Mambo unayopaswa kufanya mwanaume pale ndoa au mahusiano yako yanapovunjika

Ndondombi Mulin

JF-Expert Member
Joined
Mar 13, 2016
Posts
413
Reaction score
1,868
Nasema na wanaume kwa sababu nimesikitika kuona wanaume wakiwa wanarudia makosa yaleyale mara pale mahusiano au ndoa zao zinapovunjika na kujikuta wanapoteza muelekeo wa Maisha yao. Listen;

1. Mwanaume hutakiwi kurukia mahusiano mapya kabla hujaacha 100% yale yaliyopita. Ukisha achana nayo jipe muda wa kuwa single (mwenyewe), focus, tambua wapi ulikosea, rekebisha na ujitahidi uwe bora na imara.

2. Ndoa/Mahusiano sio mashindano. Usiingie haraka haraka ili tu kumuonyesha X wako kuwa unafanya vizuri kumzidi yeye. Hili ni kosa la karne, acha huu ujinga.

3. Pale utakapopata mwanamke, usikimbilie kumuoa au kumpa ujauzito. Kuweni wachumba walau miaka 2 kisha mlete kwako, akifika ishi nae tena walau mwaka na nusu ukiendelea kumjua tabia, kuijua historia yake vizuri zaidi, usiweke hatarini future yako kisa tu anakupa uchi muda unapotaka.

4. Ujue mzunguko wa hedhi wa mwanamke wako. Fahamu tarehe zake atakapokuwa period na uwe na elimu kuhusu tarehe hatari za mimba, pia kuwa na kumbukumbu ya siku unazolala nae. Acha kumwaga shahawa hovyohovyo (kumbuka, shahawa zikitoka mwilini mwako kuingia kwa mwanamke, huwa zinakuwa mali halali ya serikali).

5. Acha kutumia hela vibaya ili umuonyeshe X wako kuwa una hela, hii ni akili ya kimasikini.

6. Acha mazoea ya ovyo na mama mkwe, huyo sio ndugu yako. wakati wote atamtetea binti yake hata upeleke ushahidi wa namna gani. Hakikisha unatatua matatizo yako kwa kuwahusisha wanaume pekee. Baba mkwe, baba yako au ndugu wengine wa kiume, kushirikisha wanawake wataongeza tatizo.

7. Mwanaume hupaswi kuwa emotional attached na watoto wako. Utakapoanza kuongoza watoto wako kwa hisia, utaishia kuwapoteza, utashindwa kuwapa adhabu wanapokosea, utawanunulia wasivyohitaji n.k, na mwisho mama yao akishaona huo udhaifu, basi atawatumia watoto kukuadhibu. hadi utajuta.

8. Sunk Cost Fallacy ni jambo la hatari sana. Epukana nalo. Acha kuogopa kufanya maamuzi magumu kisa tu unahofia kupoteza vitu ulivyowekeza kwenye hayo mahusiano yako. Kuwa na msimamo, fanya maamuzi na uyasimamie.

9. Kabla hujaingia kwenye ndoa, hakikisha unaweza kuyasimamia haya kama Mwanaume,
I. Kuongoza II. Kulinda III. Kuhudumia IV. Kumridhisha kingono(Sex).

Mwisho, never ever, usimsamehe mke ambaye ametoka nje ya ndoa (cheating wife), haijalishi ni mtamu kiasi gani. Never.

Kuwa mwanaume wa thamani.
 
1 na 2 zipo kifeminist sana ....mwanaume ishi ndoto zako mtu akija na kuondoka ni part ya mchezo so usiyumbishwe
 
Pia umesahau mwanaume unayetoka nje ya ndoa huitaji msamaha wa aina yoyote.

Pia tusisahau kuwatoa outing wapenzi wetu na kusafiri nao mara kwa mara kama tulivyokuq tunafanya kipindi tunatafuta kyuma zao
 
Nasema na wanaume kwa sababu nimesikitika kuona wanaume wakiwa wanarudia makosa yaleyale mara pale mahusiano au ndoa zao zinapovunjika na kujikuta wanapoteza muelekeo wa Maisha yao. Listen;

1. Mwanaume hutakiwi kurukia mahusiano mapya kabla hujaacha 100% yale yaliyopita. Ukisha achana nayo jipe muda wa kuwa single (mwenyewe), focus, tambua wapi ulikosea, rekebisha na ujitahidi uwe bora na imara.

2. Ndoa/Mahusiano sio mashindano. Usiingie haraka haraka ili tu kumuonyesha X wako kuwa unafanya vizuri kumzidi yeye. Hili ni kosa la karne, acha huu ujinga.

3. Pale utakapopata mwanamke, usikimbilie kumuoa au kumpa ujauzito. Kuweni wachumba walau miaka 2 kisha mlete kwako, akifika ishi nae tena walau mwaka na nusu ukiendelea kumjua tabia, kuijua historia yake vizuri zaidi, usiweke hatarini future yako kisa tu anakupa uchi muda unapotaka.

4. Ujue mzunguko wa hedhi wa mwanamke wako. Fahamu tarehe zake atakapokuwa period na uwe na elimu kuhusu tarehe hatari za mimba, pia kuwa na kumbukumbu ya siku unazolala nae. Acha kumwaga shahawa hovyohovyo (kumbuka, shahawa zikitoka mwilini mwako kuingia kwa mwanamke, huwa zinakuwa mali halali ya serikali).

5. Acha kutumia hela vibaya ili umuonyeshe X wako kuwa una hela, hii ni akili ya kimasikini.

6. Acha mazoea ya ovyo na mama mkwe, huyo sio ndugu yako. wakati wote atamtetea binti yake hata upeleke ushahidi wa namna gani. Hakikisha unatatua matatizo yako kwa kuwahusisha wanaume pekee. Baba mkwe, baba yako au ndugu wengine wa kiume, kushirikisha wanawake wataongeza tatizo.

7. Mwanaume hupaswi kuwa emotional attached na watoto wako. Utakapoanza kuongoza watoto wako kwa hisia, utaishia kuwapoteza, utashindwa kuwapa adhabu wanapokosea, utawanunulia wasivyohitaji n.k, na mwisho mama yao akishaona huo udhaifu, basi atawatumia watoto kukuadhibu. hadi utajuta.

8. Sunk Cost Fallacy ni jambo la hatari sana. Epukana nalo. Acha kuogopa kufanya maamuzi magumu kisa tu unahofia kupoteza vitu ulivyowekeza kwenye hayo mahusiano yako. Kuwa na msimamo, fanya maamuzi na uyasimamie.

9. Kabla hujaingia kwenye ndoa, hakikisha unaweza kuyasimamia haya kama Mwanaume,
I. Kuongoza II. Kulinda III. Kuhudumia IV. Kumridhisha kingono(Sex).

Mwisho, never ever, usimsamehe mke ambaye ametoka nje ya ndoa (cheating wife), haijalishi ni mtamu kiasi gani. Never.

Kuwa mwanaume wa thamani.
Binafsi sijaona mwanamke ambaye anaweza kutoa ushauri SAHIHI kuhusu ndoa.Maana hawatumii akili na logic.Unaweza kwenda kumuomba ushauri mwanamke kuhusu ndoa Yako akaishia kutetea makosa ya mke wako na kukufanya ujione mwenye makosa ni wewe ata kama unaonewa.

Simwamini mwanamke yeyote wote ni waongo na hawaeleweki.
 
Back
Top Bottom