Mambo ya kuzingatia kabla hujasoma Biblia

Mambo ya kuzingatia kabla hujasoma Biblia

Kwanza Wakristo ndio wayahudi au waisrael na sio vinginevyo. Hawa tunaowaita waisrael (judaism) kimsingi ni wapagani kama walivyo watu wengine wasiommuamini Yesu.

Nasisitiza tena tafuta kujielimisha kwanza upate maarifa ya kutosha.

Kristo (Christ) linatokana na neno christos (greek word) lenye maana ya mpakwa mafuta ama masihi kiswahili yaani kwa jina jingine ndio Yesu.

Mkristo (christian) ni mtu anayemfuata Yesu yaani follower of Christ. Kwa maelezo hayo utaona myahudi (jew) ni mtu anayeishi kwa kufuata sheria ya Musa na hajawahi kumkubali Yesu na hivyo hawezi kuitwa mkristo.

Wale tu waliompokea Yesu na kufanyika kuwa wakristo ndio wanaoitwa wakristo, usichanganye mambo tafadhali.

Nasisitiza tena na tena, tafuta kujielimisha kwanza kabla ya kujaribu kuhubiri kitu usicho kielewa Mkuu.
 
1: Biblia sio kitabu cha kidini Sio kitabu cha kubishania, Ni maelezo ya Mungu mfalme aliyeumba sio tu dunia bali trillions za sayari zenye viumbe wasiohesabika. Hiyo lazima uyasome kwa adabu.

2: Usiende na ajenda yako mfukoni. Nenda kama mualikwa wa ikulu ya mbinguni kusikiliza hotuba na maelekezo ya mfalme wa wafalme. Hivyo sio kitabu cha wayahudi au wakristo ni cha kila mwanadamu.

3: Anza kwa maombi ili yeye aliyeandika akufunulie mistari itakayokusaidia wewe binafsi.

4: Maneno ya maandiko ni kama vifurushi vya nguvu, au kama zile namba za vocha ukiyaingiza moyoni yanabadilika kuwa nguvu au ujazo unaoleta athali chanya kwenye kila eneo la maisha yako. Soma ukiwa na mtazamo wa kupokea nguvu sio maelezo.

5: Amini kila neno aliloambiwa mtu yeyete katika biblia umeambiwa na wewe. Kila baraka zilizotamkwa ni zako pia. Kabla hujaanza kusoma biblia anza kujiepusha na watu wanaoiponda, mijadala isiyojengefu, watu wanaopenda mizaha na utani hata kama ni watumishi. Hii itakusaidia kuongeza umakini na kuwa na adabu kwa kauli za Mungu.

Ni hayo tu.

Kama umejifunza kitu, usisahau kucomment chochote.
Asante.
 
Mungu kaamua iwe hivyo.
Sio hilo tu kuna
Maombolezo ya nabii Yeremia.
Kitabu cha wafalme.
Ufunuo wa yogana na nyaraka kwa makanisa saba yaliyoko asia.

Lakini vyote vinatuhusu na sisi. Huo ndio mfumo ambao Mungu kaamua.
Kuna vitu vichache vinavyoweza kukugusa ukajifunza kitu lakini kiuhalisia ulikuwa ujumbe juu ya hayo makanisa saba, huwezi jua lifestyle zao kipindi hicho. Maelekezo unayoweza kumpa rubani hayamsaidii dereva wa gari, ni lazima utofautishe nyakati. Kwanini biblia ina vitabu vingi? Kwanini kisiwe kitabu kimoja kwa watu wote? Ni kwasababu waliandikiwa watu tofautitofauti na kwa nyakati tofautitofauti
 
Nasisitiza tena tafuta kujielimisha kwanza upate maarifa ya kutosha.

Kristo (Christ) linatokana na neno christos (greek word) lenye maana ya mpakwa mafuta ama masihi kiswahili yaani kwa jina jingine ndio Yesu.

Mkristo (christian) ni mtu anayemfuata Yesu yaani follower of Christ. Kwa maelezo hayo utaona myahudi (jew) ni mtu anayeishi kwa kufuata sheria ya Musa na hajawahi kumkubali Yesu na hivyo hawezi kuitwa mkristo.

Wale tu waliompokea Yesu na kufanyika kuwa wakristo ndio wanaoitwa wakristo, usichanganye mambo tafadhali.

Nasisitiza tena na tena, tafuta kujielimisha kwanza kabla ya kujaribu kuhubiri kitu usicho kielewa Mkuu.
Myahudi anasimama kama mrithi wa ahadi ya ibrahim. Iliyotoka kwa Ibrahim, ikaingia kwa Isaka, Akaipokea Yakobo (israel) na uzao wake ukiwemo ukoo ya Yuda (jews). Lakini ahadi hiyo ilikusudia kupitia Myahudi Yesu dunia zima tufanyike kuwa warithi wa hiyo ahadi.

