Mambo ya kuzingatia ukifikia nyumbani kwa mtu

Mambo ya kuzingatia ukifikia nyumbani kwa mtu

1. NJOO NA MAHITAJI YAKO MADOGODOGO
Njoo na mswaki wako, sabuni yako ya kuogea na dawa yako ya mswaki, taulo na mahitaji yako mengine madogomadogo. Kuna wageni wanaomba hadi nguo za...kwa wenyeji sio vizuri.

2. USIFUNGUE FRIJI WALA MAKABATI
Usifungue friji ya wenyeji au makabati bila kuambiwa ufanye hivyo. Mgeni unasikia kiu omba maji kwa wenyeji sio unaanza kufungua friji bila ruhusa eti unatafuta maji ya kunywa. Ukihitaji kitu omba kwa wenyeji sio kuanza kupekuapekua.

3. USIBAKI SEBULENI
Wenyeji wakiingia kulala usibaki sebuleni unatazama TV ingia chumbani kwako. Sambamba na hilo mkiwa mnatazama TV sebuleni usianze kushika rimoti na kubadili channel bila ruhusa ya wenyeji.

4. USIZIDISHE MUDA WA KUKAA
Ukifika ni vizuri uwajulishe wenyeji wako utakaa hadi lini na usizidishe muda labda wenyeji wakuombe wenyewe. Kama uliwaambia utakaa wiki ikifika ondoka sio unasubiri hadi wakuulize unaondoka lini.

5. USIINGILIE MAZUNGUMZO
Ikatokea wenyeji hasa mke na mume wana mjadala wao wa mambo yao binafsi usipende kuingilia na kujifanya mshauri bila kuombwa kufanya hivyo. Labda wanapanga wapike nini siku hiyo mgeni usharukia kuchagua chakula kaa kwa kutulia. Katika jambo lolote wanalojaldili subiri uombwe ushauri.

6. USITEMBELEE MAJIRANI
Usitembelee majirani "ooh jamani mie ndo mpwa wa huyu jirani yenu nimeona niwasalimie".... Pata ruhusa ya wenyeji wako kwanza kabla hujaanza kuzunguka kwa majirani. Sambamba na hilo usilete wageni hapo ulipofikia bila kumtaarifu Mwenyeji wako.

7. KULA VYAKULA VILIVYOPO
Jitahidi kula chakula kinachowekwa mbele yako na kama vinakupa shida basi nunua hivyo vyakula sio "ooh maharage yananiumiza tumbo" kanunue nyama ulete wakupikie.

8. USITUMIE VIFAA VYA WENYEJI
Usianze kutumia vifaa vya wenyeji bila ruhusa mfano unaanza kuwasha computer au vifaa vya mazoezi . Usianze kuzunguka nyumba na kuingia kila mahali labda mwenyeji wako akuoneshe sio kukagua nyumba nzima na kuingia vyumba ambavyo hujaambiwa.

9.SAIDIA KAZI
Tandika kitanda chako na safisha chumba ulichopewa kulala. Saidia kazi za hapo nyumbani ulipofikia labda wakukataze wenyeji. Sambamba na hilo utakapoondoka acha chumba katika hali ya usafi kama ulivyokikuta.

10. USIJE MIKONO MITUPU
Usije mikono mitupu beba zawadi kidogo kwa wenyeji wako.

Tukutane Taifa Yanga anapiga mtu 2 bili
Kazi za jikoni au, sebuleni tunakaa ili kumuwinda house boy/girl, friji ni muhimu kukagua ili tujue nini cha kuongezq kwenye friji,nimetoka seminar nakuja na zawadi gani mm mwenyewe ni zawadi tosha kwao na wanishukiru sana, nisitumie vifaa vya wenyeji yaani hata ndoo ya kuoga na dodoki nije navyo basi nitakuwa ni mkimbizi, taulo ni kanga ya house girl/boy,majirani muhimu kuwatembelea ili kujua tabia na mwendo wa mwenyeji wangu ili nipeleke taarifa kijijini,kama ndo nawakuta Wana Hali mbaya na Mimi ndio mwenye hela kwanini wapate shida nakaa nao mpaka wapate hela.
Ukifika kwa mwenyeji wako vaa bukta na singlend kama ni Dsm ili upate hewa vizuri.Niwashukuru kwa kunisikiliza
 
Kwakweli hiki kipengele cha ugeni kwangu huwa ni changamoto kiasi naonekana nna roho mbaya....

