Mambo ya kuzingatia kabla hujasoma Biblia

Mambo ya kuzingatia kabla hujasoma Biblia

Nimemuuliza pia huko juu mkuu matunduizi, nawe nitakuuliza pia unasoma biblia za lugha ngapi? Kutokana na tafsiri ya versions mbalimbali kuna maneno yanatumika interchangeably lakini hayana maana sawa.

Bible scolars wanatumia biblia za kiebrania na kigiriki kupata maana halisi ya neno lililo kusudiwa wakati wa uandishi wa biblia ili kuondoa mkanganyiko unaojitokeza kutokana na tafsiri ya biblia kwenda kwenye lugha mbalimbali.

Ndio maana ni muhimu sana kufundishwa namna ya kuisoma biblia na wenye ufahamu sahihi kabla ya kuanza kuitafsiri kwa muktafha wa lugha tu.
Naelewa hilo swala ndugu wala usijali.

Swala tunalozungumzia linaeleweka vizur tuu, wala usianze kuleta sababu za kwamba biblia imepitia tasfiri za lugha nyingi, tunazungumzia sheria, sio jambo la kuchanganya sana hadi tutafute biblia ya kiebrania.
 
1: Biblia sio kitabu cha kidini Sio kitabu cha kubishania, Ni maelezo ya Mungu mfalme aliyeumba sio tu dunia bali trillions za sayari zenye viumbe wasiohesabika. Hiyo lazima uyasome kwa adabu.

2: Usiende na ajenda yako mfukoni. Nenda kama mualikwa wa ikulu ya mbinguni kusikiliza hotuba na maelekezo ya mfalme wa wafalme. Hivyo sio kitabu cha wayahudi au wakristo ni cha kila mwanadamu.

3: Anza kwa maombi ili yeye aliyeandika akufunulie mistari itakayokusaidia wewe binafsi.

4: Maneno ya maandiko ni kama vifurushi vya nguvu, au kama zile namba za vocha ukiyaingiza moyoni yanabadilika kuwa nguvu au ujazo unaoleta athali chanya kwenye kila eneo la maisha yako. Soma ukiwa na mtazamo wa kupokea nguvu sio maelezo.

5: Amini kila neno aliloambiwa mtu yeyete katika biblia umeambiwa na wewe. Kila baraka zilizotamkwa ni zako pia. Kabla hujaanza kusoma biblia anza kujiepusha na watu wanaoiponda, mijadala isiyojengefu, watu wanaopenda mizaha na utani hata kama ni watumishi. Hii itakusaidia kuongeza umakini na kuwa na adabu kwa kauli za Mungu.

Ni hayo tu.

Kama umejifunza kitu, usisahau kucomment chochote.
Uko sahihi kabisa. Biblia si kitabu cha rejea (reference book) bali ni Mungu anasema nasi, sisi tunasema naye kwa maombi. Na kwa kusema hivyo Biblia haimo miongoni mwa vitabu vya kidini vilivyotungwa na wanadamu, bali ni neno la Mungu lililoandikwa kwa kuwatumia wanadamu kadri walivyoongozwa na Roho Mtakatifu.

Aidha, kumfuata Yesu si kufuata dini ya kikristo maana Yesu mwenyewe si dini, bali mkombozi wa watu wote, wawe na dini zao au bila dini.
 
Kama ni cha kazi gani, hapa unafanya nini?

You seem useless for having nothing to do
Kuwasaidia ninyi muamke, kitabu kinachanganya chenyewe mstari baada ya mstari.

Acheni kumdharaulisha Creator (Mungu) kwa kumhusisha na hicho kitabu ya hekaya.

Creator aliyehusika na huu ulimwengu hawezi kuandaa kitabu kibovu kama kile...
 
Kitabu ambacho kilishindwa hata kuelezea umbo halisi la dunia cha kazi gani sasa.

Wakatoliki wakaamua kumuua mwanasayansi wa watu bure kisa tu alisema dunia ina umbo la tufe...
Biblia tayari ilishasems dunia ni duara kabla ya Wakatoliki. Soma Isaya 40:22
Usifuate wanachosema watu wa dini, fuata inachosems Biblia.
 
