Mambo ya kuzingatia katika safari za maisha yako hususani kwa sisi vijana

Kanuni yangu maishani ni moja sehemu yoyote ambapo moyo wangu haujatulia na kupata amani staonesha lolote linalonihusu hata kama ni kwa ndugu nione tu natembea navaa ila yanayoendelea akilini mwangu hawatoyajua kamwe

MIMI NI MSIRI HADI NAKERA

nshawekwa hadi kwenye kikao na familia kisa upole na usiri mwingi niwatakie siku njema twende tukaitetee bandari yetu 😀
 
HIYO NI NZURI KAMA UNAWEZA IMUDU
 
Hakikisha haya mambo yanakua Siri kwako;

1. Masuala ya mahusiano yako
2. Hali yako ya kifedha
3. Matatizo ya familia yako
4. Siri zako binafsi
5. Baadhi ya Mipango yako mikubwa na midogo pia
6. Hatua yako inayofuata
Mengine tuendeleze kwenye comment
That's why nipo broke
1. Kila mtu anafahamu nimeoa
2. Familia na marafiki wanajua napokea TGS.....
3. Hivi ushindwe kulipa marejesho ya Oya Microfinance & kausha damu kuna mtu ataacha kujua mtaani.
4. Kama zipi labda
5. Kucheza upatu na vikoba kuna watu kibao, ukitaka kukopa wanahitaji wadhamini then hakuna siri tena.
6. Aaaah......!
 
No.7
Napita tu
 
1.kUTANGAZA MASUALA YA MAHUSIANO YAKO
Hii haikumaanisha kujua status kwamba umeoa au umeolewa,hii imelenga watu ambao wanapenda kuongelea masuala ya mausiano yao mfano mwanaume kutangaza madhaifu ya mke wako kwa watu
 
2. WATU HAWATAKIWI WAJUE KIPATO CHAKO
Mfano mimi kuna watu wanapendaga kujua kipato changu cha mwezi ni kiasi gani, hili swali wanawake wanapenda sana kuniuliza ila huwa nawajibu kwa kuwatania 'napata elfu 60 ndio maana sitaki kukuoa maana ntakutesa''
ninachotaka kusema hapa ni tafta namna ya kuwepa kujibu maswali yanayokuhusu wewe
3. UKIHITAJI MKOPO TAFTA WATU AMBAO UNAWAJUA WATASTAHIMILI HATA UKICHELEWA KULIPA
4.SIRI ZAKO BINAFSI
Mambo mabaya yaliyokutokea zamani
Mipango yako midogo
Kutoa misaada ya nguo au kifedha kwa watu
 
Pesa ni kitu kingine,
Unaona mtu ana gari ,kavaa suti mfukoni ni empty ( Hana cash) ,anaishi nyumba nzuri.
mwambie nipe Laki moja baada ya miezi mitatu nakurudishia Hana.
Uwezo wa kutoa Laki ikakaa nje miezi mitatu ,hiyo ability Hana.
Wanaojua pesa watanielewa.
 
Jamaa ukoserious sana hebu relax furahia maisha
 
 
Nyama nyekundu haina tatizo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…