Mambo usiyoyafahamu kuhusu Ngamia

Mambo usiyoyafahamu kuhusu Ngamia

Ngamia hunywa maji safi na ya chumvi. Anaweza hata kunywa maji kutoka Bahari ya Chumvi na hakuna kitakachoipata. Hii ni kwa sababu figo za ngamia huchuja maji: hutenganisha na chumvi na kugeuza kuwa maji safi yanayofaa kwa kunywa.

Ngamia pia hula miiba na haidhuru tumbo lake au utumbo wake kwa sababu mate yake huyeyusha miiba kama asidi.

Ngamia ana kope mbili: moja ni nyembamba na ya uwazi, nyingine nene na yenye nyama. Dhoruba ya mchanga inapoanza katika jangwa, hufunga kope lake la uwazi ili kuzuia mchanga usiingie machoni pake.

Ngamia pia anaweza kubadilisha joto la mwili wake: ikiwa ni baridi joto lake huongezeka, ikiwa ni moto katika jangwa la joto joto la mwili wake hupungua. Sifa alizo nazo mnyama huyu mzuri na wa kipekee ni za kuvutia.

Credit: Jr™ Creators!

Pia kuna dua maalum ya kumchinja, akisomewa yeye mwenyewe anageukia kibla tayari kwa kuchinjwa.
 
Ngamia ni haramu kabisa kwa mujibu wa Biblia. Ndiyo maana Wakristu na Wayahudi hawachomi ngamia wala kunywa maziwa yao

Walawi 11:4
Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.


Au wewe Mshana Jr unakunywa maziwa ya ngamia?
 
Ngamia huwezi kumfananisha na kinyonga unless hujui upekee wa uumbaji wa ngamia.
Point yangu ni kuwa kila Mnyama au ndege yuko unique.. kutokana na mazingira yake anayoishi.. hakuna mnyama mwenye upekee kwenye uumbaji..
 
Ngamia ni haramu kabisa kwa mujibu wa Biblia. Ndiyo maana Wakristu na Wayahudi hawachomi ngamia wala kunywa maziwa yao

Walawi 11:4
Pamoja na hayo, wanyama hawa hamtawala katika wale wenye kucheua, na katika wale walio na kwato; ngamia, kwa sababu yuacheua lakini hana kwato, yeye ni najisi kwenu.


Au wewe Mshana Jr unakunywa maziwa ya ngamia?
😀 Kinyungu ukiwa Roma ishi kama waroma
 
Huwa nasema watu wenye akili hawawezi kuongelea upuuzi kama evolution, hizo ni theories za watu wasio na maarifa ijapokuwa wanatajwa kwa heshima kama wameongea cha maana vile, eti hata twiga shingo zao zimerefuka kwasababu majani yaliisha chini ikabidi wayafuate juu, mxeww.
Uongo mtupu hii habari ya evolution
 
Back
Top Bottom