Hivi serious mgeni unakaa kwangu miezi 3+ halafu bado unataka nikutreat kama mgeni nikuandalie sijui maji nikuletee msosi chumba kwako nikusafishie chumbani??? Hapana sina huu muda treatment za hivo utazipata within a week kama tofauti na hapo nna roho mbaya basi sawa.
😀😀😀😀
 
Hiyo namba 3 ilinikuta. Nilipata mgeni ndugu yangu tena mpaka mume wangu akawa uncomfortable nyumbani kwake. Kitoto kinakaa miguu juu sebuleni kimeshikilia remote. Mr anaishia kukaa dining. Mnaenda kulala bado busy na tv na usipomfuata akalale atakesha. Kwakweli kuna baadhi ya wageni wanakera na wengine unatamani wasiondoke.
 
11.Mgeni usitongoze msichana wa kazi wala ndugu wa mke/mume wa mwenyeji wako utaaibika.
Tuliza nyege zako mwenyewe kabla hujatulizwa.
Hpo sasa ndio shughuli...mm nikikuta housegirl mwenye tako huwa simuach sslama
 
Binafsi huwa nasafiri mara nyingi mikoani ila huwa napenda uhuru ninakofika. Kama kuna ndugu nitaenda kumsalimia mchana halafu namdanganya kwamba kuna kazi ya kuandaa report usiku wa leo nipo na wenzangu, nikitoka hapo naenda kuginda pombe nikichoka naenda kulala lodge kwa uhuru hata nikifika saa tisa usiku sawa tu.

Sema kuna siku pale Mwanza nilimdanganya hivo mwenyeji wangu kisha nikapanda boda nikaenda mbali Bundesliga huko kunywa bia, nauli tu ya boda 3000. Bahati mbaya tena tukagongana na mwenyeji wangu, kumbe na yeye anapiga maji kajifunzia mjini. Ile siku tulifurahi sana maana ilibidi nimwambie ukweli kwamba mimi napenda uhuru ndio maana huwa sipendi kulala kwa ndugu kokote niendako. Pale tulipiga maji ikabidi nimrudishe nilikofikia kuendelea kula maji.
 
Binafsi huwa nasafiri mara nyingi mikoani ila huwa napenda uhuru ninakofika. Kama kuna ndugu nitaenda kumsalimia mchana halafu namdanganya kwamba kuna kazi ya kuandaa report usiku wa leo nipo na wenzangu, nikitoka hapo naenda kuginda pombe nikichoka naenda kulala lodge kwa uhuru hata nikifika saa tisa usiku sawa tu.

Sema kuna siku pale Mwanza nilimdanganya hivo mwenyeji wangu kisha nikapanda boda nikaenda mbali Bundesliga huko kunywa bia, nauli tu ya boda 3000. Bahati mbaya tena tukagongana na mwenyeji wangu, kumbe na yeye anapiga maji kajifunzia mjini. Ile siku tulifurahi sana maana ilibidi nimwambie ukweli kwamba mimi napenda uhuru ndio maana huwa sipendi kulala kwa ndugu kokote niendako. Pale tulipiga maji ikabidi nimrudishe nilikofikia kuendelea kula maji.
Hyo nzuri sana...unatembelea mule muleee chief
Siku nyingine ukija mwanza tuchekiane
 
Umesahau moja.
Usitembee na mke/mume wa mwenyeji wako hata Kama ajirahisishe kivipi.
 
Imeandikwa:

1. “Upendo husitiri wingi wa makosa!”

2. “Iweni wakarimu kwa wageni maana wengine hukaribisha Malaika wa Mungu kwa kule kukarimu kwao wageni”
 
Back
Top Bottom