Kila anayempokea Yesu anafanyika mzao wa ibrahim na mrithi. Sio mrithi wa kibaiolojia ni mrithi wa imani. Ndio maana ni ushamba kuwahusisha wayahudi wasiompokea Yesu na mambo ya Ibrahim na urithi wa ahadi. Najadili kwa mtazamo wa ahadi kwanza.
👇👇👇👇👇👇
Wagalatia 3:29
Na kama ninyi ni wa Kristo, basi, mmekuwa uzao wa Ibrahimu, na warithi sawasawa na ahadi.
 
Mungu ananjia nyingi za kufikia watu hasa wa dunia hii yenye iq ndogo kabisa iliyodunishwa na dhambi. Alitumia watu kuwapa ujumbe kwa lugha ya kawaida kabisa ili tuelewe.
Tusimpangie Mungu eti kila kitu aje aseme moja kwa moja. Tumuache atumie hekima zake kutusaidia.
Kwa nini asije moja kwa moja?

Dhana ya Mungu imeletwa na mwanadamu unakubali?
 
Uzinzi ulianza lini?
Maana Maandiko yanasema wakati wa Ibrahim sheria amri na maagizo ya Mungu yalikuwepo. Inaonekana unamaarifa ya upande mmoja.

Kwa sababu Ibrahimu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu. Mwanzo 26:5

Pia ukumbuke dhambi ni uasi wa sheria za Mungu. Vinginevyo watu wa sodoma, watu wa kizazi cha Nuhu, Kaini kumuua Habiri wasingehesabiwa kosa maana hakukuwa na sheria.

Tumuelewe Mungu kwa mapana.

Usichanganye neno DHAMBI na UOVU.

Labda nikuulize unasoma biblia zipi (kwa maana ya lugha)?

Maana naona hata the way unatafsiri mambo na maandiko unayotumia kusupport marlezo yako yana mkanganyiko wa matumizi ya lugha.
Hilo neno sheria kama linavyotumika kwenye mwanzo 26:5 si neno sheria kama linalotumika kwenye mfano kitabu cha kutoka na kuendelea likimaanisha torati.

Soma biblia ya kiebrania utaona ni vitu viwili tofauti.

Kuhusu kuzaliwa kwa dhambi soma hapa:

Romans 7
7. What shall we say then? Is the law sin? God forbid. Nay, I had not known sin, but by the law: for I had not known lust, except the law had said, Thou shalt not covet.
Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
8. But sin, taking occasion by the commandment, wrought in me all manner of concupiscence. For without the law sin was dead.
Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
9. For I was alive without the law once: but when the commandment came, sin revived, and I died.
Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.
 
Ibrahim aliishi kabla ya sheria hivyo hakuna namna utasema alitenda dhambi. Biblia inasema sheria ndiyo huzaa dhambi na dhambi huzaa mauti, na kabla ya sheria mtu hakuhesabiwa dhambi. Soma warumi 5:13 na yakobo 1:14.
Huu ni uongo na uache kudanganya watu, Hakuna kiumbe kilichoishi kabla ya sheria, Ibrahim alihesabiwa dhambi kama mwanadamu mwingine.

Sheria ilikuepo kabla hata ya ulimwengu kuumbwa, Sheria ya mungu ilikuwepo kabla hata ya mwanadamu kuumbwa, na sheria za mungu zina apply kote mbinguni na duniani.

Sasa nina swali kwako, kama sheria haikuwepo lucifer alihesabiwaje dhambi baada ya kuanzisha ugomvi wa kupinga mamlaka ya yesu mbinguni?
Kama sheria haikuwepo Adam alihesabiwaje dhambi pale Eden??
 
Kuna vitu vichache vinavyoweza kukugusa ukajifunza kitu lakini kiuhalisia ulikuwa ujumbe juu ya hayo makanisa saba, huwezi jua lifestyle zao kipindi hicho. Maelekezo unayoweza kumpa rubani hayamsaidii dereva wa gari, ni lazima utofautishe nyakati. Kwanini biblia ina vitabu vingi? Kwanini kisiwe kitabu kimoja kwa watu wote? Ni kwasababu waliandikiwa watu tofautitofauti na kwa nyakati tofautitofauti
Unaposoma maandiko. Kwanza unasoma kwa mtazamo wa wahusika wa awali, ukiishia hapo kwamba maelekezo ni kwa pilot na sio deleva. Utakuwa umemiss lengo. Spiritual application.
Ndio maana hata dalili kaz kuja kwa Yesu mathayo24 utaona kama hazihusu kuja kwa Yesu karibu zote zinahusu kuvamiwa kwa Yerusalem Mwaka 70AD.

