Mambo ya kuzingatia kabla hujasoma Biblia

Uko sahihi. Hata Yoabu, mkuu wa Jeshi la Israeli kipindi cha utawala wa Mfalme Daudi, babaye alikuwa ni Mmisri lakini mama yake alikuwa ni dada yake Daudi ambaye alikuwa ni Myahudi. Utaona kuwa japo bavaye alikuwa Mmisri, Yoabu alihesabiwa kuwa ni Myahudi. Ndiyo maana Daudi aliweza kumteua kuwa mkuu wa majeshi.
 

Asante kwa kuongezea mkuu [emoji120][emoji120]
 
Genesis 4
11. Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12. utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
Unajiabisha brother, umeleta mafungu yanayokuumbua, hapa mungu kabisa anasema anamlaaniwa mtu na sio ardhi.

Haya Unadhani sijui Scriptures 😅 😅 😅
Mwanzo 3:17
[17]Akamwambia Adamu, Kwa kuwa umeisikiliza sauti ya mke wako, ukala matunda ya mti ambao nalikuagiza, nikisema, Usiyale; ardhi imelaaniwa kwa ajili yako; kwa uchungu utakula mazao yake siku zote za maisha yako.
And unto Adam he said, Because thou hast hearkened unto the voice of thy wife, and hast eaten of the tree, of which I commanded thee, saying, Thou shalt not eat of it: cursed is the ground for thy sake; in sorrow shalt thou eat of it all the days of thy life.

Adam aliambiwa akila matunda ya mti wa katikati atakufa, lakini biblia inatuambia aliishi zaidi ya miaka 900 (mwanzo 5:5)
Brother Adam hakufa??
Mungu alimwambia "Hakika utakufa" na Adam alikufa hata kama aliishi miaka 900 mwisho wa siku ahadi ya mungu ilitimia.
Mwanzo 2:17
[17]walakini matunda ya mti wa ujuzi wa mema na mabaya usile, kwa maana siku utakapokula matunda ya mti huo
utakufa hakika.
But of the tree of the knowledge of good and evil, thou shalt not eat of it: for in the day that thou eatest thereof thou shalt
surely die.
Mungu aliposema "Hakika mtakufa" hakumaanisha Adam atakufa papohapo atakapo tenda dhambi, alimaanisha hamta ishi milele, kifo kitakuwa part ya maisha yenu. Je hii haikutimia? Adam aliishi milele??
Mungu alimuumba binadamu kuishi milele, dhambi ndo imetuletea mauti, Adam alipotenda dhambi ilibidi afe, but mungu mwingi wa huruma alikuwa tayar ameshaweka mpango wa kumkomboa Adam, na mpango wenyew ni kafara, "Hakuna Ondolea la dhambi bila damu kumwagika", baada Adam kuanguka dhambini, dhabihu za kafara adam alizokuwa akimtolea mungu ndizo zilizokuwa zinamfanya aendelee kuishi[mwanzo 3;21] maana yake nn? Maana yake yule kondoo dume asiye na ulemavu alikuwa akifa badala ya Adam, huyo kondoo wote tunajua kwamba alikuwa anam-represent yesu, mwana-kondoo aliyechinjwa tangu tangu kuwekwa misingi ya dunia.
Ufunuo wa Yohana 13:8
[8]Na watu wote wakaao juu ya nchi watamsujudu, kila ambaye jina lake halikuandikwa katika kitabu cha uzima cha Mwana-Kondoo, aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya dunia.
And all that dwell upon the earth shall worship him, whose names are not written in the book of life of the Lamb slain from the foundation of the world.


Mungu si kigeugeu, akisamehe anasamehe jumla. Unaposema ni “huruma tuu unamaanisha nini?”
Hili swali lako lieke vizur brother, unaamaanisha mungu hana huruma? Asingekuwa na huruma si angefutilia mbali dunia yote baada ya Adam kuanguka dhambini na kuumba dunia nyingine mpya?

Ukisoma utaona hizi personalities tatu i.e Wafalme, Manabii na Makuhani walikuwa responsible kwa Mungu pekee na ndio waliokuwa wanasimamia uendeshaji wa mashauri yote. Ni utaratibu huu umerithiwa hata leo majaji wanakuwa na immunity ya kutoshitakiwa.
Kwaio unamaanisha Kings, Prophets and Patriarchs had immunity from god 😅 😅
God treats all people equally and the punishment is equal for all people, who is not biased.

Una ushahidi wa maandiko kwamba shetani alikuwa na chance ya kuomba msamaha au again ni hisia zako tu?
Romans 3;23-24
Kila kiumbe mungu alichoumba kinaweza kuomba msamaha na kusamehewa, ni haki kila kiumbe, hata lucifer mshtaki wetu had that opportunity and wasted it, this is very simple to understand, sidhani hata kama inahitaji hata bible verse.

Umenena vyema.
 
Unajiabisha brother, umeleta mafungu yanayokuumbua, hapa mungu kabisa anasema anamlaaniwa mtu na sio ardhi.
Nimekuwekea mstari wa 11 na 12 ili upate context, mstari wa 12 ndio unao zungumzia “barreness” (not henceforth yield unto thee her strength). Mungu alipoumba ardhi ilikuwa fruitful na anaposema haitazaa matunda kwa ajili yako, hiyo unaitafsirije achana na issue za kiebrania, lugha ya kawaida tuu hiyo siyo cursing?

