Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
🤓🤓🤓😂😂🤝🤝Daaah maisha bhana unawaza jinsi ya kukaa kwa mtu kweli?
......ni kweli hili nalo mkalitizame, ingawa huwa naona mdada akipandisha miguu kwenye sofa ni sawa ila sio mindulu.......Umesahau ,usiweke miguu juu ya kochi
broo yeye yukowa mdahuo?Mimi nipo kwa bro hapa, najiachia kinoma noma, nasubiri game ianze nichukue rimoti kwa shemeji, niweke game, tamthilia ataangalia siku nyingine.
Kuliko kukaa kwa ndugu ni bora nikabanane kwa mshikaji kisela huku naendelea kujipanga mambo yangu🤓🤓🤓😂😂🤝🤝
Na unajiwekea na condition kabisa
📌📌📌📌📌1. NJOO NA MAHITAJI YAKO MADOGODOGO
Njoo na mswaki wako, sabuni yako ya kuogea na dawa yako ya mswaki, taulo na mahitaji yako mengine madogomadogo. Kuna wageni wanaomba hadi nguo za...kwa wenyeji sio vizuri.
2. USIFUNGUE FRIJI WALA MAKABATI
Usifungue friji ya wenyeji au makabati bila kuambiwa ufanye hivyo. Mgeni unasikia kiu omba maji kwa wenyeji sio unaanza kufungua friji bila ruhusa eti unatafuta maji ya kunywa. Ukihitaji kitu omba kwa wenyeji sio kuanza kupekuapekua.
3. USIBAKI SEBULENI
Wenyeji wakiingia kulala usibaki sebuleni unatazama TV ingia chumbani kwako. Sambamba na hilo mkiwa mnatazama TV sebuleni usianze kushika rimoti na kubadili channel bila ruhusa ya wenyeji.
4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.
5. USIINGILIE MAZUNGUMZO
Ikatokea wenyeji hasa mke na mume wana mjadala wao wa mambo yao binafsi usipende kuingilia na kujifanya mshauri bila kuombwa kufanya hivyo. Labda wanapanga wapike nini siku hiyo mgeni usharukia kuchagua chakula kaa kwa kutulia. Katika jambo lolote wanalojaldili subiri uombwe ushauri.
6. USITEMBELEE MAJIRANI
Usitembelee majirani "ooh jamani mie ndo mpwa wa huyu jirani yenu nimeona niwasalimie".... Pata ruhusa ya wenyeji wako kwanza kabla hujaanza kuzunguka kwa majirani. Sambamba na hilo usilete wageni hapo ulipofikia bila kumtaarifu Mwenyeji wako.
7. KULA VYAKULA VILIVYOPO
Jitahidi kula chakula kinachowekwa mbele yako na kama vinakupa shida basi nunua hivyo vyakula sio "ooh maharage yananiumiza tumbo" kanunue nyama ulete wakupikie.
8. USITUMIE VIFAA VYA WENYEJI
Usianze kutumia vifaa vya wenyeji bila ruhusa mfano unaanza kuwasha computer au vifaa vya mazoezi . Usianze kuzunguka nyumba na kuingia kila mahali labda mwenyeji wako akuoneshe sio kukagua nyumba nzima na kuingia vyumba ambavyo hujaambiwa.
9.SAIDIA KAZI
Tandika kitanda chako na safisha chumba ulichopewa kulala. Saidia kazi za hapo nyumbani ulipofikia labda wakukataze wenyeji. Sambamba na hilo utakapoondoka acha chumba katika hali ya usafi kama ulivyokikuta.
10. USIJE MIKONO MITUPU
Usije mikono mitupu beba zawadi kidogo kwa wenyeji wako.
Tukutane Taifa Yanga anapiga mtu 2 bili
Mweee nilichogundua humu watu wana roho ya ubinafsi tuuSiku zote ukienda mjini nenda na nauli yako. Jitahidi pia uwe na hela yako ya lodge. ukienda kwa ndugu nenda kusalimia. Nakuhakikishia, wakijua umefikia lodge, maneno yatakuwa mengi..ohh unajua siyo vizuri..kufikia lodge wakati sisi tupo hapa. Lakini deep down watafurahi na watakupa heshima yako stahiki.
niliacha kufikia kwa ndugu baada ya kuingia Chuo. nikiwa Mjini na nikiwa na mda ntaenda kusalimia. Kama nimetingwa tutapigiana simu. Maisha yanaendelea.
avoid sana kuwa mzigo kwa watu. Kila mtu anaishi kwa bajeti yake. Halafu Mimi ninavyo thamini privacy yangu….aiseee siyo rahisi kutimba kwa mtu na mabegi. Hata kama ni lodge ya elfu kumi but sitaki kuwa msumbufu kwa ndugu.
Daaah ndugu HAPANA bora hata kwa mtu baki kuna uhuru fulani ukakua nao sio nduguKuliko kukaa kwa ndugu ni bora nikabanane kwa mshikaji kisela huku naendelea kujipanga mambo yangu
Daaah ndugu HAPANA bora hata kwa mtu baki kuna uhuru fulani ukakua nao sio ndugu
Nimewahi kaa kwa ndugu kama mwezi mmoja hivi aise sitorudia tena ..Ndio maana Mimi Kwa NDUGU SIENDIIII NG'OOOOOO
#YNWA
Na sote tuseme ameeen🤣🤣🤣🤣🤣🤣Kifupi mgeni usije tuh
Kwa ndugu mambo mengi..Aise HAPANA hata kama ana roho nzuri kiasi gani siwezi kaa kwa ndugu zaidi ya siku 1 ..yani naingia jion asubuh mapema naondoka tena hapo ikinilazimu sana kulala
.......na ikitokea chakula kimetengwa kwenye hotpots na ukapewa nafasi ya kwanza kujisevia basi consider kwamba mko wengi .......jikadirie kidogo sio unachota nyama zote hadi watoto wa mwenyeji wanakosa wanaanza kumegana......mkimaliza kula basi anza hata kuwanawisha mikono wenyeji waliomaliza kula, yaani usijikute we ndo mgeeeeeeni, kila kitu ufanyiwe.....hawatakumiss ukiondoka......11. Unapokula, kula ukiwa unaangalia chakula kilicho mbele yako acha kuangalia Cha upande wa mwenzako alafu tafuna kistaarabu ukiwa umefunga mdomo acha kutafuna kwa fujo kama mashine huku mdomo umeacha wazi.
12.ukikaa kaa kistaarabu usipandishe miguu kwenye kochi.
13. Unapoongea na wenyeji acha kuongea ukiwa unachati kweny simu yako, weka simu pembeni bundle yenyewe ya mawazo boya wewe
Mimi mara nyingi nilikua sili ..nikirud nawaambia nishakula naenda tu kulalaKwa ndugu mambo mengi..
Kujistukia sana yaani hakuna amani ya roho daah