Mambo ya ajabu yamelighubika taifa letu. Umeme unakatika ovyo huku Waziri mwenye dhamana anadai kuna Megawatts 14000 za ziada

Kwanza alijinasibu kurekebisha miundo mbinu iliuochakaa ya kusafirisha umeme.

Sasa hivi anadai kuwa tuna ziada ya Mw 1400 na huku mgawo wa umeme upo kila siku.

Huyu Waziri ana wafanya Watanzania ni wapuuzi.
Kwani lini watanzania wamekuwa wamekuwa na akili??wangekuwa na akili wangeitoa CCM. Ujinga wa watz uko hapo.
 
Mkuu bado naona unazidi kuelezea hiyo nadharia ila bado sijaona cha kunishawishi kuona unachokieleza ndivyo kweli hali ilivyokuwa.

Huo ndio ukweli, ww kuridhika hilo sio kosa langu ni lako.
 
Una haki gani kwamba yeye hakuwa mpigaji?. Mtandao wa watu wake haukuwa ni wa malaika walikuwa ni wezi tu na kibaya zaidi wakajifunza hulka mbovu za uonevu na kutaka kunyenyekewa.
Habari za upigaji hazijawahi kudhibitishwa ni maneno matupu tu kama ngonjera😕

Hata kama alipiga lakini kulikuwa hakuna maumivu haya ya sasa basi waambie na wapigaji wa leo wapigie kwa akili.

period
 
Huo ndio ukweli, ww kuridhika hilo sio kosa langu ni lako.
Watu hutofautiana mitazamo ndio maana wengine wana mitazamo ya kwamba ccm bado inaendelea kuwa madarakani kwa sababu watanzania bado wajinga na ndio mtaji wa ccm watu bado wanaendelea kushabikia ccm hasa huko vijijini, ila wewe una mtazamo wa kwamba watanzania hawana tena ujinga na wameacha kushabikia ccm.
 
We ndio umejua leo kuwa Watz tumefanywa wapuuzi baada ya wakoloni kukabidhi nchi kwa TANU?

vumilia tu ndugu
Kwanza alijinasibu kurekebisha miundo mbinu iliuochakaa ya kusafirisha umeme.

Sasa hivi anadai kuwa tuna ziada ya Mw 1400 na huku mgawo wa umeme upo kila siku.

Huyu Waziri ana wafanya Watanzania ni wapuuzi.
 
Watu hutofautiana mitazamo ndio maana wengine wana mitazamo ya kwamba ccm bado inaendelea kuwa madarakani kwa sababu watanzania bado wajinga na ndio mtaji wa ccm watu bado wanaendelea kushabikia ccm hasa huko vijijini, ila wewe una mtazamo wa kwamba watanzania hawana tena ujinga na wameacha kushabikia ccm.

Watu huishabikia CCM wakati wa kampeni maana huingiziwa pesa za rushwa ili kuwahadaa. Kutokana na umasikini na ushawishi wa pesa, watu huweka shida zao pembeni kwa muda. Nenda baada ya kampeni uone madhila wanayokutana nayo kama kuna mtu anaitamani hiyo ccm.
 
Sasa hao ndio unaosema wewe kuwa ni kizazi kipya cha mabadiliko? Ni pesa kiasi gani wanacholipa ccm hadi kuweza kufanya watu kukubali kusahau matatizo ya huu utawala wa ccm na kukubali kutumika na ccm?
 
Kwani lazima walipwe walipwe wote? Wengine ni pombe za kienyeji tu wanapewa, na vitisho vya nguvu ya dola vya dola pia hutumika.
 
Ndio maana nakuuliza sasa hapo hicho kizazi kipya kiko wapi Kama mtu ukimpa pombe ya kienyeji tu inamtosha kukubali kutumika?

Hivyo vitisho ni kwamba wanalazimisha watu kwenda kwenye kampeni kwa hivyo hata wewe ukipewa hivyo vitisho utaenda kwenye kampeni za ccm?
 
Ukiona unalazimisha kutoa pesa ili ujenge ushawishi nje ya sera zako kuwa ushawishi, uju uko nje ya muda.

Huko vijijini ni rahisi kutoa vitisho na wakaogopwa. Lakini hata huku mjini unaweza kupewa vitisho vya kuhujumu eneo lako la kujiingizia kipato, na ikabidi ukubali ili kunusuru shughuli yako.
 