Ila zote zinatuhusu na sisi.

Kwenye biblia lazima ujue juna

1principles. Hizi hazibadiliki zinafqa kwa pilot wa ndege na kwa dereva wa guta.

2patterns
3parallels
4prophesies
5promises
e.t.c

Ukisoma kwa mtazamo huu mpana utagundua kila kitu kinakuhusu. Ndio maana biblia ni kitabu cha kiroho sio cha taaluma. Ndio maana wote wanaoisoma kitaaluma au kitaalimungu wanaishia kuwa atheists.
 
Usichanganye neno DHAMBI na UOVU.

Labda nikuulize unasoma biblia zipi (kwa maana ya lugha)?

Maana naona hata the way unatafsiri mambo na maandiko unayotumia kusupport marlezo yako yana mkanganyiko wa matumizi ya lugha.
Hilo neno sheria kama linavyotumika kwenye mwanzo 26:5 si neno sheria kama linalotumika kwenye mfano kitabu cha kutoka na kuendelea likimaanisha torati.

Soma biblia ya kiebrania utaona ni vitu viwili tofauti.

Kuhusu kuzaliwa kwa dhambi soma hapa:

Romans 7
7. What shall we say then? Is the law sin? God forbid. Nay, I had not known sin, but by the law: for I had not known lust, except the law had said, Thou shalt not covet.
Tusemeje, basi? Torati ni dhambi? Hasha! Walakini singalitambua dhambi ila kwa sheria; kwa kuwa singalijua kutamani, kama torati isingalisema, Usitamani.
8. But sin, taking occasion by the commandment, wrought in me all manner of concupiscence. For without the law sin was dead.
Lakini dhambi ilipata nafasi kwa ile amri, ikafanya ndani yangu kila namna ya kutamani. Kwa maana dhambi bila sheria imekufa.
9. For I was alive without the law once: but when the commandment came, sin revived, and I died.
Nami nalikuwa hai hapo kwanza bila sheria; ila ilipokuja ile amri, dhambi ilihuika, nami nikafa.
Biblia inatambua
Dhambi
Makosa
Na Uovu.

Inasema Mungu anasameme Dhambi, Makosa, na uovu.

Naomba unitofautishie kimaandiko.

Kumbuka vyote chanzo chake ni anguko eden
 
Huu ni uongo na uache kudanganya watu, Hakuna kiumbe kilichoishi kabla ya sheria, Ibrahim alihesabiwa dhambi kama mwanadamu mwingine.

Unaelewa lakini kinacho jadiliwa? Hapo ulipo nukuu nazungumzia sheria ya Musa ambayo ndiyo biblia inasema ilizaa dhambi.

Sasa ukisoma biblia utaona kutoka kufa kwa Ibrahim hadi kuzaliwa kwa Musa ni kipindi kirefu kilipita, ninaposema Ibrahim aliishi kabla ya sheria namaanisha sheria ya Musa (torati).
 
Kwa nini asije moja kwa moja?

Dhana ya Mungu imeletwa na mwanadamu unakubali?
Huwezi kumpangia.
Dhana ya Mungu kuletwa na mwanadamu ni utunzi wa wanadamu wenye frustration za kumkimbia Mungu.
 
Unaelewa lakini kinacho jadiliwa? Hapo ulipo nukuu nazungumzia sheria ya Musa ambayo ndiyo biblia inasema ilizaa dhambi.

Sasa ukisoma biblia utaona kutoka kufa kwa Ibrahim hadi kuzaliwa kwa Musa ni kipindi kirefu kilipita, ninaposema Ibrahim aliishi kabla ya sheria namaanisha sheria ya Musa (torati).
Wagalatia 3:19
Sheria iliingizwa kwa sababu ya makosa.

Makosa yalianzia wakati wa Musa au Adamu? Makosa yamesisha au hayajaisha?
 
Kwa maana nyingine kuna kitu cha kujifunza. Maana yameandikwa ili kutufundisha sisi.

Ndio maana Ibrahim alizini kwa kukoswa uvumilivu. Sisi tunajifunza kuvumilia maana Mungu sio muongo.

Kikubwa kujua application. Maana kila lilioandikwa linaaplication yake kwa kila mtu.
Kama Ibrahim baba wa imani Duniani alishindwa kuvumilia, sisi ambao hatujafikia hata kuitwa watoto wa I
Imani tuvumilie ili iweje?!😡😡
 
Biblia inatambua
Dhambi
Makosa
Na Uovu.

Mkuu ili twende sawa, niandikie unataka nikutofautishie kutoka kwenye mstari gani wa biblia?

