambo la siku moja..

Ile filing wazungu wanasema HIGH...you get HIGHER.

Mfano mzuri chid Benz anaweza sema kwa kipindi chake kua alikua na PESA kupita wasanii wengi wa zama zake Ila Sasa process ya madawa ya kulevya imemuweka mahala pake
 
mkuu endeleza hi stori tupate watu kujifunz ukisubili wabishi wamalize kubisha n wazi hutaweza kuendlea mana watu wnabishaga t hyo n kawaida yetu wnadam. lete hadithi watu tupate kujua mamb y dunia
Bado anatunga. Mpe muda akimaliza ataleta tu..
 
Back
Top Bottom