Mi naomba kuelimishwa kidogo ukisoma mathayo anaelezea ukoo wa yesu utaona kutoka ibrahimu mpaka yakobo aliyemzaa yusufu (baba yake yesu) katika vizazi kumi na nne sasa hoja na swali langu lipo hapa Kama tunaambiwa yesu alitokana na roho mtakatifu maana kigenetically hayupo kwa yusuph sasa ameingiaje kwenye ukoo wa yuda(Jews) mwenye kujua anielimishe kidogo

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app
 
Babaye wa damu ni Mungu. Yusufu ni baba mlezi.

Ukimuasili mtoto anakuwa wako Kisheria. Anakuwa na haki ya kutumia jina lako na la ukoo wako kama watoto wako wa kuwazaa walivyo na haki hiyo.
 
Naelewa hilo swala ndugu wala usijali.

Swala tunalozungumzia linaeleweka vizur tuu, wala usianze kuleta sababu za kwamba biblia imepitia tasfiri za lugha nyingi, tunazungumzia sheria, sio jambo la kuchanganya sana hadi tutafute biblia ya kiebrania.

Ukisoma kitabu cha mwanzo utaona Kaini alimuua ndugu yake Abeli na Mungu anailaani ardhi kwa ajili yake, lkn baadaye Kaini anarudi na kumlilia Mungu kwamba adhabu ile haichukuliki na Mungu anamuwekea chapa na kusema yeyote ataye muua Kaini kisasi changu kitakuwa juu yake. Hapa unaona neema ikitenda kazi katika kitabu cha mwanzo kabla hata ya ujio wa Yesu.

Lakini katika kitabu cha walawi ukisoma baada ya ujio wa sheria ya Musa biblia inasema;
Walawi 24
17. Na mtu ampigaye mtu hata akafa, lazima atauawa.

Utaona hivi ni vipindi viwili jambo moja linakuwa na hukumu tofauti kwa nini? Je, hapakuwa na amri/sheria za Mungu?

Tofauti na torati ya Musa ilikuwa hakuna cha kuomba msamaha, umefanya hiki na sheria inasema hivi basi unatendewa yakupasayo.

Sasa neno “sheria” linavotumika kwenye hivi vitabu viwili ni tofauti ukisoma kwenye biblia ya kiebrania na hata tafsiri zake ni tofauti, ndiyo maana nikajibu hivo sikuwa na maana ya ‘kujifichia’ huko eti kwa kuwa watu wengi hawasomi hizo biblia.
 
Galileo Galilei aliongozwa na Biblia kuchunguza anga na kugundua dunia ni duara. Kwanza katika kitabu cha Isaya kuna mstari unazunguzmia uduara wa dunia.

Wakatoliki dini yao ilikuwa chini ya influence kubwa ya greek mythology sio Biblia. Nadharia za misiolojia za kigiriki zilikuwa backbone ya upinzani wao kwa Galilei. Maana ilionekana anabishana na wasomi ambao kanisa liliwaamini.

Ila alishaombwa msamaha na wakatoliki miaka ya 90 kuwa walikosea kumuhukumu msomi Galileo.
Mstari huo ni Isaya 40:22
 
Waandishi wote wameweka room kwa ajili ya criticism. ILA biblia kufanya hivyo ni blasphemy( Kufuru)

Ni kitabu chenye mikanganyiko mingi sana.
 
Huwezi kumpangia.
Dhana ya Mungu kuletwa na mwanadamu ni utunzi wa wanadamu wenye frustration za kumkimbia Mungu.
Simpangii kitu wala sina uwezo huo, ila swali langu sidhani kama umejibu.

Labda nibadili, dhana ya uwepo wa Mungu mmoja ilianzia wapi? Na nani ni mwanzilishi wake hapa duniani?
 
