Kiukwel mie ni muhanga wa kusumbuliwa sana na hawa mashoga, ni wengi mnoo....
Ila kuna mmoja ana kampuni ya Tours (anapeleka wabongo nchi za nje) kwa kumuangalia ni mwanaume kabisa na tulianza mazoea kidogo kidogo mwishowe yakazidi.
Kuna wakati alisafiri kwenda USA na tulikuwa tunawasiliana mara kwa mara na wakat anarudi alininunulia simu Samsung S10+ wakati ndio zinatamba. Sasa wakati wa kuchati ikawa makopa kopa kwa sana ikabidi nimuulize babu vipi mbona sikuelewi pigo zako mwanangu. Ndio akaniambia ukweli kuwa ananipenda sana na yupo tayar kunifanyia chochote.....
Kiukwel nilichoka sana, sasa ndio akawa analazimisha nionane nae ila nikawa namgomea, kuna siku akawa anaandaa tour ya Dubai akaanza kunishawishi kuwa nimkubalie atanilipia kila kitu ili nikamgongee huko Dubai ila nikamkatalia, na ushahidi wa screenshot ninao ila nahofia kuweka humu maana nahisi jamaa na yeye atakuwepo JF.