Mambo ya kushangaza kuhusu kujamba

Mambo ya kushangaza kuhusu kujamba


Kwanini tunajamba? kwanini "ushuzi" unanuka? Kujamba inaweza kuwa kitendo cha aibu kwa wengi wetu,lakini inaweza kukufanya ujisikie vizuri kujua kwamba ni tendo la kawaida sana kwa mwili wa binadamu kutenda. Kila mtu anajamba,hata Sky Eclat nae hujamba.

1. Kujamba ni nini hasa?
Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa,ambayo inaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi. Baadhi ni hewa tuliyoimeza wakati wa kula au kunywa. Hewa ingine husababishwa na gesi kuingia kwenye utumbo wetu kutoka kwenye damu, na baadhi ya gesi huzalishwa na kemikali katika utumbo au bakteria.Kwa kawaida "ushuzi" unakua na asilimia 59 ya gesi ya nitrogen, asilimia 21 ni hydrogen, asilimia 9 ni carbon dioxide, asilimia 7 methane na asilimia 4 ni oygen.

Asilimia moja tu ya "ushuzi" inaweza kuwa hydrogen sulfide na mercaptans,ambayo ndio ina sulfur ndani yake,sulfur ndo hufanya "ushuzi" utoe harufu mbaya Kujamba huambatana na sauti,hii ni kutokana na "vibration" katika njia ya haja kubwa.Ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea "presha" inayosukuma gesi itoke nje na pia ugumu wa misuli ya njia ya haja kubwa.

2. Kwa nini Ushuzi hutoa Harufu mbaya?
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu, vyakula vyenye sulfur kwa wingi ndio husababisha hili. Vyakula vyenye sulfur kwa wingi ni kama maharage, kabichi, soda na mayai.

View attachment 1498819

3. Watu hujamba hadi mara 14 kwa siku
Mtu wa kawaida hutoa hata nusu lita ya ushuzi kwa siku 😂😂. Inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka 6,anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kutengeneza bomu la atomiki.😎

4. Ushuzi husafiri kwa mwendo wa futi 10 kwa sekunde
Harufu ya ushuzi huanza kusikika sekunde 10-15 baada ya mtu kujamba,hiyo ni kwa sababu inachukua muda mrefu kwa harufu kufikia pua. (Kwa mtu mnene kama Kiduku Lilo inaweza chukua hata nusu saa😂😂)

5. Kujizuia Kujamba Inaweza Kuhatarisha Afya Yako
Madaktari hawajakubaliana moja kwa moja kama kujizuia kujamba ni hatari kiafya.Baadhi ya wataalam wanafikiri kujamba ni sehemu muhimu katika mfumo wa mmeng'enyo wa chakula,hivyo kujizuia kujamba haitakuletea madhara.Wengine wanadhani kwamba kujizuia kujamba kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi, na pia inaweza sababisha kikundu(hemorrhoids).

View attachment 1498820

6. Kwa Baadhi ya Tamaduni, Kujamba Sio Ishu
Wakati tamaduni nyingi zikichukulia tendo la kujamba lifanywe kistaarabu, kuna baadhi ya tamaduni hawaoni haya kujamba hadharani, na pia hufurahia tendo hilo. Mfano kabila la Yanomami huko America ya Kusini,kwao husalimiana kwa kujamba,na China unaweza kupata kazi ya kunusa ushuzi! Katika Roma ya zamani, Mfalme Claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya, alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye "banquets".

Swali kwako.

Je, ulishawahi kujamba sehemu ambayo ukahisi hukustahil kufanya hivyo iwe kwa bahati mbaya au kukusudia?
Kikwetu kujamba ni aibu sana, huwezi Jamba mbele ya wakubwa, na mkubwa akijamba kwa kupitiwa huwa tunavuga kwa kupiga story nyingine hatakama kimetoa harufu kali vipi.
 
Kuna siku kiliponyoka ila uzuri nlikuwa na mshkaji,, jamaa akasema afya hiyo,,


Ila kuna jamaa yangu huwa hana aibu mkikaa wote wa kiume huwa anaachiaga tu,, na tushamzoea,, tunamchukulia poa tu
Hahahah huyo jamaa ni jasiri 🤣🤣🤣 pia nina mwanangu huyo naye tukiwa ghetto kwake yeye huvirusha tu...hawazi!
 
unajamba ukiona harufu kali unaanza kugeuka geuka nyuma km unamtafuta aliejamba kupoteza maboya.hahaha

wakati nipo form 6 kuna siku jioni tunatoka shule na jamaa yangu tukapanda daladala iliyokuwa inatoka shambani huko mule ndani kuna wazee tu wametoka shamba na kwakua ilikua kuna hali ya ka mvua vioo vilikua vimefungwa
basi bwana kufika mbele kidogo gari imechochea speed ilisikika harufu kali sana ya kijampo mimi na rafiki yangu tukaamua kufungua dirisha letu lakini wapi ,harufu ilidumu kama dakika 1 yule mzee sijui alikula nini
 
Back
Top Bottom