Mfano, niambie nipe tofauti ya dhambi km ilivyo tumika katika andiko fulani na neno makosa kama lilivyo tumika kwenye andiko hili na pia neno uovu kama lilivyo tumika kwny andiko fulani.

Toafauti na hapo tutakuwa tunajadili lugha na si maneno yaliyo tumika kwa muktafha wa biblia. Ukisoma baadhi ya version unaweza kukuta maneno dhambi, makosa na uovu yanatumika interchangeably lakini ukisoma original version ya kiebrania (kwa agano la kale) na kigiriki (kwa vitabu vinavyoitwa vya agano jipya) unakuta maana ni tofauti.
 
Kitabu ambacho kilishindwa hata kuelezea umbo halisi la dunia cha kazi gani sasa.
Kama ni cha kazi gani, hapa unafanya nini?

You seem useless for having nothing to do
 
Unaelewa lakini kinacho jadiliwa? Hapo ulipo nukuu nazungumzia sheria ya Musa ambayo ndiyo biblia inasema ilizaa dhambi.

Sasa ukisoma biblia utaona kutoka kufa kwa Ibrahim hadi kuzaliwa kwa Musa ni kipindi kirefu kilipita, ninaposema Ibrahim aliishi kabla ya sheria namaanisha sheria ya Musa (torati).
Sasa hapohapo ndo unapokosea, torati kwa lugha nyingine "Sheria" ilikuwepo wakati wa Ibrahim na kabla hata ya Ibrahim, torati ya musa ilikuwa "Amri za Mungu" ambazo ilikuwepo kabla hata binadamu hajaumbwa na baadhi ya sheria ndogondogo zilikuwa zinawahusu ile jamii ya waisraeli, ambazo waliziita "Sheria za musa" hizi sheria musa aliziweka ili ziwasaidie katika maisha ya kila siku lakini zilikuwa parallel na sheria za mungu.

Kipindi cha mussa sheria ya mungu "Torati" ndo iliandikwa kweny jiwe ila kabla ya hapo watu walikuwa wanazijua sheria za Mungu.
 
Wagalatia 3:19
Sheria iliingizwa kwa sababu ya makosa.

Makosa yalianzia wakati wa Musa au Adamu? Makosa yamesisha au hayajaisha?

Ukisoma biblia ya KJV utaona neno ambalo linatafsiriwa kama “makosa” ni neno “transgressions” ambalo kiswahili kizuri ingeweza kuwa kukosa utii. Hii ni baada ya wana wa Israel kukosa kutii maagizo ya Musa anayowapa toka kwa Mungu ndipo Mungu akampatia Musa sheria itayo waongoza hadi kuja kwa Kristo.

Ndio utaona sheria inakuja na kutoa miongozo kuwa ukifanya hivi utakuwa umetenda dhambi na adhabu yake ni hii, ndipo inapokuja dhana ya sheria huzaa dhambi na dhambi huzaa mauti.

Kipindi cha Adam pamoja na shetani makosa yao biblia ya KJV inayataja kama iniquity/treason ama uovu au uasi na hata adhabu zao zinafanana; wanafukuzwa kutoka katika uwepo wa Mungu (presence of God).
 
Sasa hapohapo ndo unapokosea, torati kwa lugha nyingine "Sheria" ilikuwepo wakati wa Ibrahim na kabla hata ya Ibrahim, torati ya musa ilikuwa "Amri za Mungu" ambazo ilikuwepo kabla hata binadamu hajaumbwa na baadhi ya sheria ndogondogo zilikuwa zinawahusu ile jamii ya waisraeli, ambazo waliziita "Sheria za musa" hizi sheria musa aliziweka ili ziwasaidie katika maisha ya kila siku lakini zilikuwa parallel na sheria za mungu.

Kipindi cha mussa sheria ya mungu "Torati" ndo iliandikwa kweny jiwe ila kabla ya hapo watu walikuwa wanazijua sheria za Mungu.

Nimemuuliza pia huko juu mkuu matunduizi, nawe nitakuuliza pia unasoma biblia za lugha ngapi? Kutokana na tafsiri ya versions mbalimbali kuna maneno yanatumika interchangeably lakini hayana maana sawa.

Bible scolars wanatumia biblia za kiebrania na kigiriki kupata maana halisi ya neno lililo kusudiwa wakati wa uandishi wa biblia ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kutokana na tafsiri ya biblia kwenda kwenye lugha mbalimbali.

Ndio maana ni muhimu sana kufundishwa namna ya kuisoma biblia na wenye ufahamu sahihi kabla ya kuanza kuitafsiri kwa muktafha wa lugha tu.
 
Back
Top Bottom