Brother Adam hakufa??
Mungu alimwambia "Hakika utakufa" na Adam alikufa hata kama aliishi miaka 900 mwisho wa siku ahadi ya mungu ilitimia.
Ni wapi nimesema Adam hakufa? Hata huo mstari niliokuwekea unaeleza aliishi miaka 900+ akafa. Nilichokuwa nakuonesha ni utofauti wa neno kufa kwenye kitabu cha mwanzo na neno hilo hilo kwenye kitabu cha walawi nilichonukuu kwamba ukiua nawe wapaswa kuuliwa pindi tu itakapo thibitishwa, hivyo neno kifo lina maana tofauti kwenye vitabu hivyo.

Kwaio unamaanisha Kings, Prophets and Patriarchs had immunity from god [emoji28] [emoji28]
God treats all people equally and the punishment is equal for all people, who is not biased.
Sijazungumzia immunity from God, nimesema walikuwa responsible kwa Mungu i.e hakuna wa kuwawajibisha kwa mujibu wa sheria except God himself na ndio maana wao walikuwa na nafasi ya kumlilia Mungu awasamehe.

Lastly, nadhani ni vizuri ukasoma ili uelewe kuliko kusoma ili ujibu, hii inaweza kukufanya kumiss out the context.

Mijadala kama hii ni kwa ajili ya kujifunza na kupeana elimu hivyo nadhani si vema kutumia lugha za kejeli ambazo zinaweza kufanya mtu akaacha kuconcrtrate kwenye hoja ya msingi unayo present na pia inaweza kufanya wasio amini wakose cha kuwashawishi toka kwetu. Bible inasema, we have to copy Christ. Pamoja na kejeli, dhihaka nk bado alipofungua kinywa kuongea hakuwa na jazba.

Otherwise nikushukuru kwa kuchangia na issues zote ulizo raise, naamini nimejitahidi kujibu hoja zako.
 
Umenena vema kabisa. UJUMBE mzuri sana
 
Romans 3;23-24
Kila kiumbe mungu alichoumba kinaweza kuomba msamaha na kusamehewa, ni haki kila kiumbe, hata lucifer mshtaki wetu had that opportunity and wasted it, this is very simple to understand, sidhani hata kama inahitaji hata bible verse.

Ukisoma hiyo mistari na sura ya tatu toka mwanzo utaona Apostle Paul anazungumzia issue ya grace (neema) kwa wale walioishi under the law (jews) kwamba kwao haki ilipatikana kwa kutimiza matendo ya sheria.

Inaendelea kuwa sheria haikuweza kuleta haki bali ilizaa dhambi nayo dhambi ikazaa mauti, lakini haki anayoihubiri Paul inatokana na neema (grace) kwa kuwa chini ya sheria hakuna aliyeweza kupata haki bali wote walipungukiwa na utukufu wa Mungu ndiyo maana wanahitaji haki ipatikanayo kwa njia ya imani. Na haki hiyo inapatikana through Jesus (the second Adam) who came to restore the glory lost in the garden by the first Adam.

Ukisema shetani anaweza kutubu na akasamehewa maana yake bible inajipinga na kusema uongo. Ukisoma kitabu cha ufunuo utaona adhabu ya shetani na other angelic beings imeshasemwa kuwa watatupwa katika ziwa la moto siku ya hukumu meaning they have zero chance of repentance na ndio maana shetani yuko busy kulaghai watu waunganr naye kwenye adhabu ya milele.
 
Je huyo mungu hakujua kuwa shetani angewalaghai watu wake na akamteketeza kabisa asije duniani?
 
Barikiwa mkuu
 
Mungu wa yakobo,mungu wa israel, mungu wa isaka, ...waraka kwa wakorinto,waraka kwa wakolosai,na mengine yanayofanana na hayo yanatuhusu nini sisi wachaga? Et yanawahusu nini wasukuma? Mbona hakuna waraka kwa wakurya? Mbona hakuna mtume kutoka kwa wanyaturu? Mbona hakuna mungu wa ibenge, mungu wa mwigulu,mungu wa shayo kwenye biblia? Mbona wagogo hawatajwi kwenye biblia,? Kwanini wanyakyusa hawapo kwenye biblia takatifu?
Vinginevyo tumenasa kwenye mtego la sivyo tutaangamia kama sio tumeshaangamia,
 
Kuna mitume kutoka kila jamii. Mungu ni Mungu wa adam baba wa watu wote. Anyway Assnte kwa maoni
 
Sasa Mkuu mbona Kuna taarifa kwenye bibilia zinaonesha wazi kwamba mwisho wa Dunia ulishatukia Sasa habari kama hiyo sisi inatuhusu kweli?
 
Wewe unaogopa kifo hii iko wazi ukiyasoma haya maneno kama sio mvivu wa kufikiri, nikwamba huyu alieandika naye alikuwa anahofu ya kufa, kwahyo waliokubali haya maneno ni waoga pia,
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
 
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
Hao ndo akina nani? Ni akina nyani au akina kuku? Au akina nzi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…