Hata chadema ililazimika kumchukua Lowassa akitokea ccm na tukaambiwa kwamba Lowassa ana ushawishi, sasa sijui waliona sera zao chadema hazikuwa na ushawishi au vp ila inajulikana Lowassa ana hela.

Muhimu hapa mkuu ni kwamba hakuna hicho kizazi cha mabadiliko unachokiongelea, watanzania wanaburuzwa na ccm pamoja na hao wapinzani.
 
Kumchukua Lowassa ulikuwa ujinga na tamaa za pesa za Mbowe na genge lake. CDM ilikuwa inakubalika bila kumuingiza huyo mzee tapeli wa kisiasa. Na tunaojitambua mpaka leo tunalaani blunder ile. Hii ndio maana nashikilia mpaka leo Mbowe aachie cheo cha mwenyekiti CDM.

Kizazi cha mabadiliko kipo, labda useme ni kizazi cha waoga. CCM kama chama haina cha kutambia, bali mbeleko ya vyombo vya dola ndio silaha yao. CCM nje ya vyombo vya dola ni bora TLP. Unapoona chama kina miaka 50+ lakini kinategemea udhaifu wa katiba kukaa madarakani kwa shuruti, ujue hamna chama hapo.
 
Ndio maana nakwambia ujinga wa watanzania ndio hutumiwa na vyama vya siasa kuanzia chama tawala hadi upinzani, hao wanachama na mashabiki wa cdm kama wangekuwa huko kwa kuwa wanajielewa na wameshawishika na sera za cdm basi wasingekubali kuletewa Lowassa(kwa masilahi ya akina Mbowe) na wao wakashabikia kabisa na hadi leo wanaamini kwamba Lowassa ndio kaongeza idadi ya viti bungeni sijui ndio kafanya wapate kura nyingi zaidi.
Ni wazi ni ujinga wao tu unatumika basi, hakuna kizazi kipya cha mabadiliko wala nini na kingekuwepo ccm isingeweza kutumia hizo hela kuwalubuni.

Halafu kusema sijui watu waoga sio sahihi labda mtafute neno lengine, watu bado mnajaa wenyewe kwenye mikutano ya ccm bila kushikiwa bunduki na mnasema mnapelekewa na usafiri hadi eneo la tukio sasa hapo mnazungumzia uoga upi tena wakati watu bado wana mapenzi na chama na ujinga.

Hivi unafikiri kufeli kwa yale maandamano ya Mange na Lissu ni kwa sababu za uoga?
 
Hiyo ya Lowassa kuwa aliongeza kura kila siku huwa napinga hapa maana ni uongo, aidha wa viongozi wa CDM kuficha kosa lao la kumpokea Lowassa. Ama ni upotoshaji wa wanaccm kutaka kuhadaa umma kuwa Cdm haikuwa na nguvu, bali ilitegemea nguvu ya Lowassa. Huwa ninawauliza wanaosema Lowassa alileta kura 6m+ na viti vingi vya ubunge na udiwani akiwa na miezi miwili, je alileta viti vingapi vya ubunge na udiwani akiwa na miaka miwili? Huwa nikifika hapo wote wanakaa kimya.

Narudia tena watu ni waoga hilo wala halina mjadala. Vitisho huwa tunaviona na sio jambo la siri. Watu kujaa kwenye mikutano ya CCM sio kwenda kusikiliza sera, bali wengi hufuata burudani, na shamrashamra zinazokuwepo kwenye mikutano ya CCM. Kama watu sio waoga, tusingeona wafanyakazi kutopandishiwa mishahara zaidi ya miaka 5, na kuishia kulalamika. Au huu mgao wa umeme na maji na watu wakawa wanalalamika tu. Labda kama una tafsiri tofauti ya uoga.

Hiyo watu kuwa waliogopa vitisho vya vyombo vya dola wala halina mjadala, labda kama utakwazika huu kuwa ndio ukweli. Tunakumbuka vitisho na magari ya vyombo vya usalama yalivyozunguka baada ya Mange kimambi na Tundu Lisu kutangaza maandamano. Labda kama tusingeona vyombo vya dola kisha watu wasiandamane ungekuwa na hoja.
 
Mwanza inahujumiwa kwa sababu ya MAGUFULI....serikali imeanza kubagua Kanda ya ziwa. Kupitia waziri wa nishati mwanza inakatiwa umeme kila siku kuanzia asubuhi Hadi jioni....hali hii inaelekea mwezi Sasa. January makamba punguza visasi....
 
Back
Top Bottom