Ndio maana nakwambia ujinga wa watanzania ndio hutumiwa na vyama vya siasa kuanzia chama tawala hadi upinzani, hao wanachama na mashabiki wa cdm kama wangekuwa huko kwa kuwa wanajielewa na wameshawishika na sera za cdm basi wasingekubali kuletewa Lowassa(kwa masilahi ya akina Mbowe) na wao wakashabikia kabisa na hadi leo wanaamini kwamba Lowassa ndio kaongeza idadi ya viti bungeni sijui ndio kafanya wapate kura nyingi zaidi.
Ni wazi ni ujinga wao tu unatumika basi, hakuna kizazi kipya cha mabadiliko wala nini na kingekuwepo ccm isingeweza kutumia hizo hela kuwalubuni.
Halafu kusema sijui watu waoga sio sahihi labda mtafute neno lengine, watu bado mnajaa wenyewe kwenye mikutano ya ccm bila kushikiwa bunduki na mnasema mnapelekewa na usafiri hadi eneo la tukio sasa hapo mnazungumzia uoga upi tena wakati watu bado wana mapenzi na chama na ujinga.
Hivi unafikiri kufeli kwa yale maandamano ya Mange na Lissu ni kwa sababu za uoga?