Ukisoma kitabu cha mwanzo utaona Kaini alimuua ndugu yake Abeli na Mungu anailaani ardhi kwa ajili yake, lkn baadaye Kaini anarudi na kumlilia Mungu kwamba adhabu ile haichukuliki na Mungu anamuwekea chapa na kusema yeyote ataye muua Kaini kisasi changu kitakuwa juu yake. Hapa unaona neema ikitenda kazi katika kitabu cha mwanzo kabla hata ya ujio wa Yesu.
Ardhi haikulaaniwa kwasababu ya kaini, soma tena kaka, ardhi ilibeba laana ya Adam baada ya kutenda dhambi.
Lakini katika kitabu cha walawi ukisoma baada ya ujio wa sheria ya Musa biblia inasema;
Walawi 24
17. Na mtu ampigaye mtu hata akafa, lazima atauawa.

Utaona hivi ni vipindi viwili jambo moja linakuwa na hukumu tofauti kwa nini? Je, hapakuwa na amri/sheria za Mungu?

Tofauti na torati ya Musa ilikuwa hakuna cha kuomba msamaha, umefanya hiki na sheria inasema hivi basi unatendewa yakupasayo.
Brother sheria ya mungu ni ileile haibadiliki, Dhambi inazaa mauti, hamna utafouti wa sheria wowote ninao uona hapo.
Mungu anapoamua kumwacha kaini aende zake hamaanishi amemsamehe(maana hakuomba msamaha) au amesahau, ni huruma tuu sometimes, but Mark words inawezekana dhambi isikudhuru wewe directly but ikadhuru watoto/uzao wako. Kuna Msamaha na kuna athari za dhambi, ni vitu viwili tofauti, unaweza samehewa dhambi zako but athari ya zile dhambi bado zikakuandama na hichi ndicho kilichomtokea kaini na wengine wengi.

Na unaposema kipindi cha musa kulikuwa hakuna msamaha unajidanganya brother kwasababu hata wakina Daudi walikuwa wanaishi kipindi cha torati ya musa, torati ya musa ndo ilikuwa msingi wa Imani yao hata kipindi cha akina Hezekia.
Sasa je kama kulikuwa hakuna msamaha kipindi cha torati, mbona daudi alisamehewa makosa yake baada ya kumuua mtu asiye na hatia?
Just think brother, Lucifer mwenyew alikuwa na dirisha la kuomba msamaha sembuse binadamu walioishi kipindi cha mussa? Na zile dhabihu walizokuwa wanatoa kwaajili kuomba msamaha zilikuwa za maana gani kama kulikuwa hakuna msamaha?
 
Ardhi haikulaaniwa kwasababu ya kaini, soma tena kaka, ardhi ilibeba laana ya Adam baada ya kutenda dhambi.

Genesis 4
11. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12. utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.

Brother sheria ya mungu ni ileile haibadiliki, Dhambi inazaa mauti, hamna utafouti wa sheria wowote ninao uona hapo.

Adam aliambiwa akila matunda ya mti wa katikati atakufa, lakini biblia inatuambia aliishi zaidi ya miaka 900 (mwanzo 5:5). Huku katika sheria ya Musa ilikuwa nawe unauwawa baada ya mashahidi wawili au zaidi kuthibitisha.

Mungu anapoamua kumwacha kaini aende zake hamaanishi amemsamehe(maana hakuomba msamaha) au amesahau, ni huruma tuu sometimes, but Mark words inawezekana dhambi isikudhuru wewe directly but ikadhuru watoto/uzao wako. Kuna Msamaha na kuna athari za dhambi, ni vitu viwili tofauti, unaweza samehewa dhambi zako but athari ya zile dhambi bado zikakuandama na hichi ndicho kilichomtokea kaini na wengine wengi.
1. Mungu si kigeugeu, akisamehe anasamehe jumla. Unaposema ni “huruma tuu unamaanisha nini?”

2. Wapi biblia inasema uzao wa Kaini umeadhibiwa? Au unazungumzia hisia tuu?

Mungu anaposema atapatiliza hadi kizazi cha nne kwa dhambi yako, anatoa nafasi ya kutubu kwa vizazi vinne pia mbele.

Na unaposema kipindi cha musa kulikuwa hakuna msamaha unajidanganya brother kwasababu hata wakina Daudi walikuwa wanaishi kipindi cha torati ya musa, torati ya musa ndo ilikuwa msingi wa Imani yao hata kipindi cha akina Hezekia.
Sasa je kama kulikuwa hakuna msamaha kipindi cha torati, mbona daudi alisamehewa makosa yake baada ya kumuua mtu asiye na hatia?

