Sijajua kuhusu agenda mkuu, pia sijasema kwamba basi gays wamekua wengi na straight wamepungua, hapana, ila nilichoeleza ni kwamba, watu hawa pia (gays) wameongezeka sana na wengi hawajionyeshi , hivyo nia yangu ni kujaribu kufahamisha tu watu wajue reality ya jambo husika ili wajue kudeal nalo, sababu ukijua jambo vizuri ni rahisi pia kulikabili kuliko ukiwa hujia inakuaje.
Kuhusu fantasy, sijajua mkuu, siwezi ongelea story ama maisha ya watu wwngine ila ukweli ni kuwa, wanasiasa pia ni watu, hao wenye hela pia ni watu, na hata wasiokua na hela pia ni watu, hivyo kama jambo hili la gays linawapata watu basi jua pia wapo watu wenye hela , wanasiasa, waheshimiwa, watu wa dini na hata wasio na dini ambao ni gays na wanadate hao hao ambao hawana kitu, ni kama ukahaba, kahaba hata atembee na mtu mwenye pesa, kama anahaja ya kumtumia tu hawezi mpa maisha mazuri zaidi ya kumpa pesa ya ukahaba, ndivyo ilivyo huko pia.
Kwa upande wangu i have my own life, with everything i needed to have. hivyo sidate na mtu sababu nataka maisha mazuri hapana, nadate na mtu sababu ya hisia nilizonazo na wala sizilazimishi.
Pia tusipende sana kuongelea mambo ya gays kutembea na watu hao maarufu na faida gani wanapata, sababu vijana wenye tamaa watajiingiza kwenye hayo mambo wakiamini watafaidika kumbe sio.
Ndege wafananao huruka pamoja, gaya wanakutana zaidi mitandaoni, hivyo yes hata hao wanaasiasa whatever wako huko online dating za gays, ila hitaweza kujua hadi mkutane sababu hua ni anonymous.
I hope umeelewa japo kiasi, mimi hia ai mzuri sana kuelezea.