Mambo ya kuzingatia katika safari za maisha yako hususani kwa sisi vijana

Mambo ya kuzingatia katika safari za maisha yako hususani kwa sisi vijana

Hakikisha haya mambo yanakua Siri kwako;

1. Masuala ya mahusiano yako
2. Hali yako ya kifedha
3. Matatizo ya familia yako
4. Siri zako binafsi
5. Baadhi ya Mipango yako mikubwa na midogo pia
6. Hatua yako inayofuata
Mengine tuendeleze kwenye comment
Ndoto zako
kuna vijana kinachowakwamisha kufanikiwa ni ndoto zao wenyewe. haiwezekani kitu hata hujakianzisha unaanza kufikiria kupata wateja wa kontena 100. kuna jamaa angu hapa yeye ana plan ambazo ataziongea kwa Elon Musk tu. Mi nadhani huyu si pumbaf tu kama kenge wengine... Elon musk ataonana nae lini?
 
Sawa tunapaswa tuwe na mipango mikubwa ila tupunguze expectations pia
Tukubali kuanza na kidogo yani kutumia ulichonacho kutafuta usichokua nacho
 
Tatizo ujuaji mwingi vijana hawakubali kujilekebisha kwenye mambo ya msingi
Watanzania wengi ni wajuaji sana ..ni bora uwe mjuzi wa vitu vingi ila uwe na hekima ya kujua mahala sahihi pakuzungumzia mambo.
Kuna mbaba mmoja niliwahi mbishia jambo ambalo nilikua sahihi tulikua kanisani kwenye darasa la mafundisho ya Biblia ,tulivyotoka pale akaniambia mimi mjuaji mpaka...muda mwingine ukieleza ukweli binadamu wanakuita mjuaji
 
Sawa tunapaswa tuwe na mipango mikubwa ila tupunguze expectations pia
Tukubali kuanza na kidogo yani kutumia ulichonacho kutafuta usichokua nacho
Don't plan impossible. Hakuna muujiza wakuu.... Kam umeshindwa kufanya kitu hata maxience melo akakuona na kukuhitaji kwa jf yake utafanya nn kwa Elon musk?
 
Hali yako ya kiafya.
1. Unywaji wa pombe kupitiliza hasa hiz pombe zisizo na kiwango na za bei rahisi.

2. Ngono zembe na magonjwa ya zinaa.

3 .ulaji wa ovyo hasa wa mavyakula ya wanga na nyama nyekundu kupitiliza.

4. Kujitwika stress hasa za mapenzi na za kujilingalisha na waliokuzid kiuchumi.

5 . Kujali mda na kuwa mwaminifu kwako na kwa wengine.

6 . Kuheshimu ushauri mzuri kuhusu mienendo yako mibovu hasa kwa kutoka kwa wazaz wako na jamii iliyokuzunguka.

7 . Kuhonga mwanamke asie mke wako huku ukijifanya una hudumia wakati hauna mzunguko wa faida ya laki tano kwa siku , hii ni yakuacha haraka sna.

8.kuongeza maarifa kwa kujisomea na hata kwa tembelea maeneo mbalimbali ya hii dunia ili kujifunza .

9. Kuacha kujifanya unajua siasa na kujifanya unaandamna ili kuisaidia tanzania wakati taifa linatatizo kubwa la kimaadili kwanzia ngazi ya familia.
Hii namba Tatu nifafanunulie na hatari ya hiyo nyama na ulaji mwingi ni kuanzia kias gani
 
Hii namba Tatu nifafanunulie na hatari ya hiyo nyama na ulaji mwingi ni kuanzia kias gani
Kula kwa kiasi na kwa afya pia ..vyakula vyenye sukari kidogo na protini kwa wingi pamoja na matunda
 
Back
Top Bottom