Ukisoma utaona hizi personalities tatu i.e Wafalme, Manabii na Makuhani walikuwa responsible kwa Mungu pekee na ndio waliokuwa wanasimamia uendeshaji wa mashauri yote. Ni utaratibu huu umerithiwa hata leo majaji wanakuwa na immunity ya kutoshitakiwa.

Hata Musa alioa mwanamke mkushi kinyume na amri ya Mungu lkn Haruni na Miriam walipojaribu kumuhoji Mungu aliwashukia na kuwaonya na Miriam alipigwa ukoma kwa sababu hiyo na huyo alikuwa nabii mke.

Just think brother, Lucifer mwenyew alikuwa na dirisha la kuomba msamaha sembuse binadamu walioishi kipindi cha mussa? Na zile dhabihu walizokuwa wanatoa kwaajili kuomba msamaha zilikuwa za maana gani kama kulikuwa hakuna msamaha?

1. Una ushahidi wa maandiko kwamba shetani alikuwa na chance ya kuomba msamaha au again ni hisia zako tu?

2. Dhabihu zilizokuwa zikitolewa kwenye sheria ya Musa ilikuwa ni za upatanisho (atornment), again from hebrew bible atotnment means just covering, meaning that sins are still there, wakati wakisubiri ujio wa Kristo ambaye baada ya ujio wake biblia inasema ni remission (complete take away) once and for all (romans 3:25 Romans 3
25. Whom God hath set forth to be a propitiation through faith in his blood, to declare his righteousness for the remission of sins that are past, through the forbearance of God.

Finally ukileta hoja nipe na scriptures otherwise sitakujibu sabab unanichosha kujibu hisia zako.
 
Kwa nini ufanye hivyo? Nini kinakusukuma? Sisi ni nani zako hadi kulala kwetu iwe tatizo kwako?
Anyway, take it easy...

Kumradhi kama umekwazika. Nilikuwa natoa maoni kulingana na kile ninachokiamini.
 
Mi naomba kuelimishwa kidogo ukisoma mathayo anaelezea ukoo wa yesu utaona kutoka ibrahimu mpaka yakobo aliyemzaa yusufu (baba yake yesu) katika vizazi kumi na nne sasa hoja na swali langu lipo hapa Kama tunaambiwa yesu alitokana na roho mtakatifu maana kigenetically hayupo kwa yusuph sasa ameingiaje kwenye ukoo wa yuda(Jews) mwenye kujua anielimishe kidogo

Sent from my TECNO KG5j using JamiiForums mobile app

Kipindi cha Yesu (sina hakika kwa sasa) kama utaratibu bado uko hivo, mtu alihesabiwa ya kuwa ni myahudi ikiwa amezaliwa na mzazi ambaye ni myahudi (Mariam), lakini pia mtu alihesabiwa kuwa myahudi kwa kubadili imani na kuwa myahudi. Mfano; Rahab pia hakuwa myahudi kwa asili lakini aliingia kwenye ukoo wa wana wa israel kwa viapo walivyo wekeana na wale wapelelezi.

Pia katika hicho kitabu cha mathayo kinataja ukoo wa Yesu na utaona inakuja hadi kwa Ibrahimu ambaye baadaye anazaliwa Mfalme Daudi ambaye biblia inamtaja Yesu kama mwana wa Daudi.

Yesu mwenyewe anasema ya kuwa yeye ni myahudi wakati akiongea na mwanamke msamaria kisimani (yoh 4: 22)

Yesu amezaliwa katika mji wa Daud, bethlehem ya uyahudi, akalelewa kwa taratibu za kiyahudi, akaziishi sheria za kiyahudi na hata kifo chake alishitakiwa kwa makosa yaliyo husiana na kuvunja sheria za kiyahudi.

Naamini kwa kifupi nimekujibu japo upo uthibitisho mwingi wa biblia kuwa Yesu alikuwa myahudi.
 
Back
Top Bottom